CEO ALINOGEWA NA UTAMU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 6
Nilipokea kipimo cha mimba nikaenda chooni. Aiseeee sijui hata kinatumikaje, nilifanya kama alivyonielekeza Tima.
Nilitoka chooni nikamkabidhi shangazi kipimo.
“Ebu Tima nisaidie, unaonaje hapa”
“Woiiiiih! Nicheke kwanza🤣🤣🤣🤣. Bikra ya nyo……ko”
“Usiniambie kwamba ni kweli haka kajibwa kadogo kadogo kana mimba?” Shangazi alimuuliza Tima.
“Mama malaika wako ana mimba 🤣🤣🤣” Tima alisema hayo na kuendelea kucheka. Alicheka mpaka machozi.
Mie kusikia na mimba nilianza kutokwa jasho kwa uoga, sura yote ililowa jasho.
“Ebu kelele mb….wa wewe. Eti Shaznah una mimba kweli?” Shamgazi aliniuliza sikuwa na lakumjibu maana mie mwenyewe sijui kama na mimba.
“Mpuuzi wewe si nakuuliza huna mdomo au?”
“Shangazi mie hata sijui”
“Hujui nini sasa na wewe ni binti kigori au sio bikra wewe?, niambie ushatolewa na wahuni na wewe eeeeh! Shangazi alikuwa anaongea kama vile amepagawa.
” Uwiiii! Milioni 20 hizo nimezikosa, hapana sitaki kuamini mimi. Ebu twende hospitali labda Tima ni muongo tu anakuonea wivu. Twende haraka” shangazi alianza kunivuta nakwambia mkuku mkuku. Njia nzima anaongea peke yake.
Kumbe bikra yangu ilikuwa iuzwe milioni 20 na kwa navyomjua shamgazi asingenipa hata buku.
Tulifika hospitali taratibu za kupimwa mimba zilifuata. Majibu yalitoka kweli mie huyu mjamzito, kama utani shangazi alilia mbele ya doctor.
Tulitoka ofisini kwa doctor huku shangazi analia. Nilijua kinachomliza ni milion 20 ambazo alishazipigia hesabu na matambo kwa mashoga zake.
“Umejua kunizalilisha uwiiiii! Nitaweka wapi sura yangu mimi wewe Shaznah”
“Shangazi naomba unisamehe” niliomba msamaha na kuanza kulia.
“Ubwa wewe unalia nini sasa, si ungeniambia tu kuwa ushavuliwa chupi kuliko kunificha. Ona sasa nilivyoghalimu mavitu kibao pesa yangu imeenda bule”
“Yaani Shaznah hata sikuelewi. Ebu twende kwanza nyumbani”
Tulifika nyumbani swali la kwanza kutoka kwa shangazi alitaka kujua nani aliyenitoa bikra na sio mimba ya nani.
“Shangazi nitakwambia ukweli.
“Niambie sasa, nani aliyekutoa bikra anilipe pesa zangu, mimi sio mjinga ki hivyo” shangazi aliongea kwa ukali.
“Eeeeeh kumbe mmeludi” haya nini kimetokea huko?” Tima aliuliza.
“Ana mimba kweli huyu mjinga”
“Kwaiyo unaamuaje mama?”
“Huyo aliyemtoa bikra lazima alipe pesa zangu”
“Shangazi nilibakwa”Niliongea hayo huku nalia.
“Nini?, wewe mtoto usinitanie sina mdhaha mimi. Twende kwa huyo bwana yaani usiku huu huu wa saa nne mguu wako mguu wangu”
“Shangazi ni kweli nilibakwa na huyo mwanaume hata simjui mimi, uwiiiih MUNGU wangu nisaidie mimi” Ilibidi nimueleze shangazi ilivyokuwa ila hata hakunielewa kabisa.
Kibao kilimgeukia Tima sasa, kwanini alikula zile pesa alizoniibia peke yake.
