TUNA MIAKA 13 KWENYE NDOA, LEO ANASEMA MIMI SIO MWANAMKE WA HADHI YAKE
Mimi ni mwanandoa wa miaka kumi na 13 nimefunga ndoa kanisa lakini kwanzia tumeanza kuishi mikasa imekuwa mingi sana mume wangu kila mara huwa namfumania na wanawake anakuja anaomba msamaha namsamehe. Lakini kwa sasa ameona amtongoze mpangaji wetu na kuanziasha mahusiano na nimekuja kujua wameshapanga hadi mikakati ya kuoana na mume wangu ameeenda kwa mjomba wa huyo binti akaidai kuwa anahitaji kumuoa
Lakini kwa imani yetu ya kikristo hairuhusu kuwa na ndoa mbili tumeshauri na wasimamazi wa ndoa akaomba msamaha akasema aliteleza kumbe alifanya hivyo ili mambo yasiwe makubwa baada ya hapo kumbe kamfungulia ofisi na huwa anaenda kumchukua usiku ndio anarudi nyumbani hii hali imenichosha sana kikubwa yule mwanamke anampost mtandaoni lakini nikiuliza mume wangu anasema anapotezea nakusema havikuathiri chochote anaomba lazima amuoe kwa sababu ameona ni mwanamke anayemfaa kinachoniumiza sana nimevumilia kwa hali zote sasa kafanikiwa ndio anasema nataka niongeze mke naomba unisaidie kaka maana moyo wangu unavuja damu

