MKE MMOJA, WAUME WAWILI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
“Tukutane hoteli ya Seven Silva, saa moja na nusu, kila kitu juu yangu, usikose, naomba uwahi nakupenda sana.”
Ujumbe huo alitumiwa Fakri, alifurahi na kurukaruka huku akiujibu kwa hisia ya furaha mno. Hakuwa peke yake, hata Gastoni alitumiwa pia, naye kwa upande wake alifurahi sana, mapema akaanza kuandaa mavazi.
Fakri na Gastoni hawakujuana, aliyewatumia ujumbe aliitwa Leki. Yeye ndiye aliyewajua wote hao wawili. Leki alikuwa ni mwanamke mrembo asiyefanana na tabia zake. Alikuwa na pesa za kutosha, aliweza kufanya lolote alitakalo.
Majira ya saa moja kamili Fakri ndiye alikuwa wa kwanza kufika. Hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano, utulivu na aina ya watu waliokuwa hapo vilisadiki kuwa masikini hakutakiwa hapo.
Fakri alipokelewa vyema na mrembo ambapo alipelekwa mpaka kwenye meza aliyotakiwa kukaa.
“Karibu sana, furahia huduma zetu,”
“Ahsante.”
Mhudumu huyo mrembo mwenye sauti nyororo alipomkarimu aliondoka.
Fakri alipoangalia vizuri hiyo meza aliona viti vitatu, palikuwa na jina lake hapo mezani ule upande aliokaa. Akaona pia jina la Gastoni upande wa kiti cha pili, na cha tatu kiliandikwa jina ambalo alilifahamu, jina la aliyemfuata hapo, Leki.
Ilipofika na robo, Gastoni aliwasili. Naye alipokelewa vyema na kuletwa alipo Fakri, akaketi ule upande uliokuwa na jina lake. Wakasalimiana vizuri na Fakri kisha kila mmoja akabaki na maswali mengi kichwani.
Kimya kilitawala kwa upande wao ambapo muda huo Leki alikuwa kitambo ameshawasili Hotelini hapo,
“Ila shoga yangu watakuelewa?”
“Hawana kazi, hapa mjini wanatangatanga tu, wataanzaje kukataa?”
“Ila ni wazuri, mimi nimemtamani tu yule mweusi,”
“Mmh…yatakushinda!”
“Yule mweupe ni anaitwa nani?”
“Fakri, mweusi ni Gastoni…”
“Sawa wame zako ndio hao wamefika wanakusubiri,”
“Acha tu!”
Huyo alikuwa ni Leki akijadiliana na rafiki yake aliyeitwa Paula. Siku hiyo Leki alikuwa amevalia gauni fulani lililombana na kumchora umbo lake, lilikuwa fupi na mpasuo mrefu uliopelekea mpaka nguo yake ya ndani kuonekana.
Hilo gauni kwanza lilikuwa jepesi, mgongo wake wote ulikuwa wazi na kuonyesha lile pindo la nguo ya ndani, kila alipopiga hatua,
..
lile gauni lilikuwa likipanda juu na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake kuwa wazi. Leki alivutia mno usiku huo.
Kwa mwendo wa madaha alitembea mpaka mezani hapo na kuwabusu wote wawili kwa zamu kisha akaketi. Wakaagiza chakula wakala kisha Leki akaanza kufunguka,
“Najua mtakuwa na maswali mengi sana, ila nimewaita wote kwa ajili ya jambo moja,”
Wote walikohoa kidogo kuweka koo sawa na kuendelea kusikiliza,
INAENDELEA