“Labda zile pesa leo hii zingenifuta machozi. Nyie mb….wa wote sitaki kuwaona nyumbani kwangu, tafuteni pa kwenda si mshakuwa nyie.
Shangazi aliongea hayo, nilipiga magoti kumuomba msamaha nilisukumiwa huko.
” kuanzia leo usinijue kabisa na nikifa usinizike” shangazi aliongea maneno makali huku analia.
“Khaaaa! Weee mama, maneno yote hayo kisa tu bikra au una mengine?” Tima alimuuliza mama yake maana aliona kabisa amevuka mipaka.
Shangazi alikuwa serious hatanii alitufukuza usiku huo huo.
“Kazi kwako, mie naenda kulala kwa bwana wangu na ndo maisha ya sogea tukae hayo, mwenzangu sijui una pakwenda?” Tima aliongea hayo huyo akaondoka hakujali chochote……..
SEHEMU YA 7
Sikuwa na pakwenda mimi. Nilitafuta tu sehemu ya kulala, nilipata gofu nikalala humo.
Asubuhi palikucha sina hata mia mbovu. Tumbo nalo linahitaji chochote kitu, yaani njaa imenikamata vibayano.
“Nilijiongeza kutafuta kazi hata ya kusugua sufuria kwa mama ntilie nipate mia mbili ya andazi.
Katika kuangaika huku na kule ndipo nikapata kazi kwa mama ntilie. Nilipewa kazi ya kuosha vyombo ili tu nipewe chai na chapati.
Nilikuwa naranda tu sijui hata naenda wapi ilimladi tu natembea. Miguu nayo ilichoka sasa. Nilitafuta kimvuli cha mti nikaka hapo. Sikujua hata ya maisha haya nayoishi ni ipi.
Nikiwa hapo chini ya mti nilianza kulia.
“Leo hii kama wazazi wangu wangekuwa hai mimi Shaznah nisigekuwa hapa” Basi nikiwa nalia pale chini ya mtu nilistushwa na sauti ya mtu akiniongelesha.
“Weee binti?” Niliinua kichwa changu kumtazama mtu yule.
Alikuwa mama mtu mzima wa makamo tu.
“Ujue nimekuona muda mrefu hapa unalia tu. Hii ndo dunia na watu wenyewe ndo sisi binti. Haya unalia nini sasa mpaka usichoke na ulivyo mzuri hivyo?”
“Maisha tu mama”
“Sasa kulia ndo suluhisho eeeeeh! Ila lia mwaya upoze machungu” mwana mama yule aliyasema hayo alafu na yeye alikaa pembeni yangu. Wacha tuanze kulia wote.
Yule mama alilia kuliko hata mimi, sijui alikuwa analia nini. Ilibidi mie ndo nianze sasa kumbembeleza.
“Basi mama nyamaza. Nyakati ngumu ni mapito tu. Amini kila gumu linakuja na neema. Nyamaza usilie mama”
“Niache tu nilie hujui tu namna moyo wangu ulivyo na maumivu makali, ninapoona mtu analia mbele yangu amanikumbusha mambo mengi sana”
“Basi mama nimenyamaza sitalia tena”.
“Ni kweli hutolia tena?”
“Ndiyo nakuahidi” aliacha kulia alijifuta machozi alafu aliniuliza naitwa nani.
“Naitwa Shaznah” Aliniuliza kwanini nalia, sikutaka kumficha nilimueleza ukweli wote. Basi kwa huruma yake aliniambia twende kwake yupo tayari kunisaidia.
Niliongozana na mama huyo mpaka nyumbani kwake. Maisha yake ya chini sana(kwangu pakavu)
“Hapa ndo nyumbani kwangu, kama umepalidhia utaishi hapa na mimi nitakuwa mama bora sana kwako. Ukiniita mama nitaitikia Abee mwanangu”
“Asante mama kwa moyo wako wa upendo. Wewe ni mama yangu” Tulikumbatiana na wote tulianza kulia.
