Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

JAMANI BABA MKWE!

PART: 11

Iliposhia, mwanangu kwa taarifa hii nzuri sana. Nikiuza mihogo yangu lazima nikupe zawadi”

Getruda alimwambia Mwajuma.

Baada ya kupata kizima, alitoka ndani kisha akaelekea kwa  Rose huku akiwa anatokwa na machozi kama mtoto mdogo.

SONGA NAYO.

Baada ya kukaribia kwenye mlango wa mkanwana wake, alianza kupangusa machozi ili aweze kuongea naye vizuri japo sura ilijionesha hadharani kama mtu mwenye hasira kali.

“Hodii…hodii..”

Mama mkwe wa Rose alibisha

“Nani..unayebisha hodi?”

Rose aliuliza huku akiwa anawasiwasi

“Ni mimi mama mkwe wako..”

Bi Getruda alimjibu

“Ohh..kumbe ni wewe mama..karibu sana”

“Asante ila nakuomba kwa nje hapa tuongee mawili matatu mwanangu”

“Sawa mama naja sasa hivi”

Rose alijibu huku akiwa anatetemeka.

Akiwa amemsubiria mkamwana wake, alianza kuwaza nini amwambie kwa wakati ule kwani kichwa chake kilichanganyikiwa kabisa mara baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Mwajuma.

Akiwa bado anaendelea kufikiria nini amwambie, Rose alifungua mlango kisha akamfata huku akiwa amejifunika kiremba kichwani.

“Habari za siku mbili tatu mtoto wangu?”

Bi Getruda alimuuliza Rose

“Nzuri mama…za msibani”

“Msibani wapowapo japo nimetoka mapema kutokana na taarifa mbaya juu ya vitendo vyako viovu ambavyo havijawahi kutokea kabisa. Ni aibu kubwa sana mpaka nashindwa nikufanyeje! . Wewe mtoto!, unamatatizo ya akili au ndio tabia zako hata kipindi ukiwa nyumbani?  sasa kwa ulichokifanya siwezi kukubali kabisa kama unataka wanaume basi niachie mtoto wangu Baraka wewe  nenda ukaishi na baba yako huyo.

Unanitia kichefuchefu kabisa yaani sitaki hata nikuone kwenye macho yangu”

Bibi Getruda alimwambia Rose kisha akajikuta machozi yanamchuruzika huku hasira zikiwa zinampanda.

“Samahani mama, taarifa hizo ni za uongo kabisa. Wanafanya hivo ili kututenganisha katika familia yetu ambayo ina upendo wa kila aina. Tangu uondoke sijawahi kwenda kwa Mzee wala mzee hajawahi kuja kwangu. Nakuomba kupuuza taarifa hizo tena ni mzee akirudi muulize akupe majibu. Nyumbani tumelelewa kwenye maadili ya dini na kumuogopa Mungu ambaye ndiye mkuu wa kila kitu. Siwezi kuongea mengi lakini ukweli ndio huo mama yangu”.

Rose alimjibu Mama mkwe wake

“Hivi wewe ni kichaa? au unahisi nimemurupuka mpaka nakwambia maneno haya? . Kwa taarifa yako ushahidi wote ninao kuanzia mwanzo unaingia na wakati unatoka bila kusahau kanga uliyokuwa umevaa.

Kwa kuwa umeleta kiburi na uongo, nakuomba kabla mwanangu hujamuangamiza ujitoe mwenyewe kabisa nasi kesho tutaenda mpaka nyumbani kwenu na ushahidi wote kisha tuwakabidhi mtoto wao”

Bi Getruda aliongea kwa hasira huku akimnyooshea kidole.

Mara baada ya maneno hayo, Rose aliishiwa nguvu kabisa kama kijana aliyevusha lakini jogoo wake akamsaliti. Bi Getruda aliondoka huku akimsihi Rose kukusanya kila kilicho chake kabla ya Baraka kufika maana mama alijua vizuri balaa la mwanaye huyo.

Baada ya kuka kijiweni kwa mda, Mzee matofali alianza kuumwa na njaa huku mifuko yake ikiwa imetiboka kabisa na ndipo alipoanza kurejea nyumbani huku akiwa ana majibu mara mabili eidha siri imetunzwa au kimesanuka. Alitembea kwa kinyong’onyea kwelikweli kisha akafika maeneo ya nyumbani kwake.

