NINA MAHUSIANO NA MUME WA MTU KWA MIAKA 12 SASA
Mimi nina tatizo kwenye mahusiano yangu nilikuwa na mahusiano na mume wa mtu takribani miaka kumi na mbili sasa nimejaaliwa kuzaa naye watoto watatu lakini kwa miaka yote hiyo hakuwahi kunipa heshima kama mke wake yaani hakuwahi kunitambulisha kwao japokuwa nyumbani kwetu alikuwa anatambulika vizuri kama mume wangu,
Mwanzo alinishawishi sana kwa pesa alizonazo mpaka akagharamia kunipeleka chuo cha maendeleo ya jamii lakini nilitafuta kazi sikubahatika kupata kazi.Basi maisha yaliendelea akawa anakuja kwangu kwa kujificha yaani asijulikane kuwa yupo na mimi, kiukweli haya mahusiano sikuyapenda kabisa na hata yananimalizia amani sina raha na hata yananikosesha amani kwa maana mke wake alivyojua sehemu nayoishi alifika mpaka nyumbani kunifanyia fujo.
Nami nimechoka na haya maisha kila nikimwambia arudi kwa mke wake hataki anasema hawezi kuniacha kivyovyote vile na muda huo mimi sitambuliki kwao na hata mahari hajatoa, naombeni ushauri tafadhali nifanyeje ili niachane naye na asinifuatilie tena?

