AFANDE INAUMA JAMANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 11
“Enhe kwahyo hutaki kuwa mpenzi wangu au? mbona unataka kunichekesha sasa hebu kaa hap la mama tuondoke, nikupeleke nyumbani ukapumzike afu tutaendelea kubishana baadae “
“Wee mimi nyumbani naenda mwenyewe niende na wewe yatokee yaliyotokea tena koma mimi bado naumwa samahani nikome kabisa π” nilisema nikiwa naondoka zangu naelekea kutafuta usafiri maan hal lazima nipande bajaji au daladala kwa hii hali siwezi kupand boda kama nilivyozoeaa japo kwetu ni magomeni kanisani kwahyo buku 2 tu nafika na boda ila kwa jinsi nilikuw naumia nisingeweza kukaa kwenye boda hat, nilishangaa nabebwa kama kamwizi jamani π, mpaka nafikishwa kwenye gari nikafungwa na mkanda “Haya kaa utulie sitaki kelele sawa ? nakupeleka kwenu toa maelezo ” nilimpa kishingo upande huku moyoni naomba dua yaliyotokea yasitokee tena maana π , jamani inauma kila nikikumbuka nafumba macho bwana, akanipeleka mpaka nyumbani, hee saa ngpi asitake kuingia mpoka ndani, nikamwambia koma wewe , kwetu kufanya nini kama sio na umbeaa mwanaume mzima π? eety anasema anataka kuwasalimia wazazi wee naijua hyoo akanichome au ? nikamgomea nikamwmabia atakuja siku nyingine nikaingia ndani sasa namkuta mama amekaa baba alikiwa ameenda kuangalia mpira kwenye viband umiza maan nyumbani Azam ilikuw imeisha
“Enhe bila salamu, toka lini umeanza kulala kwa kina Nasra bila taarifa wewe mbona unataka kunipa wasi wasi nikajua hata umekutana na tatizo jamani wew mtoto mbona umataka kutupa presha hivyo wazazi wako jamani sisi tushajizeekea ujue ? hebu usiwe unafanya vitu vya kijinga namna hyo afu ulivyo ma kusudi ukawa hupokei simu wewe hyoo tabia nishaikataa kabisa humu ndani alafu wewe hata husikii yaaani π, haya kaonge sijui ubadishe hizo nguo za watu maana najaua sio zako uje ule hapa ” Mama alisema
“Sawa mama nimeelewa kipenzi mama, sitorudia tena sawa mama yangu βΊοΈ” nilifanya aa alivyonambia kisha nikaenda kulala kesho ilikuwa jumapili nakuwaga sina ratiba ya kwenda dukani buana naelewa, nikawa nimetulizana zangu tu , navuta usingizi huku nipo nakumbuka lile tukio lililotokeaa kule π, mara ghafla sms inaingia kwa simu yangu , inasema “KESHO NAOMBA TUKUTANE AS MEETING KUNA KITU NATAMANI NIKUAMBIE HARAKA SANA LATIFA , TUKUTANE PAPAROT HOTEL” Hee ilikuwa inatoka kwa RPC, nikajuaa tu tego hilo hyo paparotomy hotel huwa wanenda watu wazito wazito mimi naishia kupasikia tu, kama Zebra tu kwenyewe sijawahi kufika huko paparot ndio nitakanyaga, nikaamua kabala ya yote kwanza, nimpigiee kwanza Naa anishauri nikamuuliza akanambia niende, yaani akanipa na memory kwamba kuwahi kataa maneno nimsikiliza yaani yupo kama vile yeye ndio mama yangu yaani π π€£π
Basi kesho yake natafuta nguo ya kuvaa amaana naenda sehemu yenye hadhi yaanin, lakini sasa π, ngo ya kuvaa ninayo basi au ndio vile ukiwa na mtoko huoni nguo π€, nilichagua mpkaa narudiaa nguo sipati mwisho ndio nakuja kubahatisha gauni langu la Pink ya manyoya manyoya, nikasema hi nikivaa lazima nipendeze βΊοΈ
