𝗠𝗔𝗟𝗜𝗣𝗢 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 16
Tulipoishia
“Mh, wanafanana sana” alisema Erick
“Sana”
Moyoni Erick alipata wasiwasi kwamba ule mfanano unaweza kupelekea mkewe kushawishika na kumsaliti kwa sababu alikuwa na mahusiano na marehemu Amidu kabla ya kifo kumfika mwaka na nusu uliopita
Siku ile Jonas alipotembea ofisini kwa Haidali alikuta namba ya Erick imeandikwa kwenye diary ya ofisi.
Akaichukua haraka huku akisema kwa sauti ndogo “Hii nina kazi nayo”
Endelea hapa…..
BAADA YA SIKU 20
(Maeneo ya Kibosho Umbwe, Moshi, Kilimanjaro)
Asubuhi saa mbili mama Aneth, alikuwa ameketi jikoni anakunywa chai ya maziwa taratibu na kiporo cha ndizi zilizochanganywa na Maharagwe.
Wakati anafanya hayo bado binti yake alikuwa amelala kitandani, binti huyu alikuwa anaitwa Janeth ila mara nyingi walimuita Manka, alikuwa ni mtoto wake wa mwisho katika watoto wanne, lakini alikuwa ni mtoto wa pili wa kike katika familia hiyo. Ambapo mtoto wa kwanza wa familia hiyo alikuwa ni Aneth, mke wa Erick au kwa jina lingine Mama Chris.
“We mankaa” mama Aneth aliita kwa hasira maana yeye kama mama wa miaka 56 alitakiwa awe amepumzika kitandani, huku mtoto wake akiwa ameshaamka akafanya usafi na kuandaa kifungua kinywa.
Manka hakuitika kabisa “we Mankaa” alisema kwa mara nyingine lakini bado binti alikuwa amelala kitandani, sio kwamba alikuwa hamsikii ila alikuwa ni mvivu na mwenye kiburi tu binti huyo.
Mama kwa hasira aliweka kikombe cha chai halafu akainuka akavuta ukuni uliokuwa kando yake na kuingia nao moja kwa moja hadi chumbani kwa binti, akamkuta kajifunika hadi kichwani, sauti ya vitufe (batani) za simu ikisikikia, kuonyesha kwamba alikuwa anaandika message kwa fujo sana
Mama alichokifanya alinyanyua juu ule ukuni aliokuwa nao akamshushia binti yake
“Auwiiiii” binti alipiga kelele huku akijifunua kwenye shuka na kutazama ni mama yake ameshatega ukuni juu anataka kuushusha tena
“We mbwa mimi ninakuita unalala mpaka saa tatu una raha gani mimi ninahangaika kupika kila kitu wewe mtoto mdogo umelala mshezi wewe” aliposema hivyo akashusha chini akamnyandua paaah
Binti alipiga kelele akashuka kitandani na kutoka speed, mama yuko hapa nyuma anamfuata kwa kasi.
Janeth kwa kuwa hakuvaa vizuri, aliingia katika chumba cha kuhifadhia nafaka na kujifungia halafu akasema “Mama nisamehe”
“Nikusamehe, mara ngapi mpumbavu wewe? Unanipa kazi mimi ya kupambana na kuku wasimwage kiporo chako halafu wewe umelala? Dada yako Aneth hakuwa hivi mshenzi”
“Nisamehe”
“Shut up….embu toka huko ukanywe chai uende kwenye majani ya ng’ombe, vyombo venyewe vichafu vinahitaji usafi pumbavu wewe”
Mama huyu alikuwa na hasira kweli kweli, alitoka pale akiwa amefura, akaingia jikoni na kukuta kuku wako juu ya kiporo na chai yake imeshamwaga saa nyingi.
Mama huyu hapa na kuku anamuulia, hapa, pale kuku haoo, maana jiko lao kidogo lilikuwa halijaziribwa vya kutosha.
Baada ya sekunde kadhaa Aneth alitoka nje, ila alikuwa amevuta mdomo kwa hasira, alikuwa ni binti mmoja mjeuri sana katika familia ya mzee Masawe.