Sikujua yule mama anapitia mambo gani maana alikuwa akianza kulia habembelezeki mpaa ahamue mwenyewe kunyamaza.
“Kuanzia sasa nitatambulika kama Mama Shaznah, wewe ni binti yangu na naamini utakuwa faraja kwangu, mimi maskini sina cha kukupa Shaznah zaidi ya upendo wa mama ambao unautakwa kwa muda mrefu”
“Hilo ndo kubwa mama kuliko yote”
Mtaani anafahamika kama Lissa. Lissa alipitia mazito sana kwenye ndoa yake na chanzo ni yeye kubeba mimba alafu zinaharibika. Mwisho wa siku hata mimba za kuharibika hakupata tena. Maneno yakikuwa mengi sana kwa ndugu wa mume na hata kwa ndugu zake. Walimuita mchawi anakula watoto wake. Usaliti wa nje nje kwa mume wake ulianza.
Maneno yalizidi zaidi baada ya mume wakd kumpa ujauzito mchepuko, hapo ndo mpaka familia yake ilimtenga wakisema ni mchawi.
Mwanaume alimfukuza kwenye nyumba waliyojenga wote, maana aliolewa mwanaume hakiwa ana kitu, walitafuta wote mpaka kuwa wafanya biashara wakubwa mwisho wa siku mwanaume anamfukuza kama mbwa.
Hakuwa na pakwenda alitanga huku na kule mpaka alipopata kazi kiwandani ndipo alifanikiwa kupanga chumba cha giza na kununua godoro dogo. Pesa aliyokuwa analipwa kwa siku ni 7000 tu. Lissa alikuwa mlevu kupindukia tena mnywa gongo.
Basi akilewa sasa ndo analia weeeee mpaka anapitiwa na usingizi. Hayo ndo maisha ya Lissa…………
SEHEMU YA 8
Nilianza maisha mapya kwa Lissa. Alinijali mno na alionyesha kunipenda sana sanaaa.
Ukaribu wangu ulisaidia kidogo kupunguza kunywa pombe.
“Nataka niwe mama bora sio bora mama. Siku zote nilimwambia MUNGU kama akinijaalia na mimi kupata mtoto basi nitakuwa mama bora sana kwa mtoto watoto wangu. Wewe ni baraka kwangu haijalishi hata kama sijakuzaa ila naamini wewe ni zawadi ambayo MUNGU ameileta kwangu.
Lissa aliongea hayo tulipokuwa kwenye jamvi tunakula chakula cha usiku.
Tangu nianze kuishi nae Lissa ni mtu mwema sana kwangu.
Siku zilizidi kukimbia mimba nayo ilianza kunisumbua, kuumwa, kutapika, muda wote mwili umechoka. Sikuweza kufanya chochote nilikuwa mtu wa kulala tu basi na mimba yangu ilikuja na uvivu ile mbaya ila yote hayo lissa hakunichoka aliendelea kunihudumia na kunipa kile kilicho ndani ya uwezo wake.
BAADA YA MIAKA MIWILI.
Nikiwa tayari naitwa mama Gift, mwenyewe nina binti yangu mzuri sana mtoto sijui ndo kafanana na baba yake maana hata huyo baba yake simjui kivile nilimuons usiku mmoja tu tena kwemye mwanga wa taa na sio mwanga wa jua🥹.
Siku moja Lissa alipoludi kazini nilimuomba tuzungumze.
“Mama umenilea vya kutosha sasa, umeniangaikia sana inatosha sasa”
“Mama Gift unataka uniache na wewe, unataka kuondoka uniache pekee?”
