𝗠𝗨𝗪𝗔𝗦𝗛𝗢
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 10
Kesho yake Asubuhi na mapema niliamka nikaswaki na kuoga kisha nikavaa kwa ajili ya kwenda chuoni.
Nilitoka nikafunga nyumba vizuri halafu nikawasalimia wapangaji wenzangu waliokuwa wakiparangana pale nyumbani wote waliitikia vizuri mimi nikaanza kutembea kwa mwendo wa madoido.
Nilifika mbele kidogo nikakutana na baba mwenye nyumba huku akiwa na daftari lake moyoni, alisimama akanitazama
“Hujambo?”
“Sijambo shikamoo baba Raj” nilimuambia
“Marahaba vipi nitamkuta?” aliniuliza swali ambalo sikuelewa kidogo
“Nani?”
“Sebastian” alitamka hapo ndipo moyo unanipiga paah maana sikujua kwamba alikuwa anamtaka wa nini seba
“Mmh hapana hayupo, vipi?” niliuliza
“Jana aliniambia kwamba atakuja Dar maana alikuwa amesafiri kidogo si unajua kwamba kodi imeisha juzi ee?” aliniuliza
“Imeisha????” mimi niliongea kwa mshtuko mno
“Ndio imeisha” alisema “Kwani hujui?”
“Mmh Ba Raj hapana mbona alisema amelipa mpaka mwezi wa sita jamani?” nilimuuliza kwani mimi kwenye malipo sikujua ila Seba aliniambia kipindi cha nyuma kwamba yeye kalipa kodi ya miezi sita
“Mh” alisema mzee na kutoa kidaftari kile akafungua, kutazama hivi kumbe Seba alikuwa amelipia miezi 3 badala ya miezi sita hakika nilipatwa na wazimu usio wa kawaida, mimi pesa ya kulipa sikujua ntaipata wapi nilibaki nimepagawa kabisa
“Sawa mzee wangu mimi nawahi chuo, jioni tutaongea” nilisema huku nikipiga hatua moja mbili tatu kuondoka
Nilimuacha mzee akiniangalia sana lakini sikuwa na jibu hata moja juu yake, Nilijikuta nikitiririkwa na machozi kwanza nikaona kama vile sina akili nzuri
“Hivi Diana kwanini siku hizi unawashwa kwa haraka hivi?” niliiuliza nafsi yangu mwenyewe na kujipa majibu “Hapana nina pepo sasa Ibra naye nilimruhusu wa nini aje eeh?” nilizidi kujiuliza
Nilianza kujutia huku nikijisemea bora jana yake nimemuambia Ibra kwamba asije kabisa hata hivyo nilihofia lakini nilijitia moyo huku nikishuka kwenye pantoni katika feli
Nilitembea mwendo wa haraka haraka na kwenda mpaka chuo nikaingia darasani na kuketi pembeni mwa Aisha
“Mambo” niliongea kwa sauti ya kunong’oneza maana mwalimu alikuwa akifundisha
“Safi” aisha alinijibu na kuandika katika notebook yake
Wakati wote mwalimu akifundisha sikumsikia kabisa ila tu mwishowe nilisikia akisema kwamba ni kipindi chake cha mwisho kwa semester hiyo hivyo tujiandae kwa ajili ya mitihani ya mwisho
Baada ya hapo aliondoka na kutuachia makaratasi ya majaribio tuliokuaa tumefanya siku kadhaa zilizopita.