SEHEMU YA 12
Niliiivaa bwana asee nilijua kunoga yaani nilipendezaa mpaka nikajiona kabisa hapa nimependeza yaani kama kuna kiumbe kimenoga baasi wa kwanza ni mimi nilipendeza mpaka nikapendeza tena yaani π₯³, nikawa najitizama kwenye kioo mara mbil mbili yaanila sijimalizi, kumbe nimekuja kumgundua kumbe nina kishepu bwana cha uchokozi nyie π€, na hivi ile gauni ni tait inikaaje ππ«£, aibu naona mimi nakwenda kwenye mtoko bwana, nilifika nikawa getini nilipoga simu, mlinzi ainielekeza mahali ambapo mtu ambae nina meeting nae nitamkuta nilienda jamani mbona alikuwa kapendeza mkaka keroo yaani kadamshi kinoma mpka sijui niseme nini yaani alipendeza kwa ufupi mpaka mimi mwenywe namtamani yaani π, ikabidi nisivunge nimsifiee maana alikuwa kavaa t-shirt lake la rangi ya dark blue na kadert yake ya kijivu na ile t-shirt ilikuwa imembamba balaa yaani mkaka kusema siwezi, imembana kwenye zile mbavu kitu ambacho kilimfanya aonekane, smart sana machoni mwangu π₯³π₯³,
“And you also unaonekana too beautiful much” alisema mimi hata sikueelwa ” Samahni mimi sikusoma hivyoo sielewi ukiwa unaongea tafadhari usiweke vingereza maaana najuaa ni siwezi kuelewa”
“Upo serious for sure hujasoma kweli?”
“Unatka ujue unipeleke shule au? kwani unaona naongea kicking hapa afu nimekwambia kwenye maneno yako usitie kingereza ntakupiga endeelea”
“Mwanamke mbabe weee ndio ulitakiwa uwe Afande sasa, maana sio kwa ukali huoo kipenzi khaa “
“Haya ukimaliza kuongea maneno yako naisubiriaa mada kuu nataka niondoke niende nyumbani maana baba na mama wapo wenywe sijui unanielewa weweπ”
“Sawa mimi natka nieleze hisia zangu, ni kwamba Latty mimi nakupenda sana ujue, yaani nilivyokuona tu nikajua wewe ni wa aina yangu maana napenda sana mwanamke muongeaji, mcheshi hana mambo mengi kama wewe yaani alafu mkweli sana nimependa nipo tayr kwa lolote, hata kutangaza ndoaa maana nataka nikupeleke nyumbani kwetu upo tayari kwa hilo?” Aliuliza, hee nilishangaa nyie sijawahi kukutana na mwanume hivi
“Unamaanisha kabisa au unataniaa?”
“Nipo serious naamaanisha nataka nikupeleke nyumbani wakufahamu maana nishamwambia mama nimepata wa kwangu wa kuendana nae hivyoo wakae mkao wa kula ubwabwa, wa ndoaa nataka nioe”
” wewe unioe mimi kabisa mimi upo serious π₯Ά, mim cha kwanza mimi sina mpango wa kuolewa labda sijui iweje, pili mimi sina hisia na wewe hat, tatu ambayo naona vyote vinawezekana ila hicho hakiweezekani ni kwamba mimi na wew hapana hatuendani maana mimi ni Latifa wee ni Frank unadhani ni sawa hilo ?” Nilisema
“Hapana hata hilo la tatu linawezekana kwasababu mimi naitwa Frank, ni jina lngu nimelipewa na wazazi wangu kabisa ila sio kwamba ni Christian hapana mimi ni Muslim kama wewe ulivyoo sema hili ni jina tu naitwa Frank Hamad Mustapha”
“Kwanini Frank?” Na mimi nae umbea sasa utakuja uniuee ila msomjai mimi mwenyewe naamini na wewe mwenyewe unatamani kujuaa kwanin Frank si eet ?