“Sina maana hiyo mama yangu, amini wewe ndo mzazi wangu siwezi kukutelekeza. Maana yangu ni kwamba naomba upumzike na ridhiki nitatafuta mimi”
“Hapana, sipo tayari kwa hilo. Siitaji uteseke binti yangu”
“Hayo sio malezi mama yangu. Yatima hadeki mama, lazima nifanye kazi ili na wewe ule”
“Kazi gani sas”
Nilimuomba Lissa mama aniunganishe kazini kwake mbadala wake alafu yeye abaki nyumbani kumlea Gift. Alikubali Japo singo upande.
Kesho yake asubuhi tuliongozana wote mpaka kazini kwake na Gift wangu akiwa mgongoni.
“Hapa ndo napofanyia kazi”
Alikuwa anafanya kazi kiwandani. Kiwanda cha ngano. Alinieleza ugumu wa kazi ila nilimwambia nitakaza sitamuangusha.
Basi niliamdikishwa mbadala wake na siku hiyo hiyo nilianza kazi. Kazi zilikuwa ngumu masaa yote ni kusimama tu.
“Aiseee kweli umasikini ni mbaya sana yaani tangu asubuhi nimesimama alafu ndo nalipwa elfu saba tu” niliyasema hayo huku naitazama hela niliyopewa.
Mwili wote ulikuwa unauma asikwambie mtu. Sema ndo maisha niliendelea kukaza ndani ya wiki mbili tu milizoea na huko nikapata marafiki wapya.
“Watu wengine hamfai hata kidogo kufanya hii kazi sijui hata kwanini mnalazimisha kuwa hapa?” Rafiki yangu mpya Nyamizi aliongea hayo.
“Mimi nafaa kuwa hapa my dear, sina elimu ya kunipeleka ofisini na pia kumbuka nina mtoto, familia yangu inanitegemea”
“Shoga wewe bhana mzuri hustahili kujiumiza kiasi hiki kwanini usijaribu hata kuomba kazi usafi ofisini kwa boss?” Nyamizi aliongea hayo.
“Ofisini kwa boss?”
“Ndiyo na naamini Boss mwenyewe akikuona atapagawa niamini mimi kazi unapata vizuri. Mjini hapa unatakiwa kuwa mjanja mjanja usikae kinyonge sana. Huu mji hauhitaji unyonge” Nyamizi aliongea hayo, nilifikiria kwa dakika chache niliona Nyamizi yupo sahihi. Kazi ni ngumu sana.
“Sasa boss mwenyewe hata simjui”
“Ni nadra sana kumuona ila nasikia yupo na anakuwa ofisini kwake kumuona nje ya ofisi labda kwa bahati mbaya”
“Eeeeeeh! Kawa malaika. Sasa mie nitampataje?”
“Kumpata kwa huyu mtu ni kuomba muonana nae japo ni jambo gumu sana maana huwezi kuonana na boss bila kupita kwenye kila uongozi labda kama utajitoa ufahamu ndo utaweza kuonana nae kwa njia rahisi” Nyamizi aliongea hayo.
Milimuelewa vizuri nilikuwa tayari kujaribu bahati yangu. Kuanzia siku hiyo baada ya kutoka kazini nilikaa nje ya geti kumsubilia boss atoke niliwai gari lake na kumlilia shida yangu……………
SEHEMU YA 9
Ilipita week mbili pasipo kukunikiwa kukutana na boss.
“Nahisi kukata tamaa. Leo itakuwa ni mala ya mwisho. Kama hatatokea basi sitajichosha tena”
“Roho ya kukata tamaa ni umasikini. Mtu mwenye maono ya kufanikiwa hawezi kukata tamaa”
“Wiki imekatika bila kutokea”
“Mvumilivu hula mbivu” Nyamizi aliniambia.
Basi siku hiyo pia kama kawaida nilikaa nje ya geti kumsubilia boss.
“Wewe kila siku nakuona hapa una shida gani binti?” Mlinzi wa getini aliniuliza.
“Shida yangu ni kuonana na boss”
“Boss?, ukimaanisha mmiliki wa kampuni hili na kiwanda kwa ujumla?
