Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

MTOTO WA AJABU

PART: 15

ILIPOISHIA,

” Sisi ni askari polisi, tunakuhitaji kwa mahojiano” walichomoa vitambulisho na kumuonesha Bonge ndipo aliponaki kinywa wazi huku akiwa anatetemeka mwili mzima…

SONGA NAYO…

” Mahojiano nimefanya  kosa gani” Bonge aliwauliza askari

” Mama tunakuheshimu sana na polisi ni sehemu salama ebu twendeni kistaarabu kabisa bila kuwekwa pingu..” walimwambia kwa sauti ya chini.

” Mi sikatai kwenda lakini nina haki ya kuambiwa kosa langu…”

” Huna kosa lolote bali tunakuhitaji kwa mahojiano mafupi..”

” Sawa  nisubiri  niende nyumabani kwanza…”

 ” Wewe mama!, muachie dereva wako vitu vyako vyote!, acha kutuchelewa bwana!” Walimfokea.

Bonge alinyamaza kisha wakamshika mkono na kuondoka naye.

Kwa mwili wake mkubwa, hawakuona haja ya kumfunga pingu ndipo waliendelea na safari ya kuelekea kituoni.

Walipokaribia kituoni, Bonge alianza kuhisi hali ya hatari kwake ndipo aliposimama kisha akawambia,

” Samahani naomba niwambie kitu…”

” We mama vipi!?, kitu gani hicho..”

” Najua huko kituoni sio sehemu ya kupokea wageni hivyo naomba tuongee mniachie..”

” Hee!, kwani unajua kosa lako?”

” Sijui kivile lakini nahisi ndo hicho mmenipelekea..”

“Kwahiyo unasemaje?”

” Nipo tayari kutoa chochote ili mniachie nami nitajua sehemu salama ya kujihifadhi..”

Askari walimuangalia mara mbili hivi kisha wakamuuliza,

” Unataka kutoa nini?”

” Nina kiasi cha milioni 30 ili mniachie..”

” Hee! Unazo hapo!” Askari walipagawa.

” Ndio zipo kwenye gari langu..”

” Ebu mpigie dereva wako alete gari..”

Bonge alimpigia mlinzi na kulete gari sehemu waliyokuwepo.

Askari hao pamoja na Bonge walipanda kwenyr gari kisha wakasogea sehemu ambayo haikuwa na makazi ya watu.

Mlinzi aliamrishwa kushuka ndipo alipofanya hivyo.

Bila kuchelewa, Bonge alinyanyua Seat ya gari kisha kisha akafungua sanduku la chuma lililokuwa limejaa noti nyekundu

Askari walijifanya wameangalia pembeni huku wakizichungulia kwa jicho la chongo.

Baada ya kumaliza kuzitoa, aliwakabidhi kwenye mfuko mweusi ambao uliwekwa nguo chini na juu.

Huko kituoni, mkuu wa kituo aliendelea kusubiri bonge aletwe kituoni ili taratibu za kisheria zifuatwe.

Baada ya mda mrefu kupita aliamua kuwapigia askari wake aliowatuma ndipo walipomwambia kuwa bado wanamsubiri na hajafika.

Alikata simu na kuendelea kuwahoji akina Asia na Mariatabu waliokuwa wamechafuka na kupoteza mwonekano wa sura zao.

Zoezi zima lilikamilika ndipo askari walipotaka kufungua mlango wa gari ili waondoke zao.

Walivuta lakini milango haikufunguka. Walijaribu kushusha vioo vya gari lakini haikuwezekana ndipo Bonge naye alipofanya hivo lakini wapi.

” Hee hili gari lako vipi!” Askari waliongea kwa mshangao.

” Na mimi nashangaa maana halijawahi kuwa hivi..”  Bonge aliongea.