“Nitakwambia kila kitu …”
SEHEMU YA 13
“Enhe nakusikilizaa” mimi nae masikio yangu ka ya panzi
“Mimi hapa nilipozaliwa baba na mama yangu ni wanapesa nyingi sana ila kupata mtoto kwao ilikuw shida sana, walihangaika sana kunipata walitumia kila njia kunipata sas kuna mtu walimpta akwaaaelekeza sijui kuna nabii gani anatibu, haya maswala lakini ni wa upande wa Christian, mama na baba aikuwa washachoka ilibidi wakubaliane na kila kitu mama ikuwa tayari hata kuuwa na kutoa kafara kwa ajili ya hili ni miaka Mingi sema imepita ndio kwend kwa huyo nabiii sijui ndio waliombea sijui ndio mama kupata ujauzito wa kuzalikaa maana, ilikuwa kila akipata mimba inaporomoka kwahyo kwasababu walinipata kwa hivyoo ndio maana nikaitwa Frank kama vile hi jina linakuwa ni kumbu kumbu la jinsi walivyonipata kwa shida na taabu yaani ndio hivyoo mamy hakuna kingine kipenzi “
“Oooh ndio maana unaitwa Frank hapo nimekuelwa ngoja nikupe sasa book langu π€£ π€£ π€£, mimi hapa buana naitwa Latifa Shabani Kassim, ni mtoto wa uswahini nina miaka 28 mpaka sasa, kwetu tupo wanne, ila wote wakike na wote watatu washaolewaa yaani, na mimi hapa ndio mdogo wa mwisho japo naelekea kuzeeka ila nina akili za kitoto, mimi niligoma kusoma toka chekechekaa yaani sijasoma nasitaki kusoma, elimu kwangu haina faida kwanza, hao waliosomaa wengi nimewaona wanatanga Tanga tu mitaani bila sababu maalum, hivyoo mimi sijasoma ila hakuna Hesabu dukani iliyowahi kunishindaga yaani π€£, enhee hyo ni kwa ufupi na wazazi wangu ni wazee sana yaani , mhh hujanambia miaka yako” yaani nilijikuta namzoea hapo hapo, kiufupi mimi ni mtu ambae ukitka nikuzoee kuwa tu na story yaaan kukuozeaa ni haraka sana, haya kuw bubu sas nikuonyeshe vyenye na mimi nakuwaga sipendi watu kama hao
“Hhhh kwanini ila hujasoma mrembo kama wewe, japo kila mtu ana fikra ila mbona wapo waliosoma na wamefanikiw kama mimi, nikiamua kuwa daktari nakuwa maana kabla ya kuwa RPC nishawahi kuw daktari wa jeshi, baba alitaka anikabidhi kampuni ila nikaona nifanye kazi kwanza mambo mengineyatafuta, naelewa, enhe nina miaka 32 now, nakuomba unambie kama umekubali ombi langu maana kwenye vyote vinawezekana mim sitaki kukupoteza nimekupata unaendana na mimi”
“Ngoja nipe dk 5 narudi na jibu halisi ” nilitoka kwanza pembeni nikaenda kiteta na jinga lenzangu Nasra, akanambia nikubali niache ufala yani mtu ana pesa mimi naleta ujinga sio kweli, nilirudi nikakubali,
“Okay asante kwahyo keshokutwa ntakuwa free tutaenda nyumbani sawa haya kaongee kwanza na wazazi wako, mimi ndio nililokuitiaa hapa sawa?” Alisema Frank, akasema atanifundisha nyumbani pia, ila kabla ya kufika nyumbani kuna sehemu tulipitiaa kwanza tukalaa, sikuuliza kwanini hataukula PAPAROT, tulikula na tukalaa na ice cream, ndio tukaondoka,
Nilifika nyumabni nilishushwaa na gari kabisaa, leo nilimruhusu aje ndani, aliingia mpaka ndani akawasalimia wazazi mhh alitoka na baba je, na kumpa noti za elfu 30, hizoo ndio zilizozuaa mada hapo maana ndio lilikuwa swali la kwanza kwamba yule ni nani yangu
SEHEMU YA 14