Wakati huo baba na watoto wake wawili wa kiume walikuwa mbali sana, huko shambani wakipalilia mahindi.
*
Baadaye jijini Dar es salaam Aneth akiwa amekaa ofisini alipokea ijumbe kutoka kwa mdogo wake
“Dada shikamoo, ile ishu uliniambiaga ya kuja Dar vipi?” alimuuliza
“Marahaba mdogo wangu….nilikuwa nimeshasahau, we jiandae jioni nitaongea na shemeji yako maana sikumshirikisha ili asije akakasirika” Aijibu Aneth
“Sawa dada” alisema Manka
Haya yote alikuwa anayafanya kwa sababu alikuwa amekasirishwa na kitendo cha mama kumpiga na fimbo asubuhi yake.
Siku nzima binti alikuwa amenuna tu kwa sababu alikuwa ameambiwa vile.
Jioni ilipofika Aneth alirejea nyumbani kwake Wazo Ya Tegeta, na hata kumsubiri mume wake ambaye kipindi hicho alikuwa hachelewagi sana kufika nyumbani.
Baada ya `Erick kurejea nyumbani, mke wake alitanguliza ombili la mdogo wake kuja jijini Dar kwa ajili ya kubadilisha upepo
“Hamna shida, hamna shida kwani alitaka aje lini?” aliuliza Erick
“Nilitaka nimtumie nauli aje hata kesho”
“Haya hamna shida”
Erick hakujali kuhusu hilo, aliruhusu kirahisi tu, kwani alikuwa hanaga makuu kijana yule, aliamini kitu hicho kinaweza kumsababishia mafanikio shemeji yake
*
Hata baada ya siku tano Manka aliingia jijini Dar es Salaam. Alifurahi sana kupafahamu.
Siku hiyo Jonas alikuwa ameketi katika ofisi ya kampuni yao, muda huo Haidali hakuwepo, alikuwa ameenda kutembelea ofisi ndogo ya Bagamoyo.
Hii ilimpa nafasi Jonas kuamua kumrushia ndoano kwa mara ya pili binti Aneth
“Kwanini Aneth kila nikikuomba unanikatalia?” aliuliza Jonas
“Jonas…” binti alimuita huku akimtazama kwa jicho la onyo
“Nini Aneth lakini”
“Kama huwezi kuzungumza mambo mengine naombau kae kimya” binti alifoka
“Nakupenda na naomba tuwe wapenzi Aneth unanitesa”
“Jonas, mimi sio wa hadhi yako, mimi na Wangoni wapi na wapi? Naomba usinizoee kama unataka kuendelea kukaa hapa kwenye ofisi hii, naomba usiendelee kunisumbua, mimi ni kama boss wako” alisema kwa matambo
“Tokaa boss gani, unaliwa tu unaachwa” alisema kwa hasira jonas
“Acha niliwe, au unataka na wewe uliwe?’ alimjibu kwa kashfa
Ili neno lilimuuma Jonas, moyoni akasema ‘ngoja nitakuonyesha dawa yako’
EP 17
Siku moja baadaye Erick akiwa ameketi kazini kwake alikuwa anatafakari masuala ya muhimu sana ya biashara yake, ndipo alipopokea simu kutoka kwa Jonas
“Hallo” Erick alisema baada ya kupokea simu
“Hallo braza kwema?” alisema Jonas
“Kwema kabisa, nani?”
“mimi kijana ambaye nafanya kazi katika ofisi yako na mke wako”
“Yupi?”
“Tuliyekula matunda hapa siku ulipofika mara ya kwanza” alisema Jonas
“Anhaa, nimekukumbuka, vipi kuna tatizo?” aliuliza
“Hakuna tatizo ila kuna ishu nilitaka kuongea na wewe bro” alisema binti
“Ishu gani tena?” aliuliza Erick
“Ninaomba ukirudi mapema unitafute ni ishu ya kibiashara” alimdanganya lakini kiukweli ni kwamba Jonas alikuwa anataka ampe siri ya kile ambacho kimekuwa kikifanyika muda mrefu pamoja na Aneth pamoja na Haidali
“Daah…sawa kwa hiyo haiwezekani kuongea kwenye simu?”