Ukimya alioukuta nyumbani hapo, ulimpa matumaini makubwa na kuanza kujifariji kuwa siri haijafichuka.

Alitembea taaratibu kisha akaingia ndani ambapo alimkuta mkewe akiwa amkekaa kwenye mkeka huku akionekana mwenye hasira.

” Mke wangu mbona unaonekana mwenye kuhuzunika?. Nini kimekupata mke wangu kipenzi..”

Matofali aliongea kwa upole

” Naomba uende kwa mke wako!!….Nenda kwa mke wako sasa hivi kabla hatujauana ndani.. wewe mzee huna hata aya!…muone ndevu kama magamba ya mamba. Hujiheshimu wewe! naomba uondoke ndani humu kama ni chakula changu hakuna kula na kama ni kulala utajua utakapo lala. Kama hutaki ngoja Baraka aje afu uone tutakachokufanyia. Yaani huyo si mjukuu wako! utaongea nini kwa wazazi wake ! jamii unaifundisha nini! mzee jina tu lakini akili hovyo kabisa”.

Baada ya kuambiwa maneno hayo, Mzee Matofali alishikwa na aibu kali sana kisha akatoka nje kimyakimya huku akiwa anapiga miruzi . Baada ya kutoka nje, mke wake alifung mlango kisha akashika simu yake kumpigia  Baraka ili awahi kurudi nyumbani.

Kama kawaida yake, Mwajuma alikua mazingira yakaribu akizikusanya huku akijifanya kuosha vyombo karibu na eneo la tukio.

Rose alichungulia na kumuona Mwajuma kisha akatoka ndani ma kisu kikali kwani hakuwa na ujanja wowote kama ni siri basi ilikuwa tayari imeshatibuka.

Akiwa anaosha vyombo, alimuona Rose akiwa tayari ameshamkaribia huku akiwa ameshika kisu mkononi…

JE ITAKUWAJE?

BARAKA ATACHUKUA MAAMUZI GANI?

MATOFALI ATALALA WAPI?

PART: 12

Ilipoishia, Rose alichungulia na kumuona Mwajuma kisha akatoka ndani ma kisu kikali kwani hakuwa na ujanja wowote kama ni siri basi ilikuwa tayari imeshatibuka.

Akiwa anaosha vyombo, alimuona Rose akiwa tayari ameshamkaribia huku akiwa ameshika kisu mkononi…

SONGA NAYO..

Ama  kweli  unaweza kufanya majaribio ya vitu vyote lakini sio kwenye uhai wako. Baada ya kumuona huku akiwa ameshikilia kisu hicho, Mwajuma alitimua mbio kali sana mithili ya swala anayefukuzwa na simba.

Kwa kuwa Mwajuma alikuwa kimbaombao huku kifuani ndala zake ndefu zikiwazinajigongagonga kama makofi, aliweza kumuacha mbali sana binti Rose huku wakanza kurushiana maneno mpaka majiirani waliokuwa karibu wakaweka mikono yao midomoni huku wakifumba macho kutokana na ukali wa maneno hayo.

“Malaya wewe mtembea na baba yako tena mchana kweupe kabisa…umelaaniwa mbuzi wewe. Ila utaondoka labda sio mimi. Nitakutangaza mtaa mzima maana umeona wazee wetu wa busara uwaambukize laana zako mbuzi wewe”

Mwajuma ndala ndefu alipaza sauti .

“Mbona unaongelea mbali…kaone tako kama bati, maneno mengi na umbea ndo maana hata hunenepi. UKIMWI unakusumbua kazi yako kujiuza ndo upate hata hela ya kununua mihogo…ila omba nisikukamate yaaani nitakuvunja mifupa yako hiyo! mshenzi wewe!”

Rose alimjibu Mwajuma huku akiwa ameanza kutembea kurudi chumbani mwake.

“Heeh…hayo maneno niliyosikia ni kweli! au  ni ugomvi wenu? huyu binti si ameolewa juzijuzi tu! hata miezi 3 bado sasa kutoka na Baba mkwe wake ni laana isiyo sameheka kabisa. Tangu nimekua mpaka umri huu, sijawahi kuona tukio kama hili”

Bibi Coletha aliongea huku akiwa na majirani wengine.

