NIMEMPA KWA SABABU YA PESA ZAKE, YEYE ANATAKA KUMUACHA MKE KABISA
Naomba nisaidie kuposti kwa fansi wako nipate kushauriwa.Mimi ni Binti wa miaka 21 Ninaishi dar es salaam, katika maisha ya kuhangaika kujitafuta niliingia kwenye mahusiano na Mme wa mtu na huyu mwanaume Mimi sikumpemda nilikuwa kwake sababu ya pesa tu basi baada ya kuanza mahusiano tulidumu kama miezi mitano akaja kaniambia anataka anipeleke kwao wakanijue Mimi nikawa na pingamizi nikamwambia kuwa wewe si Mme wa mtu utanipelekaje kwenu?
Akasema kuwa Mimi simpendi nilikuwa naye kwa ajili ya kumchuna tu nikamdanganya kuwa mimi mbona nakupenda jamani akasema kuwa yeye ni Muslim anaruhusiwa kuowa mke wa pili basi nikaona sio shida nikakubali kwenda kwao kweli mama yake alinipokea vizuri tu na ndugu zake pia baada ya hapo nilirudi nilipo kuwa ninaishi shida kilicho nileta kwako ni kuwa huyu mwanaume simtaki nimejaribu kumuacha mara nyingi lakini ananifuatilia kila hatua anasema yeye hajawahi kuachwa nimeshamwambia Baki na mke wako.
Mimi nataka kuwa na vijana wenzangu hataki kusikia amehaki mpaki simu yangu mahali popote nitakapo kwenda anapajua nimeshamkataa mara nyingi haelewi kabisa nifanyeje naomba nisaidie kuposti nipate ushauri kwa watu wako