“Ndiyo?”
“Mbona kama unapoteza muda wako bule binti au kuna agenda yoyote baina yenu amesema uwe unamsubili hapa”
“Vipi kwani ameshaondoka?” Nilimuuliza mlinxi wa getini.
“Sijui maana kiwanda hiki ni kikubwa nafikili ujapata nafasi ya kufanya utalii humu. Kuna mageti zaidi ya matatu so leo anaweza kuingilia geti hili ila asitokee hapa akatokea geti lengine ndo maaana nimekuuliza ka ana ahadi ya kuonana na wewe maana nakuona kila siku unamsubilia hapa.
Nilichoka mwenzenu baada ya mlizi kuniambua hayo. Alifunga geti akaludi eneo lake la kazi.
“Sina bahati mimi mtoto wa kimasikini” niliyasema hayo na baada ya hapo niliinuka huku najipangusa vumbi kwenye makalio yangu.
Mdogo mdogo nilianza kuondoka eneo hilo kwa mwenda wa kinyonge sana.
Kama hatua 20 hivi nilisikia geti linafunguliwa. Niligeuka nyuma nilishuhudia magari mawili ya kifahari yanatoka.
Moja kwa moja nilijua huyo ndo boss mwenyewe sasa.
Nilianza kuyapungia magari yale kwa mikono miwili kwa kuyasimamisha.
Huwezi amini ni kama vile hawakuniona hivi, kwani walinipita na kuniachia vumbi.
Aiiiih mie huyu hata sikukubali. Nilianza kuyafukuzia mbio mbio huku naendelea kuyapungia mkono. Yaani sikujali kabisa watu watanitazamaje kama mwendo wazimu au kichaa.
“Ni nani kwani huyo anayefukuzia gari?” Boss alimuuliza Dereva wake.
“Simfahamu”
“Simamisha gari”
Gari la mbele liliposimama na la nyuma lilisimama pia. Niliyafikia magari hayo nikiwa nahema balaaa!
Kioo cha nyuma ya gari la mbele ambalo ndilo alikuwepo boss kilishushwa.
Nilisogea usawa wa kikoo. Bado nilikuwa nahema kwa nguvu mpaka uwezo wa kuongea ulipotea.
Nilipewa chupa ya maji ninywe kwanza. Niliipokea ile chupa nilikunywa maji yote.
“Niambie shida yak” Sauti ya mwanaume rijali ilipenya vizuri masikioni mwangu. Si ndo nimtazame vizuri sasa. Nakutana na kijana Handsome balaaa!
“Zungumza au upo hapa kwaajili ya kunishangaa tu?” Aliniuliza. Wenge likanitoka sasa.
“Hapana nisamehe kwa kukuwekea mshangao. Mimi ni mfanya kazi wako kwenye kiwanda chako. Nilikuwa naomba”. Kabda sijamaliza kuongea Boss alimwambia dereva aliondoe gari.
Nyie sikuamini kama nimefanyiwa madharau namna hiyo🥹🥹🥹.
Ndani ya gari dereva alivunja ukimya kwa kuzungumza.
“Mr Remmy umegundua nini kutoka kwa huyo binti?”
“Hakuna chochote nilichogundua kutoka kwake zaidi ya usumbufu tu”
“Ni binti uliyelala nae usiku mmoja pale hotelini kama unakumbuka” Dereva aliongea……….
SEHEMU YA 10
“Ni lile tukio la miaka miwili nliliyopita. Namkumbuka vizuri huyu binti kwasababu mimi ndiye niliyemleta kwako”
“Nyamaza usizungumze tena mpaka pale nitskapohitaji kuzungumza hili swala” Ceo Remmy aliongea.
Ukimya ilitawala mpaka anafika kwake.
“Umeludi muda muhafaka sana Nari yupo hapa” Mama yake alimuambia.
