Nimemlipia ajifunze Upambaji, Baada ya Wiki Mbili kaomba Talaka awe Huru
Mimi na mke wangu tulikuwa na miaka 6 kwenye ndoa, tulikuwa na watoto wawili tayari.
Mwezi wa 6 mwaka huu aliniomba tushauriane kipi afanye mana amechoka kuwa mama wa nyumbani, nikamwambia mke wangu kwani unakosa Nini? Akasema hakosi kitu ila tu na yeye anataka kuwa na mchango kwenye familia, ilibidi nimwambie atulie, lakini kadri siku zilivyo kuwa zinazidi kwenda akawa ana sisitiza kuwa anahitaji fani yoyote ajifunze, akawa ameanza na kununa, ikabidi Sasa nimwulize anahitaji fani Gani, akaniambia nimchagulie, nikamwambia siwezi kukuchagulia kitu ambacho sitoenda kufanya Mimi, kama wewe unahitaji kazi Ina maana tayari kichwani umesha jiandaa na kitu unacho hitaji kufanya.
Basi akachagua upambaji, nikamtafuta dada mmoja akawa ameniunganisha na dada mwingine ambaye ni mpambaji na anajihusisha na kutengeneza keki, akaniambia nimpe laki 5 tu Ili amfundishe mke wangu Kila kitu.
Ilibidi nitafute mdada wa kazi Ili mke wangu yeye awe huru na kujifunza.
Dada huwezi amini, baada ya wiki mbili tu mke wangu alinitumia sms nikiwa kazini, mume wangu Kuna kitu nahitaji kuongea na wewe naomba Leo ukitoka kazini uje nyumbani Moja Kwa Moja, nikamuuliza Kuna Nini? Akanijibu hapana.
Jioni nilivyo rudi tu, mke wangu hata hakupoteza muda, alifika na kuniambia eti kwanza naomba unisamehe Kwa hiki ambacho nataka nikuambie, Mimi nataka kuwa huru naomba tu unipe taraka , nikamwambia acha utani mke wangu, akasisitiza kuwa ana maanisha na hataki kuondoka na kitu chochote Wala kugawana, ilibidi niende chumbani kulala niliona kama utani.
Usiku mke wangu hakuja chumbani kulala, ikabidi nirudi sebuleni nikamkuta kalala kwenye sofa, nikamwuliza vipi mbona umelala hapa, akajibu anataka taraka awe huru.
Kesho yake alizidi kusisitiza ikabidi nimwite rafiki yangu na mke wake waje wamsikilize, akasema anahitaji kuwa huru hivyo apewe taraka tena akawa amekuwa mkali hasa, wiki yote nilikuwa siamini kama ana maanisha ila mwisho wa siku ndugu na marafiki wakanishauri nifanye hivyo anavyo taka.
Dada tayari ni mwezi na nusu umepita Toka niachane na mke wangu bila sababu yoyote, na ndo kwanza tulikuwa na mwaka Toka tuhamie kwenye nyumba yetu, naumia sana.
Na kinacho niuma zaidi, yule dada mpambaji aliniambia siku ambazo alihudhuria hazizidi 5, na wakati Kila siku alikuwa akiniaga anaenda, sikuwahi hata kumfikiria mke wangu kama anaweza kunifanyia huo unyama, tulikuwa hatuna shida yoyote.