Walijaribu kuwasha gari lakini halikuwaka pia ndipo taharuki ilipotanda miongoni mwao

” Ee bwana ebu tuvunje vioo tuondoke hapa maana ….” Askari alimwambia mwenzie kisha wakajaribu kuvunja vioo lakini hawakuweza

Walibaki wametazama huku wakiwa hawajui  nini wakifanye.

Walikaa ndani humo mpaka wakaanza kutokwa na kijasho kwa mbali.

Wakati wakiwa humo, Mkuu wa kituo aliamua kuwatumia ujumbe mfupi ( meseji).

” Kama bado hamjampata  ebu rudini kituoni tuone njia ipi tufanye”

Askari hao wakiwa kwenye gari, waliisoma ndipo waliposhindwa nini wajibu kwa mkuu wa kituo.

Ni askari wawili na Bonge wakiwa hawaelewi chanzo ni  nini .

Huko upande wa nyumbani kwa Braison , watu walizidi kumiminika huku huku jitihada za kila namna zikioneka kushindwa.

Kamati ya wazee iliyoongozwa na Kipara, waliendelea kufanya  kila namna mara baada ya maombi ya kummaliza Sarah kushindwa.

Walipanga mipango  mingine ikiwa ni kwa njia ya kumnywesha juice ya sumu.

Walinunua Juice kisha wakatoboa kizibo kwa juu na kumimina sumu kwa kutumia sindano.

Baada ya kumaliza, waliitikisa kwa nguvu mpaka ikachanganyika vizuri kabisa ndipo walipofanya mchakato wa nani na nani waende hospitali.

Mzee kipara kama kawaida yake, alijitolea akiongozana na mwanamke mmoja .

Mnamo mida ya saa 7 za mchana, Kipara na mama Zawadi walifika hospitalini hapo wakiwa na chakula kwenye hotpot pamoja na  juice.

Waliomba ruhusa ndipo walipokubaliwa kuingia ndani.

Akiwa kitandani amelala huku akiwa ameshika  tamu, Sarah alishangaa kumuona mama Zawadi akiwa na mzee kipara.

” Unaendeleaje?” Mama zawadi alimuuliza.

” Naendelea vizuri…” Sarah alijibu.

” Ohh pole sana …”

” Asante sana..”

Baada ya mazungumzo hayo, Mama Zawadi ambaye hakuwa anajua kama juice ina sumu, aliitoa kwenye kwenye mfuko wake kisha akampatia Sarah.

Sarah ambaye alikuwa na kiu kwelikweli, aliifungua ….

PART: 16

ILIPOISHIA,

Kwenye gari maaskari walibaki na hali ya sintofahamu mara baada ya milango kushindwa kufunguka huko nako hospitalini, Sarah bila kujua alipokea juice yenye sumu kisha akaifungua kuinywa…

SONGA NAYO…

Mda ulizidi kutaradadi kwelikweli huku hali ikizidi kuwa tete kwa askari hao waliokuwa na Bonge ndani.

Hasira kili ziliwapanda na kuanza kuwaza kumua Bonge ndani  ya gari hilo kwa kumshuku kuwafanyia tukio hilo.

Walikoki bunduki zao kwa umakini kabisa bila Bonge kujua kisha wakataka kumfyatuliar sisasi lakini kabla hawajafanya hivo, waliwaza maswali haya,

” Je tukimuua na kushindwa kutoka ndani ya gari si watatukamata kwa kosa la mauaji. Na je huyo mlinzi wake hatojua?”

Ugumu wa maswali hayo uliwafanya washushe siraha zao chini.

” Kwanini hivi lakini?!, tutakosa kazi kwa ajili yako!, mpaka sasa meseji kutoka mkuu wa kituo zinamiminika nasi tunashindwa tumwambie nini!, acha kutuchezea bwana..”

” Mimi sijui chochote na sipendi kuwa hapa” Bonge aliongea huku macho yakiwa yameanza kuwa mekundu.