“Enhe huyo ni nani mbona, kama kuna utofauti maana najua hunaga rafiki wa kiume, na huyu direct sip rafiki yako haya nambie huyu ni nani?” Aliuliza mama
“Mama naelewa kama ungeuliza hiloo huyu ndio sio rafiki yangu ila ntakuelezea kila kitu yaaan mama yangu usiwaze mimi tena kwenye hayo maswala ya kukuelezea na kukupea umbeaa wote nipo vizuri mama” nilisema nikawaambia kila kitu, ila mama ndio nilimwambia kuwa nimelala nae kabisa, mama alinichamba akaniona mimi mzinifu utasema yeye hajawahi kuwa binti π
“Haya ndio uolewe upunguze mdomo na kiherehere maan wewe unakihere here kama mkojo wa asububi naelewa vizuri hizoo akili zako haya, ndio utuliee kesho kitwa unaeda kutambulishwa hayo mambo ni mazuri ntawambiaa hata dada zako maaana unaenda kuzeeka sasa, kama wazazi wako tupo hivi wewe sasa si kabibi ka zamani kabisa π” mamaa anavyoongea hivyoo utadhani mimi na akina dada tumetofautiana miaka sana wakati tumezidia miaka miwili tu kuna wengine wamezidiana mwaka na miezi mama nae alikuwa anafutisha sana, wahenga wanasema Mbegu ya zamani ni kakamavu,
Usiku nilienda kupumzika maana hata hivi nilirudi usiku bwana, Alinipigiaa simu Frank tukaongeaa asee kumbe huyu Afande ni romantic jamani, ila japo nilikuwa na wasi wasi yaani mtu kakutana na mimi mara moja hata wiki hatuna anataka kunipeleka kwao, hivi wakaka wa hivi wapo au huyu ndio wale watoa kafara maana Afande mwenye hapana π, au kwasababu ana cheo π€, hayo yalikuwa ni mawazo yangu tu ya kipuuzi kuchwani niamua kulala zangu, kesho yake nilimwabia kila kitu Naa tulivyokuwa dukani, alifurahi utafikiri bwana kaambiwa naolewa kesho kutwa jamani π, hii siku aliwahi kuondoka, na mimi niliwahi kufunga duka hii siku nzima sikutafutw na Afande nilijua tu landa alikuwa busy na kazi kwahyo sikutaka hata mimi kujisumbua kumtafuta pia π
Hatimae siku ya kwenda ukweni ilifika bwana mhhπ, nyie acheni mtu anataka kunipeleka kwao nilikiw nachukulia utani ila hapa nilaamza kuwa serious maana hayo ni mambo ya kwenda kwa Mama mkwe kabisa, hata hivi Frank alinipigia simu mapema sana yaani π, mpaka nikawa najiulizaa akanambia nijiandaee, nilijiandaa nikavaa ile nguo yangu ninayoijuaa mimi nikivaa napendeza alikuja kanichukua muda huoo hata nyumbani hajajitambulisha mimi ndio nilimtambulisha kwa juu juu tu, wazazi waliruhusu niende tu maana mimi nae π, wanahamu niolewe hata buree eety nazeeka wakati mimi najiona bado mbichi na nilikuwa siwazi
Basi bwana kabla ya kwenda popote tulipitia kwanza saloon nikatengenezwee kwanza, nyie nilijua kupambwa tena walinipodoaa make up ya hadhi za juu yaani π, nilionekana π, sijawahi kupaka make up ya hivi mimi mtoto wa uswahili mtoto wa Magomeni kanisani, nilijua kupodokaa maana saloon yenyewe nilienda ya Hadhi kwa Shuu kama mnamisikia anapamba vibaya mnoo nilikuwa namsikiaga tu hatimaee leoo nimefanikiwa kupambwa nae, tukaotoka hapo moja kwa moja tunaelekeaa Sinzaa, napaelewa mpaka dukani kwa Esma nyie sijawahi kuwaza kama naweza kuingia dukani kwa huyu mdada π
SEHEMU YA 15