“Nimechoka sana leo naomba nipumzike na isitokee nikasumbuliwa. Mwambie Nari tutaonana kesho Asubuhi”
“Kwaiyo hata chakula hautokula?”
“Kama nitahitaji nitakwambia” Remmy aliyasema hayo akaenda chumbani kwake.
Mama yake ni mtu muelewa na huwa hapendi kumkwaza kijana wake hivyo alitumia hekima kumtuliza Nari asiweze kumsumbua Remmy.
Nilipoludi nyumbani nilipokelewa na Gift, mwanangu mwenyewe anapenda kucheka yaani kitenda cha kuniona tu mama yake anakuwa kwenye furaha sana.
Nilivuta kumbukumbu kilichotokea muda mchache uliopita.
“Mbona kama namfahamu au wamefanana?, alafu mbona kama vile ile ni sura ya mwanangu mtupu yaani amefanana na gift mpaka rangi” Niliongea mwenyewe yena kwa sauti kubwa.
“Nani huyo kafanana na Gift na asije kuwa ndo baba yake”
“Yaani mama hata sielewi? Ila bhana mie siwezi kumsahau sura mtu aliyenitoa bikra yangu. Ni yeye bhana baba Gift” niliongea hayo.
“Nani huyo sasa si useme?”
“Unaweza usiniamini ila ukweli ni kwamba boss wa kiwanda cha ngano ndiye baba mtoto wangu”
“Khaaaaaa! Unasema kweli?, Inamaana Yule Ceo ndiye aliyekufanyia huo ukatili?”
“Huo ndo ukweli”
“Ebu subili kwanza nakuja” Mama aliingia ndani alitoka na gaazeti mkononi. Hili gazeti ni la miaka minne nyuma. Nililinunua huko barabarani baada ya kukutana na hili tangazo la nafasi za kazi kiwandani likiwa limeambatanishwa na picha ya mkurugenzi mkuu ambaye anafahamika kwa Jina la Mr Remmy na wengi tumezoea kumuita Ceo.
Mama aliyasema hayo huku anaitazama picha ya Remmy. Alisadiki ni kweli Gift ni copy ya Remmy.
“Aiseeeee! hata siamini kama mtu mzito kama yule anaweza kuwa mkatili”
“Kwaiyo unafikilia nini?” Nilimueleza mama namna nilivyokutana nae na hakutaka kunipa muda wa kunisikiliza.
“Mjinga huyu itakuwa amekukumbuka vizuri ndo maana amekukwepa, na kuanzia sasa mtoto atalea yaani katoto kanaishi maisha ya tabu huku baba yake ni mto mwenye pesa. Hili halikubaliki na ikitokea amekataa nitamshtaki”
“Mama usifike huko. Kwanza tambua hatuna uwezo wa kushindana na mtu mwenye pesa, Tuwe wapole tu na tufute kumbukumbu za nyuma. Zawadi amekuwa binti nachoamini dunia hii haina siri hata kidogo ipo siku kila kitu kitakuwa wazi ni swala la muda tu”
“Nakumbuka huruma, unyonge na upole kama wako ndo ulionifanya leo nipo hapa. Kuna muda inabidi tuwe ngangali ili tupate haki yetu ila kama wewe mwenyewe unaona upo sahihi siwezi kupinga maamuzi yako” Mama aliongea hayo.
Upande wa Remmy aliludisha kumbykumbu zake nyuma. Alikumbuka vizuri namna alivyonitendea.
“Nilimkatili sana huyu binti ila inabidi nifanya kama simjui maana ni jambo lililopita muda mrefu sana. Ila napaswa kulipa ubaya kwa wema nitafanya jambo kwaajili yake ila sitotaka ajue kama ni mimi ndiye nimemfanyia………..Je ni jambo gani Ceo huyo anataka kulifanya kwa Shaznah mama mtoto wake……….
INAENDELEA