Watu waliitwa wakachukua karatasi zao lakini ya kwangu sikuweza kusikia nikitajwa, nilimfuata muwakilishi wa darasa
“We Mwantumu, Pepa langu liko wapi?” nilimuuliza lakini ghafla nikavutwa kwa nguvu nyuma
Niligeuka huku nikiwa na bonge la tusi mdomoni lakini sikufanikiwa kulitoa lote maana nilikuta ni Chris ananinyooshea karatasi langu
“Ah wewe ningekutukana” nilisema huku nikinyoosha mkono kupokea test ile lakini Chris alinitazama kwa mshangao usoni mpaka nikajishtukia na kuanza kujishika usoni “Vipi Chris” nilimuuliza
“Aah mh, samahani, njoo” alisema na kunivuta mkono tukatoka nje moja kwa moja hadi hotelini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa “Diana” aliniita huku akimega chapati kwa jino lake
“abee” nilisema na kumtazama usoni
“Samahani you aren’t okey, kweli vile haupo sawa” aliniambia sijui alijuaje lakini Nilitabasamu kwa kujilazimisha maana nilikuwa na huzuni isiyo ya kawaida
“niko sawa Chris wala usihangaike kunijali hivyo” nilimuambia
“Why jaman?” aliniuliza mi nikasikia sms imeingia kwenye simu yangu ndani ya begi
“nina matatizo makubwa ambayo nikikuambia matatizo yenyewe kamwe hautaweza kunisaidia” niliongea huku nikifungua begi nitoe simu
“Ah mh matatizo gan, au ndo shemeji anazingua” aliongea maneno ambayo yalikuwa ya kweli kabisa lakini ilibidi nimbishie
“Hapana bana” niliongea huku nikiandika PIN na kufungua SMS kwenye simu yangu nikakuta ni ya Flora “SHOGA UKO WAPI?” aliniuliza
“Cafe” nilimjibu kwa mkato na kurudisha simu kwenye begi kisha nikaendelea kuongea na Chriss
“Unajua Christian bana nina shida hadi basi naogopa, maana sitaweza kuzisolve kwa sasa”
“Nambie kuna shida gani ambayo siwezi kukusaidia kwa mfano” aliniuliza
“Mwenzako kodi imeisha na hata nyumbani hawataki kunijua kabisa nawasumbua hawajibu simu zangu” nilimuambia bila kujua machozi yanatokea wapi
“Ni sh ngapi?” aliniuliza
“Kwa mwezi 60,000/=” niliongea kwa ufasaha mno huku nikimtazama usoni mara ghafla Flora akaingia pale na kuketi
“Mambo zenu” Flora alisalimia
“Fresh, Safi” tuliitikia
Kitu kimoja ambacho Chris niligundua hapendi ni umbea umbea, kuanzia muda ule alikuwa kimya mpaka kumaliza kunywa chai halafu akainuka na kwenda kunawa huku akinitazama na kuweka mkono sikioni kwa ishara ya kupiga simu “Tutawasiliana” alisema na kwenda kulipa, kisha akaondoka
Tulibaki mimi na Flora, pale ndani ya Hoteli
“Mwenzangu vipi mbona kama unalia?” aliniuliza
“Seba mwenzako” nilisema kwa huzuni
“Mh Seba tena? Kafanya nini?” aliniuliza
“Kaniacha, halafu akachukua vitu vyake ndani”
“Mmmmh jamani”alinigunia
“Ndo hivyo ila sawa najua sitashindwa kuishi peke yangu” niliongea kwa huruma halafu ghafla nikahisi kitu fulani ambacho kilinishtua sana
“vipi D” aliniuliza
“Mi naenda nyumbani” nilisema
“Kwanini uondoke? Je vipindi?”
“Sina hamu ya kuingia darasani”
Niliinuka kama mshale na kuchukua pochi hata mikono sikunawa, huyo kigamboni
**
Nilifika baada ya nusu saa mpaka nyumba niliyopanga halafu nikakuta majirani nje wakabaki wananishangaa, niliwasalimia na kufungua mlango, ile nimeingiza uso ndani kutazama hivi!!! Nilibaki nimeduwaa hakuna kitu zaidi ya begi na nguo zangu pale ndani, vyote vimeshachukuliwa….Niliumia sana.
EP 11
Nililegea, nikashuka chini mzima mzima huku nikiwa nalia machozi yasiyo ya kifani yaani muwasho kidogo tu umenifanya nikampoteza mwanaume aliyenipa kila kitu
Nilifunga mlango huku nikiwa chini halafu nikachukua simu na kumpigia Seba, lakini hakupokea ndo nikapata shida zaidi
Nilimtumia message “SEBA JAMANI KWANINI UMEAMUA KUNIFANYIA HIVI?”
Nilipomaliza kutuma ule ujumbe nilibaki naangalia kule ndani huku machozi ya kizidi kunitoka maana sikuwa na jambo la kufanya zaidi ya kulia.
Niliinuka, niliona aibu kutoka nje majirani ntawaangalia vipi usoni, roho iliniuma zaidi.
Nikiwa nawaza mara mlango uligongwa nikatulia na kusikiliza zaidi kama patagongwa tena
“Hodiiiii” sauti ya Ba mwenye nyumba ilisikika
Nilifuta machozi haraka haraka halafu nikainuka na kusogea mlangoni huku nikijitahidi kuufanya uso kutokuwa na machozi kabisa ili nikifungua mlango asijue ninalia
“Hodii humu ndani” aliita tena halafu ikafuata minong’ono hapo nje kana kwamba alifuatana na watu.