Kwa hasira kali, askari mmoja alirusha bunda lote la pesa kisha akataka kujiua ndipo mwenzake alipomshika na kumnyang’anya bunduki.

” Usifanye hivo!..mke anakutegemea!, watoto wanakutegemea!, wazazi na ndugu zako wanakutegemea!,…hee!” Alimwambia mwenzake aliyebaki ameinamisha kichwa chini.

Askari huyo akiwa mikono mitupu, alijaribu kufungua mlango wa gari ndipo aliposhangaa kufunguka.

Wote walitoa macho ndipo askari alipobeba furushi hilo la pesa na kutoka nalo.

Kabla hajatoka, mlango ulijifunga ndipo mwezie alipomwambie atupe pesa hizo.

Alifanya hivo na mlango ukafunguka. Asee  walimchomoa Bonge kwa hasira zote kisha wakaanza kukimbia naye kwa speed mpaka akaishiwa pumzi.

Bila kumpumzisha walimbeba mzimamzima mpaka jasho likawachuruzia mpaka kituoni.

Walimkuta mkuu wa kituo akiwa kwa nje huku anafoka kwa simu.

” Huyu ndo mmechukua mda wote kumleta hapa!” Alitamka kwa sauti.

” Alianza kutusumbua ndo maan tumeamua kumbeba..”

” Ebu mlete hapa..” Bonge akiwa anatokwa na kijasho chembamba kwenye pua, walimfikisha kwenye sehemu ya mahojiano .

” Tunaomba usitusumbue wala nawe usisumbuke!. Tunachotaka ni maelezo ya kweli na sio longolongo…” alimwambia.

” Kwani kuna nini?” Bonge alihoji.

” Wewe ndo unaitwa  Bonge…!”

” Ndiyo…”

” Unatuhumiwa kwa kununua mtoto wa mwenzio na kumchukua nyumbani kwako ukishirikiana na wahudumu wa hospitali kwa kuwalipa kiasi cha shilingi milioni  20 huku ukijua ni kinyume na sheria. Tuhuma hizi zina ukweli wowote?”

” Hapana wala sijui chochote. Kwani nani kawambia?”

” Ohh sawa mdogomdogo tutaelewana tu. Vua viatu vyako na kabidhi simu yako. Kama una pesa nazo kusanya.”

 Bonge akiwa anatetemeka alifanya hivo kisha wakamuweka kwenye chumba walichokuwa wamewekwa akina Mariatabu.

Akiwa miguu peku , aliogopa kukanyaga ndani kwa harufu kali iliyokuwa inatokana na maji machafu.

Walimlazimisha kulala chini na kujiviringisha kwenye maji hayo ndipo alipofanya hivo kwa dakika kama 1 kisha akasema huku akiwa analia,

” Nitoeni niwambie ukweli…hoohhohhh..”

Walimuamuru anyanyuke kisha wakamwagia maji.

Akiwa hata hajielewi alirudishwa kutoa maelezo,

” Enhee!..ebu twende..mtoto ulimnunua au hapana.?”

“Ndiyo ila waliniuzia wao wala sikuwa na lengo hilo..” alijibu kwa kutetemeka.

” Huyo mtoto yuko wapi?”

” Nimemuacha nyumbani “

” Tunaweza kumpata mda huu!”

” Ndiyo..lakini..”

” Lakini nini?”

” Nisamehe..”

” Ulitaka kumfanyia nini huyo mtoto..”

” Nilitaka awe wangu wala sio lengo baya..”

” We huna mtoto..!”

” Sijabahatika kupaa mtoto na umri wangu unaniacha..”

” Unajisikiaje kama wewe mtoto wako ndo angechukuliwa mtoto wako!”

” Vibaya lakini nisamehe sitorudia”

” Mama mwenye mtoto unamfahamu”

” Ndiyo namfahamu yupo hospitali”

” Anaumwa?”

” Ndiyo alijifungua kwa operation”

Baada ya mahojiano hayo, bonge alitiwa pingu ndipo kisha Mariatabu pamoja na Asia wakatolewa ndani.