“Haitawezekana kaka…ni jambo la muhimu sana, ni jambo ambalo litakomboa maisha yako na pesa zako nyingi sana” alisema
“Sawa hamna tatizo”
Erick aliwaza sana, na kwa kuwa alikuwa na wasiwasi kuhusiana na mkewe, hakuweza kuvumilia alijikuta alihisi ndilo jambo ambalo anaenda kuambiwa na kijana huyo aitwaye Jonas
Hata hivyo akiwa ofisini kwake, kuna kijana mmoja alikuwa akifanya kazi na Dullah, ambaye kijana huyo alikuwa ni muuzaji tu pale dukani, ndipo akamfuata Erick na kumuambia anataka kuuza simu yake
“Simu ipi?” Erick aliuliza
Yule kijana aliitoa mfukoni na kumuonyesha, ilikuwa ni infinix s5 ndipo Erick akasema “Hii rimoti unauza shilingi ngapi?”
Yule kijana akacheka “Usiite rimoti, hilo ni tambo broo….nipe laki mbili?”
“Laki mbili???” Erick aliongea kwa mshtuko na kumrudishia simu yake “Embu shiak gobole lako wewe”
“Haaa, bro kwani wewe una shilingi ngapi?” aliuliza yule kijana
“Sina kazi nayo, nilikuwa naulizia tu bei, ungekubali laki na ishirini ningekupa akaitumie hata housegirl wangu” alisema Erick
“Mh, fanya mia na hamsini nikupe (laki na hamsini)”
“Kwanza ina ukubwa gani wa storage?”
“GB 32” alisema yule kijana
“Anhaa, nakupa na arobaini sa hivi, toa kila kilicho chako” alisema huku akitoa wallet mfukoni”
“Daaah” yule kijana aliishiwa pozi lakini hakuwa na namna, alikuwa na shida yake ya kwenda kulipa kodi, maana mshahara mwenyewe ulikuwa haumtoshi vizuri.
Ni kweli yule kijana alitoa vitu vyake, na kuhamisha vya muhimu kwenda kwenye kikadi cha kumbukumbu kisha akampatia Erick naye akamkabidhi shilingi laki moja na arobaini.
*
Usiku saa 4 Erick alienda mpaka nyumbani ambapo alimkuta housegirl akipanga panga vyakula ukumbini, alitaka kumpa ile simu, lakini moyoni alisita na kukumbuka kwamba shemeji yake ndiye mwenye thamani kuliko dada wa kazi.
Alimpa salamu kisha akapita zake kuelekea chumbani, alipofika alimkuta mkewe amekaa anaongea na Manka wote kwa pamoja, chumbani.
“Shemeji shikamoo” alisema Manka huku akiinuka na kutaka kutoka maana kile ni chumba cha wanandoa
“Marahaba umeshindaje?”
“Salama tu”
Erick alimshika mkewe kichwani na kusema “Mama Chris, vipi?” halafu akaketi kando yake, huku Manka naye akiondoka
“Safi pole na majukumu”
“Asante…oh shit” alisema Erick kisha akaita “We shem…. Manka ee”
Manka akageuka na kuitika “abee”
“Embu njoo” aliongea Erick huku akitoa simu mfukoni na kumuonyeshea mke wake “Kuna mtu nimemkuta anauza simu yake bei rahisi nikasema nimchukulie shemeji au wewe unaonaje?” aliuliza
“Hamna shida” Aneth alijibu huku akiipokea na kuikagua kagua ni kweli ilionekana imetumika.
Manka alipofika pale ndani akasema “Shem nimekuja”
“Anhaa….nimekuletea simu hapo utumie tumie, kipindi uko free” alisema
Moyo wa Manka ulimuenda mbio, alishtuka sana, alijisikia furaha ya ajabu, hakuwahi kumiliki simu janja kabisa ndiyo yake ya kwanza, Aneth alimkabidhi, hawakuwa na roho mbaya wanandoa hawa wala hawakuwaza kumfurahisha ndugu yao, au shemeji mtu.