Nilisogea mlangoni na kufungua nikatazama amekuja na watu wawili nliokuwa siwajui “Shikamoo ba Rajabu” Nilimsalimia
“Marahaba, vipi umerudi saa ngapi maana niliambiwa kwamba utakuja kuchukua nguo zako” aliniambia, japo sikuwa na taarifa hivyo nilimtazama usoni na kumjibu
“Ndio nachukua ila mpaka jioni” nilimuambia
“Ok… Sasa huyu niliyefuatana naye ni mpangaji mpya hivyo basi anaangalia chumba kikimpendeza alipie twaomba nafasi kidogo”
“Sawa” Niliongea na kusogea pembeni nikiwaachaa waingie mimi nikasimama barazani mara nikasikia sauti
“Dianaa” ilikuwa sauti ya mpangaji mmoja pale ndani alikuwa anaitwa Mama Seven nilimgeukia na kumtazama halafu akakunja mikono kwa ishara ya kuniita
“Njoo”
Nilianza kutembea huku nikiwa najiuliza anataka kuniambia nini halafu nilipofika alisogea ili wote tuketi kwenye kigoda
“Mama Seven” niliongea
“Pole sana Diana, najua amekuacha yule kijana ila usijali maisha ndivyo yalivyo lakini nikuambie kitu chunga sana marafiki wako kwani ni mashetani tu” aliniongelesha kunitia moyo na kunielimisha
“Sijakuelewa” nilisema
“Utanielewa baada ya muda mfupi, lakini pia kama hauna pa kulala utaniambia nikutafutie huku ukitafuta maisha” aliongea
“Asante ma Seven” nilimshukuru mara simu yangu ikaita kwenye mkoba, haraka haraka nikaitoa nikijua ni Seba kumbe ni Chris, kiukweli sikumpenda yule kaka kabisa lakini nilipokea
“Hallo Chriss”
“Uko wapi mbona sikuoni darasani” aliniuliza
“Niko Nyumbani si unajua nina matatizo kibao jamani?” nilimuuliza
“Sawa usijali, lakini Sir Eliudi anakuulizia sana” aliniambia
“Sawa, siwezi kuja wameiba kila kitu” niliongea kwa huruma
“Wameiba???” Aliniuliza
“Ndio yaani ni shida tupu”
“Pole sana, una mpango gani?” aliniuliza
“Sina lolote natafuta rafiki wa kunisaidia nipate pa kulala kipindi cha mitihani ili nisifeli halafu nikimaliza ntaenda kujipanga likizo”
“Ok ukiwa na tatizo usisite kuniambia”
“Sawa Chris”
Baada ya Chris kukata simu nilipata wazo kwamba labda mwalimu Eliudi ana uwezo wa kunisaidia hilo tatizo hivyo nilimuaga mama Seven na kuanza kutembea tembea mpaka sehemu fulani nikaketi na kununua maji ya uhai kisha nikatuma mesage kwa Sir Eliudi
“Samahani mwalimu sijaweza kufika kwenye kipindi chako nina matatizo mengi sana” nilituma na kutulia kimya kusubiri atasema nini lakini hakujibu
Baadaye Ikiwa ni mida ya saa 12 jioni nilikuwa sijui nielekee wapi na nilikuwa nimesimama katikati ya chumba hicho nilichokuwa nikiishi, na begi nimeshika mkononi, nilichukua simu na kumpigia Flora
“Hallo Flora shoga angu” nilimuita
“nambie Diana shoga ake” aliniambia kwa ukarimu nikajua pa kulala nimepapata
“Jamani unajua hapa nilipo sina raha?” Nilimuambia
“Pole najua jinsi gani unateseka lakini ndo hivyo wanaume walivyo”
“kweli shog, hivi unajua kaja kuchukua kila kitu akaacha begi na nguo zangu tu?” nilimuuliza lakini hata hakushtuka
“Kawaida Shogaa” alinijibu hivyo
“Sawa, sina pa kulala naomba nije kulala hapo kwako kwa siku chache” Nilimuambia
“Kwangu???” aliuliza kwa mshangao “Kwangu hapana, sitaki na haiwezekani” alisema Flora
“Jamani Flora kwanini sasa mbona sisi ni marafiki….”
“Sitaki nimesema Mfyuuuu” nilishangaa amegeuka mbogo na kukata simu mimi nikabaki nikijiuliza KWANINI AMEKATAA?
EP 12
Maswali yasiyokuwa na kifani yaliniandama, nikawa nawaza hivi Flora ndo kanijibu hivo au naota, maana alikuwa rafiki wangu wa damu.
Nilijaribu kupiga tena simu alikuwa hapatikani halafu muda huo huo kifirushi kikaniishia muda wake
“Daah jaman” niliongea peke yangu huku nikikumbuka maneno ya baba mwenye nyumba “JIONI UKISHATOA VITU VYAKO NAOMBA UNILETEE UFUNGUO WA CHUMBA” aliniambia mchana wakati alipokuwa anaondoka na yule mpangaji mpya.
