JOIN US WHATSAPP
CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM
CLICK HERE
Nina Hamu Sana Ya Tendo, Mume Wangu Ana Kisukari
Kaka habari za majukumu? Kaka Mimi Ni mwanamke umri wangu miaka 32 Nina watoto wanne nipo kwenye ndoa. Kaka nahitaji ushauri japokuwa najua wapo watakaonitukana na kunikashfu ila nimekwama.
Mume wangu ana umri wa miaka 54 alikuwa vizuri tuu,ila akaugua kisukari kilichopo kukosa kabisa nguvu za kiume sasa hivi Kaka tangu mwezi wa 9 mwaka Jana Hadi Leo sijawahi kushiriki tendo la ndoa nikiwaza kuchepuka naogopa nawaza nitakayekuwa naye hataleta dharau kwa mume wangu?
Lakini pia sitamani kuchepuka na mtu wa maeneo ya karibu nataka awe wa mbali Sasa najiuliza sitaongeza mzigo wa mawazo Maana huyu kipindi akiwa mzima alinipiga matukio mpaka nawaogopa na wengine.