“Asante shemeji asante sana” alisema kwa furaha, haamini mtoto wa kike
“Usijali” aliongea Erick kisha akamtazama mkewe “Vipi kazi inaendeleaje?” aliuliza Erick
“Salama tu…upande wako wewe vipi?”
“Biashara ngumu, ila Alhamdulillah sio mbaya tunaendelea kuishi, vipi bado unatamani kuendelea na kazi au tufungue tu biashara ambayo utakuwa free zaidi kufanya mambo yako?” aliuliza Erick
“Mh, hapana bora nifanye hivi, halafu tufungue biashara tumuweke Manka aifanye” alitoa wazo Aneth
“Umeongea point”
*
Upande wa Manka, yeye alienda sebuleni akaanza kumtambia Katarina ambaye alikuwa ni binti wa kazi
“Shemeji kaniletea simu” alisema huku akimuonyesha na kumringishia
“Amekununulia simu?” aliuliza Katarina huku akiangalia
“Ndio” alisema Manka kisha akaketi kwenye sofa kisha akaanza kutoa laini zake kwenye kiswaswadu atie kwenye simu yake kubwa aliyoletewa
Sio siri, wivu ulimjaa sana Katarina, aliumia kwa sababu ameishi muda mrefu sana na watu hao lakini hakuwahi kununuliwa hata kiswaswadu, alikuwa anatumia cha kwake ambacho kilikuwa hakina hata mfuniko lakini hawakumjali. Alijisikia vibaya japo hakutaka kulionyesha hili
************
Erick alitafuta muda kesho yake akaenda maeneo ya mbezi beach muda wa jioni saa kumi na mbili, ndipo akakutana na Jonas kama walivyokuwa wameahidiana jana yake
Siku hiyo kwa bahati mbaya sana, Haidali alikuwa katika hoteli moja na Aneth wakila maisha juu ghorofani, na kwa kuwa Jonas alikuwa anajua kabisa watu wale wapo pale, yeye alifanya makusudi akakaa kwenye ground floor ya hoteli hiyo ili wakishuka tu wamkute pale Erick awafumanie maana alikuwa anataka kulipa kwa kitendo cha Aneth kumkatalia penzi.
Erick aliagiza pombe na nyama, akala kidogo sana ndipo kapokea simu ya uongo na kweli akatoka akiongea ongea kuelekea maeneo ya nje.
Alipofika nje alikaa kwa muda mrefu bila kurudi, lakini Erick alimsubiri pale pale.
Kwa bahati mbaya kama ilivyoelezwa hapo awali, Haidali na Aneth walishuka taratibu wakiwa wameshikana kiuno.
Wote walikuwa wamelewa tayari na walikuwa wakijiamini sana maana ni muda mrefu wamekuwa wakifanya hivyo bila hata kufumaniwa.
Erick alishangaa kuona mtu kama mke wake akipita huku ameshikwa kiuno, japo kulikuwa na giza fulani hivi, na walikuwa wanapita mbali kidogo, Erick alijua mwendo ni wa mke wake. Walipita watu wale bila kugundua yeye yuko pale, wakatoka nje
Roho ilianza kumuuma mtaalam akaamua kuacha kunywa pombe na kufuatilia nyuma taratibu. Alipofika nje alishuhudia mke wake akiwa amesimama kando ya gari la Haidali mara wakapigana mabusu mdomoni. Alishtuka nusu adongoke
Alishangaa wawili hao wameingia ndani ya gari bila kuliona la kwake limepaki maeneo yale wakaondoka moja kwa moja.
Erick alipaniki, aliingia kwenye gari yake na kuanza kuwafuata nyuma tararibu, kumbe Jonas alikuwa maeneo fulani nje ya hoteli anaangalia tukio linavyoenda, moyoni anafurahi misheni yake kukubali.