Nilitoka na mabegi yangu nikaenda hadi kwa mama Seven na kumgongea mlango
“Naniii?” aliuliza
“Diana” nilisema
Mama Seven alinifungulia baada ya sekunde chache “Samahani mama Seven naomba niweke begi langu hapa ili nipeleke ufunguo wa ba mwenye nyumba
“Sawa hamna shida” alisema huku akiwa anapokea begi langu na kuweka ndani.
Nilishukuru kisha nikatoka huku nikiwa naitazama simu yangu ambayo alikuwa ananipigia mwalimu Eliudi, niliitazama kwa muda kisha nikaipokea
“Hallow” ilitoka sauti yake nzito
“Shikamoo Sir”
“Marahaba ndo nimefungua message yako hapa, nilikuwa bize sana”
“Ndio”
“Uko wapi Diana?” aliniuliza
“Niko kigamboni”
“Ok njoo haraka huku tabata tuongee” aliniambia
“Sawa nakuja”
“Ok”
Niliona moja ya matatizo yangu yanaweza yakatatuliwa siku hiyo, hivyo nilitembea haraka haraka mpaka kwa ba mwenye nyumba kisha nikampa ufunguo na kuaga kuondoka kuelekea kivukoni
Nililipa 200 tu kupanda pantoni maana nilikuwa nina kitambulisho cha kuwa mimi ni mwanafunzi wa chuo
Nilipofika posta tu nilikutana na Chris akiwa amesimama na marafiki zake wa kiume karibia na kituo cha mwendo kasi walitaka kupanda magari hayo kwa safari za haraka
“Aaah Diaaana” Chris aliongea nikafutabasamu halafu akanifuata
“Unaenda wapi?” aliniuliza
“Tabata kwa Flora” ilibidi nimdanganye kwa sababu yeye mwenyewe Flora alikuwa akiishi tabata
“Ok sawa dear” alisema huku akiweka mkono mfukoni mwake na kutoa noti kadhaa za elfu kumi kumi zikichanganyika na elfu tano tano halafu akanikabidhi “Hizi kalipie kodi miezi mitatu au ushalipa?” aliniuliza
“Hapana sijalipa, jamani nashukuru sana Chris” nilisema kwa furaha na kuziweka zile hela kwa begi halafu nikamshika mkono
“Uwahi basi huko unakoenda kesho utaniambia imekuwaje” aliniambia mimi nikatabasmu
“Sawa”
Nilitembea haraka Haraka huku nikimshukuru Mungu, Chris alikuwa kama mkombozi wangu hata hivyo alinifanya hadi nipande boda boda kwa hela yake ili nimuwahi Sir Eliudi kwani nilikuwa najua kabisa yeye nikikaa naye vizuri atanipatia pesa nyingi zaidi
Ndani ya dakika 16 nilikuwa pale tabata, nikambipu mzee huyo halafu nikasimama pembeni mwa barabara huku nikisubiri apige
Kweli dakika moja tu alipiga
“Diana”
“Abee”
“Uko wapi?”
“Nimeshafika Tabata”
“Mh kumbe haraka tu hivyo? Ok samahani niko kwenye kikao na wana sacoss wenzangu kama dakika 30 nitakuja hapo, Vivyo unaweza kula chochote nikija ntalipa” aliniambia
“Ok” nilisema
Alikata simu mimi nikasonya kwa hasira maana alikuwa kama ananicheleweshea hivi
Nilibaki nikiwaza kwa dakika chache, ndipo nikaenda kununua vocha na kutembea mpaka kwa Flora maana kulikuwa mitaa ile ile.
Nilipofika kwa Flora, nilisikia muziki mzito chumbani kwake na mlango ulikuwa wazi halafu walikuwa wakiongea kwa nguvu kama watu wawili hivi hivyo nikaamua kusogea mlangoni na kugonga
Niligonga nikagonga na kugonga lakini hawakusikia, ikabidi nijiongeze niingie ndani.
Nilipoingia ndani hivi sikuamini, niliona kituko, Flora aliduwaa maana alikuwa kitandani akikatika wimbo wa Kadogo juu ya kifua cha mwanaume lakini walikuwa na nguo, halafu mwanaume mwenyewe ni Seba, nilibaki mdomo wazi huku nikitazama kushoto kulia, vile vitu vyangu vyote alivyochukua Seba vilikuwa kule ndani kwa Flora
“Flora!!!” Niliita kwa uoga “Seba” niliita kwa kuduwaa.
INAENDELEA