Alinichaguliaa abaya Fulani hivi, nyie ila Esma ni ana beii etty abaya laki 2, nilijua kuwaka jamani nilipendeza kuliko wanavyopendeza watu wengine mimi mwenyewe kabla ya kusifiwa nilijipa marks, nikajipiga picha japo nina infinix π€£ π€£ π, tuliondoka na gari mpaka maeneo ya osterbay Masaki hapo mhh kweye bonge la nyumba, kama vile kasri kwanza movie linaanza nyumba inafunguliwa kwa remote, jamani π, mwenye hela sio ndugu yako hhhh π€£, mpaka nikaanza kingiwa na wasi wasi nilikuwa naona kama vile. Jamani hapa siwezi kuingia nikawa nawaza nashuka kwa mguu upi hapa kwenye hivi vigaee nyie nishazoea kwetu cement na vumbi mtindo mmoja yaani nyie π, nilishuka yaani najiona kama vile takataka hapo π,
Nikanyooka mpaka, ndani niliwakuta wazee wawili, mwanaume na mwanamke wakiwa wamekaa hapo kwemye viti wametulia akili yangu ilinambia hawa ndio baba na mama wa Frank, hakuna kingine hapo au niache umbeaa bwana
“Mama huyu ndio Latifa niliokuwa nakwambia, ni mwanamke mmoja mzuri sana nampenda mnoo ndio huyu niliokuwa nasema namleta, nadhani mmemuona kwahyo kama kuna swali la kuumuliza muulize yupo hapa ” alisema Frank, mama yake alikuwa kavaa miwani akaishuhsa kidogo kwa chini, akawa ananitizama hii tabiaa siipendi π π₯Ά, naonaga kama vile mtu kanidharau na nisivyoipenda dharau, ni vile hawajui tu π
“Okay then binti tutaongea baada ya kupata lunch, hivyoo naomba tukapike kwanza” alisema mama yake na Frank nyie hapo mimi sijaelewaa nimekuja kushtka kwenye twende tukapike ikapasa niingie jikoni wee na kwenye kupika ni moto kinoma yaani π, nijaza viungo kwenye hivyo vyakula ila moyoni nipo nasema Hii familiaa ya wasomi sijui kama ntaiweza asee π, mama mkwe mwenyewe anavyoonekana ni ana nyodo balaa, tuliweka mezani mimi sikutaka kula sana japo napelekaa asikwambiee people π, walikuwa wanasema vingereza vyao mimi hata nilikuwa sielewi nilikuwa naona kama wananitukana nyie mimi mtu mimi akiongea kingreza mbele yangu naona kama ananidhihaki Fulani hivi, afu na kijana wao alikuwa anawasaport wakat anajua kabisa mimi sijui wala sielwi kitu pale π
“Okay then, binti kuna quality nazitaka kuzijua una miaka mingapi, umesoma wapi, elimu yako, unafanya kazi gani sawa nakusikilizaa endeleaa maaana mwanangu kanambia wewe una kila kitu anachostahiki kwahyo nadhani wewe unaweza ukajielewa just continue” aliongea mama yake na Frank, mimi kuna maneno nilikuwa simuelewi kabisa yaaniπ
“kwanza mama, samahani nimekuwa kama vile sikuelewi maana yake mimi sijawahi kusoma najua kiswahili ambacho kila mtanzania anaelewa kwahyo nakuomba uwe unaongea kiswahili, hilo la kwanza pili mimi nimetoka kwenye famili ya kawaida tu sijatokeaa hizii familia kama za kwenu, tunatagemea kula kama nikienda dukani tunapouza nguoo nadhani nimejielezea kwa ufupi na mmenielewa “
“What the hell, Frank huyu ndio mwanamke ulisema kuwa ana kila kitu hali ya kuwa hajasoma wala haelewi kitu upo serious kweli wewe ” Mama yake alionge kwa kufoka
Asee mimi niliona hizi dharau nilibeba pochi langu ilimradi mlango nilioingilia naujuaa, nikainuka sipendi mtu aniletee dharau za kipuuzi, nadhani hata wewe pia hupendi dharau
Inaendelea….π₯