“Unafikiri nawadanganya! ni ukweli mtupu na ndicho chanzo cha ugomvi na mimi. Sasa namsubiri mme wake afike ili nimpe mkanda mzima”

Mwajuma aliwajibu huku akiwa anawaonesha video ya Rose akiingia na kutoka kwa baba mkwe wake akiwa amejifunga kanga tu iliyokuwa imemshika kweli.

Baada ya kuwaonesha video ile, watu walimuomba sana awatumie na kwasababu Mwajuma alikuwa na hasira na Rose, aliwatumia wote huku wengine wakiwa wanadiliki mpaka kumpatia hela ya bando.

Ama Kweli kumchokoza Mwajuma ujue utapata taabu sana yaani ni kama kumchokoza (kigogo 2014 wa twiter).

Video ile ilisambaa sana hasa kwenye magrup ya wasap huku wengine wakaanza kuipost instagram na kujizolea commnt na likes zakutosha.

Rose baada ya kuona Mwajuma amezungukwa na watu wengi, aliona aibu kali sana huku akiwa hajui hatima yake ni ipi .Aliendelea kutembea kuelekea chumbani mwake kisha akajifungia ndani.

Baada ya mda mfupi, aliwasha data kisha akaingia wasap na ndipo alipokutana na clip iliyoonesha sura yake huku akiwa amevalia kanga.

“Loo..!! mambo gani haya !! yaani kumbe mpuuzi huyu alinirekodi mpaka video! (NAFA)”

Rose alianza kutokwa na machozi huku akiomba sana wazazi wake na mme wake wasiweze kuziona.

Baada ya clip hiyo, Rose alijiondoa kwenye magrup yote ya wasap kama njia ya kupunguza uchungu kisha akalog out instagram yake. Aliwaza sana lakini ndo hivo kwa bongo  clip kama hiyo ikovuja, wazee wa connection wanaipata mapema kabisa.

Bibi Getruda naye alianza kuandaa mazingira yakuhakikisha Mzee Matofali haingii kwenye chumba hicho.

Mda uliendelea kutaradadi na ilipofikia mida ya saa kumi na moja za jioni, Baraka alitumiwa clip ya rafiki yake Juma kisha akamwambia ameikuta kwenye Gruop la burudani na udaku.

“Heehee!!” Baraka alibaki mdomo wazi huku akiwa haamini kabisa alichokiona kwenye clip hiyo.

Alijiuliza masawali mengi sana kisha harakaharaka akafunga ofisi kwani mda wa kazi ulikuwa tayari umeshafika .

Alijikuta anaanza kutokwa na kamasi puani huku ndita zikianza kumchora usoni.

Baada ya kufunga ofisi, alimuita boda kisha akapanda kuelekea nyumbani huku akiwa hajielewi kabisa..

JE ILIKUWAJE?

PART: 13

Ilipoishia, Heehee!!” Baraka alibaki mdomo wazi huku akiwa haamini kabisa alichokiona kwenye clip hiyo.

Alijiuliza masawali mengi sana kisha harakaharaka akafunga ofisi kwani mda wa kazi ulikuwa tayari umeshafika .

Alijikuta anaanza kutokwa na kamasi puani huku ndita zikianza kumchora usoni.

Baada ya kufunga ofisi, alimuita boda kisha akapanda kuelekea nyumbani huku akiwa hajielewi kabisa..

SONGA NAYO…

Ama kweli hata ujigalagaze kwenye udondo au utoe machozi ya kujaza bahari nzima lakini haitokuja kutokea ngoma ya watoto kukesha.

Unaweza kuchezea kila kitu namna ujuavyo lakini usije ukathubutu kuchezea mitandao ya kijamii hata siku moja .

Baada ya msala huo, Mzee matofali aliingia kwenye wakati mgumu huku njaa ikiwa imeanza kumtafuna tumboni mithili ya mchwa atafunavyo mazao shambani. Licha ya njaa hiyo lakini aliwaza zaidi juu ya wapi atalala na vipi mtoto wake atakavyopokea taarifa hiyo.

Wahenga husema mkubwa hakosei na hata akikosea huwa haadjibiwi lakini kwa mzee huyu mambo yanaanza kwenda kinyume kabisa.