Erick aliifuata gari ya Haidali taratibu nyuma, licha ya kuwepo kwenye foleni kubwa, lakini hakuweza kuwapoteza alizidi kuwafuatilia taratiibu
Walipofika mbele kidogo walikuta kuna njia moja ya mkato ambayo wangeipita wangetokea ofisini kwao ili Aneth akachukue gari yake aende nyumbani, walikatiza hapo naye akawafuata
Kwa kuwa walikuwa wamelewa hawakutilia shaka gari iliyokuwa nyuma yao, alisonga taratibu na kufika mahali wakasimamisha gari kando ya barabara naye akazima taa na kupaki, alipoitazama ile gari kwa mbaali aliona kimya kikiwa kimetawala, na mara baada ya dakika moja tu gari ilianza kunesa nesa maana kuna tukio lilikuwa likiendelea.
EP 18
Ilikuwa ni dakika kama kumi zimepita, Erick alikuwa anatokwa na machozi kila alipokuwa akitazama ile gari, kilichomuuma zaidi alijaribu kumpigia simu mke wake lakini mke hakupokea simu aliikaushia tu maana alikuwa amenogewa na penzi la unyang’anyi alilokuwa akilipata kwa kijana huyo wa kiluguru na kikurya.
Erick alitoa bastola yake akataka kutoka nayo akawaangamize wawili hao, lakini roho ikamuambia aachane nao kwanza, labda anaweza kupata suluhisho baadaye.
Erick aliondoa taratibu gari yake akarudi nyuma na kuligeuza akaondoka huku roho ikimuuma sana, njiani alilia machozi, hakuwahi kumsaliti mke wake hata mara moja, hakuwahi hata kumuonea, moyo wake ulimuuma hasa pale alipokuwa anampenda mno.
Erick alikuwa ni mtu mwenye pesa, angeweza kuchukua mwanamke wa aina yoyote lakini kwa sababu alikuwa anampenda mke wake hakuwahi kufanya hivyo, mara nyingi alimuamini kwa sababu alikuwa ni mwanamke mwenye akili za maisha lakini kumbe ni msaliti mkubwa sana moyoni mwake.
Siku hiyo, Erick alifika nyumbani, akawasalimia Manka na Katarina ambao walikuwa sebuleni wakiangalia runinga.
Alipoingia chumbani kwake aliendelea kulia kwa uchungu wa hali ya juu, macho yalikuwa ni magumu upande wake
‘Kwanini unanifanyia hivi…..kwanini lakini mke wangu??? Aaaah daaah umeniumiza sana” alisema mtaalam hali iliyopelekea mtoto kushtuka usingizini maana alikuwa amelazwa kitandani na Manka.
Erick aliendelea kutoa machozi, macho yalikuwa ni mekundu lakini hakujali kelele za mtoto aliyekuwa analia kitandani pale.
Baada ya Manka kusikia kelele za mtoto zimezidi, alijikuta anaenda moja kwa moja mpaka mlangoni kwa shemeji yake, na kumgongea
“Shemeji….shem” alisema
“Naomba nimchukue mtoto” alisema binti akiwa mlangoni
Erick hakujibu chochote bado alikuwa anasikia maumivu ya hali ya juu, ikabidi Manka afungue tu mlango na kuchungulia, alimkuta shemeji akiwa amekaa tu kashika tama, hajali mtoto ambaye anapiga kelele nyuma yake
“Shemeji” alisema Manka na kuingia chumbani kwa shemeji yake “Mbona nakuita hauitiki?” aliuliza na kumfuata mtoto akambeba, alipomtazama shemeji machoni hivi alikuwa anasikitisha ikabidi binti amuite kwa mshangao huku akimbembeleza mtoto “Shemeji unalia??”
“Daaah” alisema na kufuta machozi bwana Erick halafu akainamisha kichwa chini na kukisikitisha
“Tatizo nini?” aliuliza
Erick alinyanyua uso na kumtazama shemeji yake akamuuliza “Kwanini dada yako ananifanyia hivi lakini?” alimuuliza na kuzidi kuumia
“Kafanyeje dada?” aliuliza shemeji
“Hivi kweli Aneth ni wa kwenda kutembea na mwanaume mwingine nje ya ndoa? Nimemkosea nini mimi? Kwani ni kitu gani nimeshindwa kumfanyia huyu mwanamke?” alisema kwa hasira sana huku akijutia nafsi “Hakika mapenzi yanauma shemeji, mapenzi yanauma eti daa” alisema na kunyanyua T-Shirt akafuta machozi yaliyoririkika mashavuni kutoka machoni.
