MKE WAKO NI MZURI SANA, NI VILE TU UMEMZOEA SANA
Wanaume wenzangu
Mke wako anawezaje kuonekana mbichi na mrembo kama mchepuko wako huyo na wakati umemzalisha watoto na amejifungua mara 5,Umempeleka leba (labour) mara 5 amenyonyesha kwa awamu 5 ya vizazi vitano vyenye umri tofauti tofauti, pamoja na Masumbufu ya kulea na kuhudumia watoto wako hao watano hadi wengine wamefikisha miaka 20!??
Yale mabasi ya njano kila siku anakimbizana nayo asubuhi na jioni kuhakikisha wanao wanaenda shule na kurudi salama nyumbani,anawapikia watoto wako hao watano wote kila siku .Amekuwa nao hospital kwa miaka miaka ,amelala macho siku nyingi watoto wako wanapougua usiku.Kelele na usumbufu wa watoto wako na wengine wakiwa wakorofi wote aliwavumilia! Mkeo ni bora kuliko huyo Mchepuko (side Chick)
Umempa mimba 5 kwa vipindi mfululizo na zingine alijifungua kwa kisu,je unataka awe mrembo kwenye tumbo lake kama huyo mchepuko wako?? Kifua chake ndicho chakula cha watoto wako hao watano hakiwezi kikawa l sawa na cha huyo mchepuko ambaye kila akipata mimba anazitoa na P-2 ndicho chakula chake , kapitia mengi akiwa mjamzito mara kutapika,mara mgongo uume ,mara adondoke ,mara atokwe damu nyingi ,mara skate tamaa ya kuishi na wakati mwingine alinusurika kufa wakati akijifungua ,hayo yote huyakumbuki ,unalokumbuka tu ni kwamba yeye siyo mrembo na mzuri (romantic) kama mchepuko wako! Kumbuka hata huyo mchepuko anaonekana mzuri kwakuwa hauishi naye!
Haya tufanye hivi,Mchukue huyo mchepuko wako mlete kwenye majukumu ya mke wako uone kama atayaweza hata kwa wiki mojaal! Wanaume wenzangu tujifunze kuwaheshimu wake zetu wanapitia magumu mengi na wanatifanyia mambo mengi mazuri ambayo hiyo michepuko haiwezi hata kidogo!
Maisha ya ndoa siyo NGONO tu yamebeba mambo mengi sana ,heshimu sana huyo mkeo maana anakulelea watoto wako ambao ni damu yako jambo ambalo kamwe huliwezi na usingeliweza pekee yako!
Usisahau alivyokuwa wakati unamchumbia ,kisha mwangalie alivyo kwa sasa ! Hali aliyonayo kwa sababu wewe umechangia maana wanawake hubadilika wanapojifungua na kadiri maisha yanavyozidi kusonga mbele.
God bless every hardworking mother, wife and to all the caring husband’s.
Mungu awabariki wamama wote ,wake wa waume wasiowatesa waume zao ,wasioona haya kuwafanyia mema waume zao.
Ujumbe wangu upo kwenye 1 Wakorintho 7 :1-7 Wanawake msiwanyime TENDO LA NDOA waume zenu maana huo ndio udhaifu wao mkubwa!
Chanzo: Jamii Forums