Alijikongoja taaratubu huku suruali yake iliyokuwa na mauamaua aina ya pajama, ilianza kumshuka taaratibu kutokana na mawazo ambayo laiti kama ungepewa uyabebe basi hata kuyanyanyua usingeweza kabisa.

Baada ya mda alifika kijiweni kisha akamkonyeza mzee Moses huku akionesha dalili za kuwa na jambo la falagha.

” Habari ya mda mzee wangu..”

Mzee matofali aliongea huku akiwa anavuta suruali yake

“Nzuri mzee mwenzangu, mbona unaonekana mwenye mawazo? kulikoni au ndo vyuma kukaza mzee wangu..”

Mzee Moses aliongea huku akionesha hali ya tabasamu.

“Mhh..Mzee wangu.., kweli nakumbuka marehemu baba yangu aliniambia kua uyaone …na leo nimeyaona kweli”

“Nini tena mzee? maana sijaelewa chochote kile. Si unajua wengine tulikimbia umande”

“Mzee wangu naomba unisikilize vizuri kisha unipe ushauri wa haraka na wa busara. Aisee ni kama shetani alinipitia nami nikamkaribisha kwenye roho yangu kisha nikajikuta nimetembea na mke wa mtoto wangu Baraka kipindi Baraka yupo msibani na mke wangu. Sasa leo hii habari zimeanza kusambaa huku msambaza habari akiws ni jirani yangu Mwajuma jambo lililomfanya mke wangu kukasirika sana na amenifukuza nyumbani kabisa. Unavyoniona hapa sijala wala sina hata senti mfukoni. Sasa ninaomba unisaidie kumtuliza mke wangu kisha ukaongee na Mwajuma ili asije kumwambia mwanangu”

Mzee matofali  aliongea kwa huruma sana.

“Hee..!! umetembea na mkamwana wako!  makubwa!! kweli walisema tembea uyaone”

Mzee Moses aliongea huku akiwa anatikisa kichwa.

“Sasa hayo ndio sitaki mzee mwenzangu, nimekuja kwako ili unipe ushauri . Hata wewe yanaweza kukutokea hivo usinicheke”

Mzee matofali aliongea.

“Sawa mzee wangu, sasa siku zote mikono mitupu hailambwi na ukitaka kumdanganya mtoto basi mpe pipi. Wanawake akili zao ni kama za watoto hivo nitakukopesha laki moja hii lakini tutandikiana kwani sitaki hata mke wangu ajue, kisha mnunulie kitenge cha 25 na 25 nyinginw mnunulie nguo za ndani, viatu pamoja na kacha ya kuvaa mkononi. 40 tutampa huyo Mwajuma na 10 itakuwa yangu”

Mzee moses alimwambia Matofali.

” Asante mzee wangu kwa ushauri mzuri, sasa nenda dukani ili zoezi lifanyike kwa dakika 10 tu kabla ya Baraka kufika”

Matofali aliongea.

*************************************************************

Ilikuwa mida ya saa kumi na moja na nusu saa za jioni ndipo Baraka alipofika nyumbani kwake kisha akamlipa boda hela yake.

Baadae alitaka kuingia ndani lakini akashindwa huku akiwa na hasira kali za kuua mtu. Ama kweli kwenye mapenzi hakuna cha ndugu wala mzazi.

Aliweka begi lake chini kisha akaelekea kwa mzee wake huku akiwa na mawili eidha afe yeye au afe mzee wake.

Baada ya kufika mlangoni, aliingia moja kwa moja bila kubisha hodi huku akiwa anahema kama mkimbia marathoni.

Alimkuta mama yake akiwa amekaa huku mzee akiwa wala hayupo kwenye mazingira hayo.

“Mama ..mama..yaani mzee niwakunifanyia tukio kama hili! nimeumia sana, nimedhalilika sana, tena mpaka mke wangu alianza kuninyima haki yangu ya ndoa kwa kisingizio eti amechoka kumbe shida ni mzee! sasa mama mda huu naanza na Rose namnyonga kisha Mzee nami nitafuatia. Sioni haja ya kuishi tena kwenye ulimwengu huu wa kishetani. Naomba nikuage kwa maneno haya lakini uwe mwalimu kwa watakao baki”

Baraka alimwambia mama yake

“Mwanangu!..mwanangu!..nakuomba sana mwanangu..usimpige mtoto wa watu wala mzee wako! nakuomba tena na tena. Kikubwa hapa tutampeleka mpaka nyumbani kwao tumkabidhi kwa wazazi wake na tutawaonesha ushshidi wa alichokifanya. Wakati tunafanya hili, na  mzee wako lazima awepo hapo ukweni najua ni adhabu tosha na kama atakaidi basi atafute pa kuishi”

Mama Baraka alimwambia mwanaye huku akiwa amempigia magoti kama ishara ya kumuomba kitu.