Waliwapanga na kuwapiga picha kisha wakawapandisha kwenye defenda kuelekea kwa Bonge kumchukua mtoto.

Baada ya kufika nyumbani kwake , waliingia ndani kisha wakamwambia awaoneshe alipo mtoto lakini hakuweza kumuona.

” Mtoto yuko wapi?!, usituchezee akili! tuoneshe mtoto yuko wapi!”

” Nilimuacha hapa sijui kaenda wapi!”

” Unajua we mama unataka ufie mikonoi mwetu!, mtoto mchanga unasema  kaenda wapi !, hatutoki hapa mpaka wote mtuoneshe alipo mtoto!”…

Wakati mambo yanakuwa hivo,  huko hospitalini bila kujua kama juice ina sumu, Sarah aliifungua kisha akataka kunywa lakini kabla ya kunywa, alimwambia mama zawadi,

” Naomba na wewe unywe kidogo afu unibakishie maana sijapata nguvu vizuri”

Mama Zawadi ambaye alikuwa mroho wa juice , aliipokea kisha akainua kinywa chake kunywa.

Kabla hajafanya hivo, mzee Kipara aliona moja kwa moja mama Zawadi anaenda kufa kwa sumu kali ndipo alipowaza kwa sekunde kumwambia au akae kimya ….

JE ILIKUWAJE?..

PART: 17

ILIPOISHIA..

Askari wapo nyumbani kwa Bonge huku wakizidi kumtafuta mtoto na hawampati. Huko hospitalini, Mama Zawadi alishika juice yenye sumu  na kutaka kunywa bila kujua kama ndo utakuwa mwisho wake….

SONGA NAYO….

Mzee kipara baada ya kuona mama Zawadi ameweka chupa mdomoni!, mapigo ya moyo yaliongezeka gafla huku macho yakimtoka.

Bila kupoteza mda, Mzee kipara alitamka kwa gafla!,

” Usinywe juice hiyo!, usinywe!” Alimwambia.

Mama zawadi pamoja na Sarah walibali wameshangaa huku wakiwa hawajui sababu.

Mama Zawadi akiwa halewi chanzo, alishusha chupa ya juice na kubaki nayo mkononi.

” Kwanini unasema nisinywe?” Alimuuliza kwa mshangao.

“Nimeota itakuwa sio salama nenda kaimwage” Mzee kipara akiwa anatetemeka, aliongea.

Sarah alibaki anaangalia huku akiwaza na kuwazua.

Haraka mzee Kipara alichukua juice hiyo kisha akaenda kuimwaga kwa nje ili kupoteza ushahidi.

Baada ya tukio hilo, Mzee kipara hakurudi ndipo aliposhika tama huku akiwaza njia ipi waitumie ili kummaliza Sarah.

Kitendo hicho, kiliongeza hofu kwa Sarah ndipo alipokataa kula chakula alicholetewa na Mama Zawadi.

” Kula chakula!” Mama Zawadi alimwambia

” Asante sijisikii kula kwa sasa…” Sarah alijibu huku njaa ikiwa inamsokota tumboni.

Mama Zawadi alibeba chakula chake kwenye hotpot kisha akatoka nacho nje ndipo alipomkuta Kipara akiwa anaota jua.

Walisogea pembeni kidogo kisha wakaanza kukipiga chakula hicho na badaye wakaanza utaratibu wa kurudi nyumbani.

Huko nyumbani, hali ilizidi kuwa tete mara baada ya maiti ya kuanza kutema cheche yenye kuashiria kuanza kuharibika.

Walifanya mpango wakanunua dawa kisha wakaipulizia lakini cha maajabu kila waliposogea maiti hiyo iliongea,

” Nipelekeni mkanipumzishe nyumbani”

Hakika kila mtu alizidi kustaajabu huku wakichachamaa Sarah aletwe kwa nguvu au alazimishwe ili ataje aliyempa huo ujauzito.

