KABLA HUJAONYESHA PICHA ZA MTOTO WAKO KWA WATU AU MITANDAONI, SOMA HII KWANZA
Kupata mtoto hufurahisha kila mtu, na si ajabu ukataka watu wamuone mtoto wako, wengine utawarushia picha za mwanao huko mitandaoni. Sasa, hii dunia ina mengi sana ndugu yangu, sio wote watafurahishwa na wewe kuwa mtoto, wengine hiyo picha ya mwanao wataitumia katika mambo mabaya sana, hebu endelea kusoma hii makala
UCHAWI WA PICHA
Labda maana sahihi ya uchawi haifahamiki kwa watu wengi ndio maana watu hawana tahadhari kwenye mambo yao.
Uchawi ni nguvu hasi inayoweza kumuingia mtu yoyote ikiwa amekusudiwa au bila kukusudiwa. Uchawi unaweza kumuingia mtu kwa kutumia athari yake. Athari ni nini?.
Athari ni kitu kinachomuunganisha mtu na kitu chake. Mfano. Nguo, Mabaki ya chakula chake, Picha yake, Jina, Jasho lake au mate, Kiatu na hata sehemu aliokanyaga mtu.
Vyote hivi vinaweza kutumika kurogewa na ukarogeka bila shaka. Sasa lazima uwe na tahadhari kwenye miasha yako kwa kila hatua zako hasa siku hizi.

Picha kama hii ya mtoto imetumika kumuumiza huyu mtoto kwa uchawi. Matokeo yanaweza kuwa mabaya pengine kwa maradhi au mtoto kuwa hayupo sawa kiakili.
Usitume picha za watoto wako mitandaoni au zinazohusu mafanikio yako hatari muwe munaelewa ubishi ndio chanzo cha matatizo mengi leo duniani.
Chanzo: Abdulrazaki issa


1 Comment
Noma sana