“Sawa mama nimekuelewa”

Baraka aliondoka kisha akae chumbani mwake. Wakati anafanya hayo yote, Mwajuma na Aisha walikuwa wanausoma mchezo huku wakitamani kwenda kumpa mkanda mzima lakini waliona kwanza watulie.

“Hodi humu ndani”

Baraka alibisha hodi

“Karibu mme wangu”

Rose aliitikia kisha akamfungulia mlango

Baada ya kuingia ndani, Baraka alijifanya hajui chochote kisha mke wake akamkaribisha chakula lakini Baraka alikataa kwa kudai ameshiba.

“Samahani sana kwa leo sijisikii kula ila leo kuna katuni moja nimetumiwa yaani nimecheka mpaka basi, naomba uwashe data nishakutumia wasap.”

Baraka aliongea kisha akamtumia clip iliyomuonesha akitoka kwa baba mkwe huku akiwa amejigunga kanga iloyokuwa inaonesha karibia viungo vyote

“Waoooh…asante mme wangu ngoja niwashe data”

Rose alimwambia mmewe huku akiwa hajui kama katumiwa clip inahomuhusu yeye.

Baada ya kuwasha data….

ITAENDELEA….

JE MOTO UTAZIMIKA?

JE ROSE ALIJISIKIAJE?

PART: 14

Ilipoishia, Waoooh…asante mme wangu ngoja niwashe data”

Rose alimwambia mmewe huku akiwa hajui kama katumiwa clip inahomuhusu yeye.

Baada ya kuwasha data….

SONGA NAYO…

Baada ya kuwasha data alishangaa kuona clip yake na ndipo alipotamani ardhi ipasuke na kummeza kabisa. Alitumbua macho mithili ya mjusi uliobanwa na dirisha huku akiwa hajui nini mme wake atamfanya.

“Katuni hiyo umeiona?” Baraka alimuuliza huku akiwa amekasirika kweli

Rose hakujibu chochote kile kwani video ilitosha kabisa kujieleza yenyewe huku ikiwa inatamanisha kweli kuiangalia.

“Kwanini unaniabisha kiasi hiki!, kitu gani umekosa kwangu, kila siku unasema umechoka kumbe ndo tabia yako hii! sasa kuanzia mda huu nakuomba ukusanye kila kilichochako ili tukakukabidhi nyumbani kwa wazazi wako. Yaani unabahati sana tena sana kama sio mama kunishauri, mda huu ungekuwa umechukuliwa na wajuba”

Baraka aliongea huku akiwa amemtia jicho kali sana.

Nako upande wa pili kwa wazazi wake Rose, palianza kuwaka moto na ni pale Mzee wake Rose ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya alipoona clip hiyo ikiwa inasambaa mtandaoni.

Alistuka sana kisha akaiangalia mara mbili lakini ukweli ukabaki palepale kuwa ni mwanaye.

Harakaharaka alirudi nyumbani kumuonesha mkewe kwani hakuwa na simu ya whatsap.

Baada ya kufika nyumbani, baba Rose alimuonesha clip hiyo mke wake,

“Hee..!! mke wangu! umeona mwanao alivyonivua nguo leo! nilikwambia mtoto huyu umemlea vibaya sasa ona mambo hayo. Na clip hii imesambaa nchi nzima mpaka ukienda google utaiona. Ni aibu kubwa sana ambayo sijawahi kukumbana nayo”

Baba Rose aliongea kwa kigugumizi.

“Jamani mme wangu..huyu ni mtoto wetu wote na jukumu la malezi ni la kwetu sote wala sio langu peke yangu. Sio tu ameakuaibisha wewe hata mimi ameniaibisha tena mara mbili yako. Hapa tusilaumiane ila tuone tunafanyaje maana kama ni maji basi yashamwagika”

Mama Rose aliongea kwa uchungu.