Minong’ono ilirindima kila sehemu huku watu wenye kichefuchefu wakisogea mbali kabisa kwa harufu ambayo ilianza kutoka.

Mambo yakiwa magumu kwelikweli, huko nyumbani kwa Bonge askari walizidi kumbana ili awaoneshe alipo mtoto.

” Mama tunakuheshimu sana!, kama umemua utasema kama umemuuza utasema na kundi lako hili” Askari waliwafunga miguu wote watatu kisha wakawambia walale chali ndio walipoingia ndani na kuanza upekuzi.

Waliingia chumba kwa chumba wakapangua vitu vyote vitanda makabati na kila aina ya vitu ambavyo walihisi kuna mtoto lakini hawakumuona.

Waliumiza kichwa mpaka wakaingia chooni na bafuni kisha wakachungulia lakini hawakuona hata dalili yoyote.

” Hawa watu wanatuchezea akili! Mtoto watakuwa wamemtoa kafara au wamemnyonga !” Waliongea wakiwa ndani kwa sauti ya chini.

Baada ya kumkosa mtoto, waliwafata tena kwa nje kisha wakawambia,

” Sasa liwe jua iwe mvua mtataja tu kwa lazima!”

” Jamani mtoto nilimuacha hapahapa nyumbani sijui kaenda wapi!” Bonge aliongea.

” Nyamaza hatutaki upuuzi wako huo!, toeni maamuzi ya mwisho kabla ya kupelekwa kwa kesi ya mauaji “

” Jamani mtoto wangu ndo alifariki lakini huyu sijamuua”

” Hee! Mtoto wako umemzika wapi na lini!”

” Sijamzika yaani nilibadilisha kwa Sarah na nasikia watakuwa wamemzika…”

” Hivi wewe mama ni kichaa eeh!, unaruhusuje mtoto wako kuzikwa na mwingine!, panda gari mpaka hapo unapopataja ila lazima mtoto apatikane”..

Waliwaingiza kwenye defenda kisha wakaelekea kwa Braison huku wakiwa wamefungwa miguu na mikono.

Wakiwa  nyumbani wanaendelea kuumiza kichwa juua ya maiti iliyoshindikana, gafla waliona Defenda ya polisi ikiingia ikiwa kasi kweli.

Walipaki pembeni kisha wakawashusha akina Bonge.

Waliwafungua miguu na kubaki na pingu na kusogea nao.

Baada ya kukaribia kwenye tukio, askari walishangaa kuona umati wa watu wengi huku harufu ikiwa imesambaa kila sehemu.

Waliangaza huku na kule ndipo mwenyekiti wa mtaa alipowaona kisha akaongea nao na kuwaeleza  mwanzo mwisho.

Bonge baada ya kuona mwili huo, alilia sana ndipo walipomwambia,

” Nenda ukaangalie kama ni mwanao..”

Bonge aliogea akiwa anahisi harufu kali ndipo maiti hiyo ilipomrukia mpaka mgongoni mwake.

Alipiga kelele na kurukaruka lakini maiti ilimgang’ania mgongoni huku ikisema,

” Mama nipumzishe..mama nipumzishe!..mama kwanini unanitesa hivi..! Mama kwanini unanidharirisha hivi!..mama kwanini unanitelekeza!..mama nipumzishe..”

” Nisaidieni…Nisaidieni!..yooh!…yooo!..nisaidieni…” Bonge alizidi kutapatapa huku watu wakimkimbia ….

PART: 18

ILIPOISHIA,

Akiwa nyumbani kwa Braison, Bonge maiti ilimg’ang’ania mgongoni mwake huku nzi wakiruka na kusherehekea kwa furaha..

SONGA NAYO..

Baada ya tukio hilo, wazee waliokuwa hapo walibaki midomo wazi huku wakiwa hawaelewi .