“Dada amekusaliti?” aliuliza Manka
“Daaah…..basi tu shem…embu nenda nje niache nilie mpaka niridhike ndio nitakaa sawa” alisema Erick, hakuamini kama atakuja kupitia maumivu makubwa ya mapenzi kiasi kile.
Manka alitoka nje na kumuacha Erick akiwa anazidi kulia, hata hivyo honi zilianza kusikika getini kwani ndiyo Aneth alikuwa anarudi nyumbani saa hiyo akitoka kupata raha, na hakujua kama mumewe analijua hilo.
Katarina alienda kufungua geti na binti aliingia, alishtuliwa kidogo na kukuta gari ya mume wake pale ndani, akajua mume alisharudi mapema wakati mara nyingi alikuwa akichelewa, alijiuliza atamjibu amechelewa wapi.
Hata hivyo binti alipaki gari yake kisha akaingia ndani lakini alipofika chumbani hakumkuta Erick chumbani, Erick alikuwa ameshatoka muda mrefu kupitia mlango wa nyuma, hakutaka amuone mkewe machoni maana aliamini anaweza kufanya jambo baya kabisa kwa mke wake huyo.
Alifika njiani akachukua pikipiki na kusema kwamba apelekwe mpaka Mwenge, nia yake ilikuwa ni kwenda mahali akanywe pombe kali alewe sana.
Hata hivyo Aneth alipomkosa chumbani alirudi sebuleni na kumuuliza Manka “Kwani baba Chris yuko wapi?”
Manka akajibu “Ba Chris ameingia chumbani mbona”
“Mh hayupo mbona”
“Je bafuni?”
“Hayupo pia”
“Labda katokea mlango wa nyuma”
“Atarudi” alisema Aneth akijua shemeji hajaenda mbali sana. Lakini pia alifahamu shemeji yuko katika hali gani na hakutaka kumuambia dada yake.
*
Kule mwenge Erick aliingia katika night club na kuagiza pombe kali za gharama, akanya mpaka akahakikisha amelewa kisawasawa, ndipo akachukua mwanamke mmoja na kwenda kulala naye.
Ilipofika saa saba Aneth alijaribu kumpigia mumewe lakini hakupatikana, alijifanya amekasirika na kumtumia message nyingi za lawama kwamba abaki huko huko aliko kwani alikuwa anahisi mumewe anamsaliti, huku yeye akijiona hafanyi kosa kutembea na Haidali.
Ilipofika asubuhi saa kumi na mbili yule mwanamke aliyelala na Erick aliondoka akamuacha Erick peke yake, Erick aliwasha simu yake, na kusoma jumbe za mkewe akazipuuzia, lakini kuna message mbili zilitoka kwa namba mpya zikisema hivi
1. Samahani sana kaka kwa lile uliloliona, nia yangu kukuleta pale ni ili uje ujionee mwenyewe uchafu wa mke wako
2. Kila mara amekuwa akikusaliti na huyu mwamba, sio kwamba namuonea wivu ila niliamua kukuambia hivi ili ujitoe mapema kwa sababu huyo kijana pia ni muathirika wa virusi vya UKIMWI hivyo epusha afya yak
Hizi message zilizidi kuurarua moyo wa Erick akajikuta anatetemeka mwili “ANA UKIMWI??!!!!” aliongea kwa sauti kubwa na kwa uoga “AMEAMUA KUNIUA???” Alijiuliza mtaalam kwa uchungu maana alikuwa akilala na mwanamke huyo bila kujua ana mwanaume mwingine.
Kwa haraka haraka alijua kwamba yule aliyetuma zile jumbe alikuwa ni Jonas licha ya kutumia namba nyingine tofauti ambayo labda alifanya hivyo ili message zisitumike kama ushahidi
HIVI, JE NI KWELI HAIDALI ANA VIRUSI VYA UKIMWI?
NA JE ERICK ATACHUKUA MAAMUZI GANI BAADA YA KUGUNDUA MCHEPUKO WA MKE WAKE ANA UKIMWI?
INAENDELEA