“Ila na huyu, mzee amefanya mambo ambayo sijawahi kuona kabisa! yaani anaanzaje kutembea na mwanaye?, hii ni laana tena isiyosameheka na inabidi mzee aitwe mpaka hapa nyumbani kisha kamati ya wazee wa busara na ushauri itatoa mwongozo wa  nini afanyiwe. Kama atakataa basi nitajua nini cha kufanya. Hatuwezi kuvumiliana kwenye mambo ya kijinga kama haya”

Baba Rose  alifoka huku akiwa anatokwa na mate mdomoni.

***********************************************************

Baada ya maneno mazito kutoka kwa mme wake, Rose alianza kukusanya nguo zake huku akiwa hajui nini ataongea nyumbani maana baba yake ni mkali kwelikweli.

Wakati anapanga nguo zake, alipata wazo la kutoroka kwani hakuwa na mtoto lakini pia sura yake nzuri aliona itamfanya aweze kupata mwanaume mwingine.

Alishika tama huku akiomba mme wake aweze kubadilisha maamuzi lakini haikuwezekana kwa mda ule na ndipo Baraka alipotoka nje kuelekea kwa mama yake.

Wakiwa wamekaa nje, Baraka na mama yake  walimuona Mzee Moses ambaye alikuwa ametumwa na Mzee matofali ili waweze kuyaongea na kisha wafikie muafaka .

Mzee huyo ambaye ni mtaalamu wa sana wa kuongea, alimpatia mama Baraka Zawadi zilizokuwa zimefungwa kisha akaongea maneno yake mengi mpaka wakashawishika.

Kwa kuwa mzee Matofali alikuwa anahitajika ili waende naye mpaka ukweni, walimtuma Mzee Moses amwambie arudi nyumbani huku wakimsihi kuwa  tayari wameyamaliza.

Baada ya jibu hilo, Mzee japo umri ulikuwa umeenda lakini alitimua mbio kwelikweli mpaka akawacha watu midomo wazi huku wakishangaa mbio zake.

“Mama..sasa hapa akishafika nitamkamata afu wewe utaenda na Rose “

Baraka alimwambia mama yake

“Hapana mwanangu..hapa tutakachofanya nikuwafungia kila mtu kwenye chumba chake harafu tutawapigia simu wazazi wake waje hapa”

Mama Baraka alimwambia aliongea.

“Mama usijali..kama ni ulinzi upo na hakuna wa kukataaa. Akikataa mtu atabebwa”

Baraka aliongea kisha akawafuata vijana 4 ambao walikuwa na nguvu kwelikweli.

Baada ya kuwaleta, aliwambia waingie ndani ili mzee asiwe na machale.

Mda si mrefu mzee matofali alifika nyumbani hapo huku akijua mambo yameisha.

Baraka kwa kuwa alikuwa na hasira kweli, aliondoka mpaka chumbani kisha akamtoa nje Rose na begi lake nakumvuta mpaka alipokuwa mzee.

“Samahani mzee kwa unyama ulionifanyia nimeumia sana lakini sitokufanya chochote kwani wewe ni mzazi wangu. Natamka rasmi kuwa huyu sio mke wangu na mda huu tutaongozana naye mpaka nyumbani kwao kisha tutamkabidhi kwa wazazi wake. Kwa kuwa na wewe ni mmojawapo wa wazazi basi nawe unalazimika kwenda ili uwepo kwenye tukio hilo”

Baraka aliongea huku akiwa amemshika mkono Rose

“Hee..!! niende ukweni…hee!! kutafuta nini!”

Mzee Matofali alishangaa kisha akatimua mbio lakini vijana wa kazi waliokuwa wamejificha walimkimbiza kisha wakamleta wamembeba juu kwa juu..

Baada ya kumfikisha, Mama Baraka alimpigia simu mama Rose kuwa wanakuja nyumbani hapo kwani hapakuwa mbali sana kisha safari ya kuelekea kwa akina Rose ikaanza huku mzee Matofali akiwa ameshikiliwa vizuri ili asiweze kuwatoroka….

JE ITAKUWAJE?