Polosi walimshika Bonge kisha wakampandisha kwenye gari na kuwambia aongee mbele ya umati.

Bonge kwa uchungu aliokuwa nao, alianza kuongea,

” Jamani huyu ni mwanangu! ” aliongea.

” Hee!.kulikoni tena!” Watu waliunguruma kwa sauti.

Askari aliwatuliza na kuwahakikishia kuwapa mrejesho mara baada ya kuhifadhi mwili hùo.

Ni moyo wa kijasiri waliokuwa nao askari hao mpaka walipofika nyumbani kwa Bonge.

Walimshusha kisha wakawambia Asia na Mariatabu watoe maiti hiyo.

Waliogopa sana lakini walilazimika kufanya hivo kisha wakachimba kaburi kwa harakaharaka na kuzika mwili huo.

Huko kwa Braison bado hawakuamini kama wataweza kuzika mwili huo lakini badaye walipata taarifa kuwa wamefanikiwa kuzika.

Bonge alimwaga machozi kwelikweli kwa kumlilia mwanae lakini hilo halikumuondolea tuhuma yake ya kuiba mtoto.

Bila kuchelewa , askari walimwagi maji gari hilo kisha wakapulizia pafyumu na kisha wakawambia,

” Sasa tukio la kwanza tumelimaliza!, kinachofata tunataka mtoto wa watu!. Panda gari wapuuzi nyie!”

Waliwapandisha gari kisha wakawaburuza kituoni ndipo walipoanza kula kichapo cha mbwa koko lakini hawakuweza kutaja wapi alipo mtoto.

Huko kwa Braison, watu walizidi kushangaa huku kaburi likiwa limebaki wazi.

” Huu mchezo mbona unatuuacha midomo wazi?” Mzee Kipara aliongea huku Braison akiwa ameshika tama.

Sasa kila mtu alianza kuongea ya kwake kulingana na alivyoona.

Kilichowashangaza ni juu ya  Bonge kudai maiti ni ya kwake ndipo walipoanza kufatilia kwa kina.

Katika taarifa za awali ambazo walizipata, walisikia kuwa mtoto wao aliuzwa tena akiwa hai na wahudumu hao.

Habari zilisambaa kwelikweli ndipo askari wakishilikiana na wanakijiji wote walipoanza msako kila sehemu walau wapate uhakika wa wapi alipo mtoto huyo.

Mchakato huo haukufanikiwa kabisa ndipo walipoamua kumuachia Mola kwani walikuwa wameshalia vyakutosha.

Walichukua udongo kisha wakanyunyuzia majivu kwenye kaburi na kuzika hivo hivo huku taharuki ikiwa inaendelea kutanda.

Kesho yake, walianua matanga na watu wakatawanyika isipokuwa wanaukoo ambao walibaki kwa kikao maalumu.

Kutokana na sakata hilo, uongozi wa hispitali walipata taarifa juu ya kukamatwa kwa wafanya kazi wao kwa tuhuma za kuuza mtoto ambaye alidaiwa kutolewa kafara.

Walifatilia mpaka kituo cha polisi na kuonana na mkuu wa kituo ambaye alimhakikishia kuwa watuhumiwa hao wako hapo kisha akamsomea kosa linalowakabiri.

Baada ya kusomewa, alinyoosha mikono juu na kumwambia hatua kali za kisheria zitumike kulingana na sheria inavyosema.

” Kamanda mimi sina utetezi wowote juu ya wahudumu wa namna hii. Tuko tayari kutoa ushirikiano kadri tutakavyohitajika ili iwe fundisho kwa wengine’ alimwambia.

Kabla ya kuondoka, Askari aliwafungulia kisha wakamuona mkuu wao ndipo walipoinamisha vichwa vyao kwa aibu huku machozi yakiwa yanawatoka.

