Nimuoe Akiwa ana Mtoto Mmoja, Awe Mke Wangu, Au Abaki tu Kuwa Rafiki?
Hello habari, Naomba unipostie kwa fans nipate ushauri kidogo hapa……
Mimi ni mwanaume age 29 mwajiriwa Serikalini, nina mwanamke wangu ambae nilikuwa nae kwenye mahusiano kwenye miaka ya 2014, nikiwa form four, na yeye alikuwa form three kwa wakati huo
Sasa tulianza mahusiano kwenye hyo miaka 2014, mpaka matokeo yangu ya kwenda Advance ilivotoka nikaenda shule, huku bado tunawasiliana, nikamaliza six mawasiliano bado yapo
Sasa mtoto wa kike alianza kubadilika mdogo mdogo nlipoenda chuo Iringa, mpaka ikafikia wakati hatuna mawasiliano kabisa, nikamaliza chuo miaka mitatu yote nakuja likizo sina mawasiliano nae,
Sasa kuna kipindi fulani hiv mwaka 2020 nikatokea kumkumbuka, sasa kwa vile nilikuwa nafahamiana na dada yake, japo sikuwa na namba yake ikabidi nimfate inbox messenger kuomba namba ya mdogo wake, bila hiana akanipa, nikamtafuta nikajitambulisha kwamba mimi fulani nimekukumbuka tu nikupe hi,
Aliitikia salam, japo sio kivile… kumbe nikaja kugundua alikuwa na mahusiano na jamaa mmoja hivi rafiki yangu FB, maana niliona post yake jamaa kapost walikuwa wote, sasa mi uvumilivu ukanishinda ikabidi nimuulize vipi? Upo kwenye mahusiano? Alijaribu kukataa lakini mwishoe kanambia yaah nipo kwenye mahusiano sasa ningewezaje kukaa muda wote ule tulipopotezana??
Nikamwambia ahaa sawa, maana mimi Katika pitapita zangi FB nikakuona bhana jamaa kakupost..
Sasa mwaka 2022, dogo karudisha mpira kwangu kazidisha kunitafuta, kunipigia kwa sana, ila nikashtuka kidogo nikamuuliza vipi kulikon? Mbona siku hizi umewekeza sana time kwangu ukilinganisha na kipindi cha nyuma??? Alichonijibu ni kwamba, aaah bhana haya maisha yaache tu jinsi yalivyo mambo hubadilika….
Nikamwambia okay sawa, tukaendelea kuwasiliana hivo hivo kawaida, ila wakati huo tunawasiliana sikuwahi tena kumwambia mambo ya kurudiana kwani nilishaona kwamba huyu kuwa nae ni uongo, acha nifocus na mambo mengine,
Sasa nilichokuwa nataka niombe ushauri kwa fans wako ni hivii., mwaka jana 2024 huyo mdada kapewa mimba ambapo mwaka huu 2025 mwezi wa tatu aliweza kujifungua salama, lakini cha ajabu sasa wakati akiwa na hiyo mimba hakuniambia alikuja kuniambia baadae sana wakati anakaribia kujifungua, mimi nikawa nambishia kwamba hauna (why ni kwa sababu huwa naona anapost status haonyeshi kabisa kwamba ana mimba)
Sasa kuna siku alikuwa anaenda clinic kwa ajili ya ultrasound hakuwa na pesa, akanipigia akanambia rafiki yangu naomba unisaidie sh 5000 niende hospitalini, sasa mimi kwa vile nishamjua hali aliyonayo ikabidi nikajiongeza nikamtumia elfu 20, feedback kanambia asante sana umenisaidia mno,
Baadae sasa alikuja kunambia kwamba Mimi nilikuwa na mahusiano na jamaa fulani hiv ndo hivo kanipa mimba ila tulikuja kushindwana tukagombana, nikaachana nae japokuwa hakunioa bado, ndo maana nilikupigia unisaidie, maana mara nyingi namtegemeaga dada yangu hapa sasa leo alikuwa vibaya hana hata mia, mimi nikamwambia okay sawa hamna shida, wewe hiyo sijakukopesha nimekusaidia tu kwa hiyo kuwa na amani,
Mdada kweli Mungu kamsaidia kajifungua salama, mtoto wake sasa hivi anaelekea kutimiza mwaka kama sio miezi 10,
Sasa tatizo ni kwamba najikuta nampenda sana huyu mdada na ukizingatia ndo mtu wa kwanza mimi kuwa nae kwenye mahusiano, yaani mapenzi nilijulia kwake japokuwa hapo katikati tulipotezana, ila sasa kwa upande mwingine nikikaa nikiwaza huyu mtoto alienae nashindwa tena jinsi ya kuendelea nae japo hatujaongea mambo ya kuhusiana tena ila mawasiliano tunawasiliana vizuri, akiwa na shida namsaidia either ya mawazo au kifedha hivo yaani, nachompendea huyu mdada ni fighter yaani anapambana kwenye masuala ya kutafuta hela, kwa sababu ni mtu ana saloon yake sasa hivi kubwa tu ambayo dada yake baada ya kuona vile kaamua kumfungulia ili aiendeleze na kweli anaiendeleza kwa sababu ingekuwa ni mtu ambae hana mahesabu ya kesho angeiua mapema sana… na hapo mipango mingi tunapangaga sana kuhusiana na maisha hivo yaani…
Ila pia nimemuuliza vipi jamaa yako ambae ulizaa nae yuko wapi?? Una mawasiliano nae? Akasema hana ila anasikia kupitia kwa marafiki zake kwamba kashaoa tayari huko kijijini, ambapo ndo hofu yangu kwamba je mwisho wa siku hawatakuja kurudiana??
Naombeni ushauri jamani nifanyeje?? Nimuoe ingali bado ana mtoto mmoja?? awe mke wangu au abaki tu kuwa rafiki, nifanye kumtafuta mwingne,
Ahsanteni