PART: 15

Ilipoishia, Baada ya kumfikisha, Mama Baraka alimpigia simu mama Rose kuwa wanakuja nyumbani hapo kwani hapakuwa mbali sana kisha safari ya kuelekea kwa akina Rose ikaanza huku mzee Matofali akiwa ameshikiliwa vizuri ili asiweze kuwatoroka….

SONGA NAYO..

Safari iliendelea ya kuelekea kwa akina Rose huku Mzee Matofali macho yakiwa yamwmtoka kwelikweli mithili ya macho ya paka.  Alijaribu kukupuka lakini wala hakuweza kwani vijana hao walikuwa makini sana.

“Jamani mwanangu…nioneeni huruma, huko mnakonipeleka nitajibu  nini? . Jaribu kuvaa viatu vyangu afu uone kama  vinaweza kukutosha”

Mzee Matofali aliongea huku machozi yakiwa yanamlengalenga.

“Mimi sina ubaya na wewe wala mama hana ubaya na wewe kwani kama kungekuwa na mtu mwenye ubaya, ungekuwa udongoni mda huu. Umeyataka mwenyewe nasi tunakupeleka wenyewe ili ukutane na wenyewe”

Baraka alimjibu mzee wake.

“Tena huna hata haya kuongea haya mbele yetu! msimamo ni uleule tunaenda kuwatambulisha ili muwe huru kabisa. Kama ulikuwa unahofu basi usingethubutu kufanya unyama na laana hiyo “.

Mama Baraka aliongea huku akiwa na hasira kweli.

Nako nyumbani kwa akina Rose,walifanya maandalizi ya kuwapokea wageni wao huku wakiwa tayari wameandaa kamati ya wazee kwa ajili ya kutoa neno na ikiwezekana kutoa adhabu kwa wahusika wote.

Ama kweli kama ni siku ya aibu kwa Mzee matofali na Rose ilikuwa ile. Baba Rose aliandaa fimbo zake 3 nzuri huku akimwambia mke wake kuwa,

“Imeandikwa kwenye vitabu vitakatifu kuwa mtoto usimnyime mapigo”

Mama Rose hakuongea chochote kile kisha akatoka akaenda kupika jikoni kwani katika utaratibu wa jamii hiyo, mwanamke hakuruhusiwa kukaa karibu na wageni hasa wakiume.

Wakiwa wamekaa ndani, gafla walisikia sauti zilizoambatana na kelele na ndipo walipochungulia na kuona kuwa ni wageni wao. Harakaharaka wazee walikaa kwenye nafasi zao kisha wakafungua mlango nakubaki wazi.

Ndani ya dakika kama 4 hivi, Baraka na kikosi chake  pamoja na Mzee matofali walioambatana na Rose na mama Baraka waliwasiri maeneo hayo huku Mzee matofali akiwa anatetemeka kwelikweli .

“Hodi…wa humu ndani”

Mama Baraka alibisha

“Karibu sana ingieni ndani moja kwa moja”

Mzee mmoja aliongea.

“Asante…sasa bila kupoteza mda, mbele yenu naitwa Baraka kijana niliyekuwa nimemuona binti yenu lakini kutokana na kitendo alichonifanyia akishirikiana na mzee wangu huyu, nasema inatosha na leo namkabidhi mikononi mwenu akiwa salama kabisa. Najua  inaumiza sana hasa ukizingatia ni mda mfupi wa takribani miezi 2 lakini sina namna”.

Baraka aliongea huku akiwa anatokwa na machozi.

“Tunashukuru kijana wetu kwa uamuzi wa busara mpaka umeamua kumfikisha hapa akiwa salama kabisa bila alama wala jeraha lolote. Kwa kuwa umeleta lalamiko lako basi nasisi tunalifanyia kazi . Kwa taratibu zetu kama kweli wamefanya laana hiyo, adhabu huwa ni viboko 6 kwa kila muhusika na baada ya hapo watapelekwa kanisani kuombewa kisha watatubu dhambi zao hizo. Sasa tunaanza kusikiliza pande zote mbili ili tuweze kujua kama ni kweli.au sio kweli”

Wazee waliongea huku wakiwa wanapitisha kinywaji kwa mbali.

Baada ya mda, baba Rose alifika kisha akaanza kumcharaza viboko Rose huku akiwa amekasirika sana. Rose alilia sana mithili ya mbwa aliyeungua mkia kisha akamuachia kwa mda.