” Mnafikia hatua ya kufanya unyama huu ambao ni kinyume na maadili ya kazi zenu. Ona sasa!, mnatuaibisha!, mnakosa nini mpaka mnafikia hatua hii!. Sina utetezi wowote juu yenu kama “

Hawakujibu chochote balo waliendelea kulia tu.

Baada ya mda kidogo , walirudishwa ndani huku mchakato mzima wa kuwapeleka mahakamani ukiwa unaendelea.

Ni kilio na kusaga meno kwa watatu hao ambao walikonda kwa siku hizo huku wakitamani kuliona hata jua lakini hawakuweza.

Baada ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani kukamilika, waliwafungulia kisha wakawambia,

” Sasa nafasi ya mwisho ndo  hii!, mda huu mnapelekwa mahakamani kujibu tuhuma hizi ambazo kwa vyovyote vile lazima mkutane na hatia ya kifungo cha maisha jela. Kama mnajua wapi alipomtoto!, ebu ongea mnaweza punguziwa adhabu…”

” Bonge si useme wapi alipo mtoto?., kwanini tunateseka hivi jamani!, halikuwa kusudi lako lakini umetuponza. Tunakuomba sana uwambie ili watuachie jamani” Asia na Mariatabu walimwambia Bonge huku wakimwaga machozi.

” Mtoto nilimuacha nyumbani na wala sijamuua wala kumfanya chochote!, kama ningekuwa najua alipo nisingeteseka kiasi hiki. Niamini ninachowambia” Bonge aliongea kwa huruma.

Wakati wanaongea hivo kumbe walikuwa wanarekodiwa bila kujua kama ushahidi wa mwisho wa kwenda nao mahakamani.

Waliwatia pingu kisha wakapitia kwa Bonge na kumuhoji mlinzi,

” Mtoto mmemuweka wapi!” Walimtisha kidogo.

” Mtoto sijawahi kumuona kwa macho yangu na wala sijui kama kulikuwa na mtoto ndani humu” aliongea.

Bonge alimuangalia Mlinzi wake kisha akatikisa macho lakini hakuwa nachakumfanya.

Kutokana na maelezo hayo, moja kwa moja walijiridhisha kuwa huenda  walimtoa kafara hivo ni mda wa kuwapeleka mahakamani.

Waliwasha defenda na kuanza safari huku wakipitia hospitali ili kuchukua maelezo ya mwisho kwa Sarah ambaye yeye hakuwa anajua chochote.

Akiwa amelala huku kwa mbali usingizi ukiwa umeanza kumuishia gafla alihisi kitu kinamtekenya kwenye ziwa lake ndipo aliposhutuka.

Ile anageuka, alipiga kelele ya mshangao mkubwa sana kwa kile alichokiona.

Si kingine bali ni mtoto mchanga aliyekuwa amelala pembeni mwake huku akiwa analamba kidole gumba.

Mda si mrefu askari nao walifika hospitalini hapo ndipo walipomkuta Sarah akiwa amelala na kichanga pembeni.

Walishangaa sana mpaka wahudumu wote wakakusanyika.

Wakiwa wamesimama, kichanga hicho kiliongea,

” Wasameheni maana hawajui walitendalo ila wasirudie tena”

Sauti hiyo iliwafanya watu wote kukusanyika sehemu hiyo ndipo habari ziliposambaa mtaa mzima juu ya mtoto wa ajabu .

Sarah alifurahi sana kisha akapokelewa na mme wake Braison pamoja na wanakijiji wote kuelekea nyumbani.

Bonge aliachiwa kisha Asia na Mariatabu wakasamehewa ndipo walipoapa kutorudia tukio kama hilo.

Shangwe vifijo na nderemo vililindima nyumbani kwa Braison huku wazee na wanaukoo wakimuomba radhi Sarah kwa kile walichotaka kumfanyia.

Giza lilitoweka, nuru ikaangaza .

…..NA HUO NDO MWISHO WA SIMULIZI  YETU SEASON 1…..

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!