“Wazee wangu! hapa tunapotezeana mda tu! hawa watu wapewe adhabu kama ilivyoamuliwa kwani ushahidi ninao na wala sitaki kusikia mtu anajitetea. Mzee umenidharirisha sana lakini na mimi leo nitakudharirisha hadharani”

Baba Rose aliongea huku akiwa anatokwa na mate mdomoni.

Baada ya kusikia hivo, Mzee Matofali alibaki na wasiwasi mkubwa huku akiwa hajui nini atafanyiwa…

PART: 16

Ilipoishia, “Wazee wangu! hapa tunapotezeana mda tu! hawa watu wapewe adhabu kama ilivyoamuliwa kwani ushahidi ninao na wala sitaki kusikia mtu anajitetea. Mzee umenidharirisha sana lakini na mimi leo nitakudharirisha hadharani”

Baba Rose aliongea huku akiwa anatokwa na mate mdomoni.

Baada ya kusikia hivo, Mzee Matofali alibaki na wasiwasi mkubwa huku akiwa hajui nini atafanyiwa…

SONGA NAYO…

Ama kweli sheria ni msumemo unaokata mbele na nyuma bila kujali ni nani anakatwa.

Baada ya baba Rose kutoa kauli hiyo, iliamuliwa Mzee matofali alambe bakora 6 za nguvu ili liwe fundisho kwa wengine ambao wanashundwa kujiheshimu.

Kwa kuwa walengwa walikuwa wawili, walianza na Rose ambaye alipokea bakora kali sana iliyofanya makalio yake yawake moto bila hata kiberiti. Rose alilia sana mara baada ya kupokea bakora mbili huku akiweka mikono yake kwenye makalio  hayo kitendo kilichofanya wafute na kuanza upya.

Rose kusikia hivo, alistuka mpaka akajikuta anatokwa na haja ndogo lakini haikuwa sababu ya kumsamehe kwani utaratibu ulibaki palepale. Baada ya kipigo hicho cha mbwa mwizi, alikimbilia chumbani huku akiwa analia na kuchuruzika machozi

Mwenzako akinyolewa basi zako tia maji na ndivo mambo yalivyoanza kumuwakia mzee Matofali.

“Mzee samahani hatuna namna tunakuomba usogee mbele kisha ulale chini kwa ajili ya kupata adhabu yako ya viboko 6 matakoni. Sheria unazijua vizuri, tunakumbushana kuwa hutakiwa kuweka mkono wakati unachapwa mpaka vitimie viboko 6”

Aliongea kijana mmoja aliyeteuliwa na wazee ili kutoa adhabu hiyo.

Baada ya kusikia hivo, Mzee alitokwa na machozi yaliyomfanya mama Rose kuona aibu na ndipo walipoamua kuwaomba watu watoke nje wabaki wazee tu na kijana huyo.

Walitoka nje kisha mzee huyo akapokea mikwaju 3 ya nguvu ns ndipo alipogaragara nakuamua kumuachia kwani wangezidisha  huenda hata kutembea asingeweza.

Mzee Matofali alijipangusa machozi kisha watu waliokuwa nje wakaruhusiwa kuingia ndani.

Baada ya zoezi hilo, kilichofuatia kilikuwa kufanya maagano huku Rose akiwa amekabidhiwa rasmi kwa wazazi wake.

Waliondoka wakarejea nyumbani kisha Mzee Matofali akaandaa tafrija fupi kwa ajili ya mapatano na familia yake.

Walikula wakanywa kisha wote wakawa kitu kimoja kama familia lakini Mwajuma akabaki na wasiwasi mkubwa hasa kwa  mzee Matofali.

Na huko nyumbani, Rose alianza kupauka na uzuri wake ukaanza kupotea huku akianza kujuta kwa nini alifanya kitendo hicho? ama kweli majuto ni mjukuu na adhabu ya dhambi ni mauti.

Baada ya miezi 5 Baraka alioa mke mwingine na ndipo ndoto za Rose za kurudiana na Baraka zilipopotea kabisa.

Mpaka sasa hivi Rose anamiaka 40 huku akiomba apatikane mme yeyote tu ilimradi aolewe kutokana na upweke na masimango anayoyapata kwa jamii inayomzunguka.

************************************************************

HUO NDIO MWISHO WA SIMULIZI YETU

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!