Nimeanza Kuamini Umri na Elimu, kuna Wakati ni Vitu vya Kuzingatia
Hello Kaka Spesho Nakufuatilia sana nimeona mtu ana tatizo Kama langu nami nikaona nisikae kimya
Binti Nina miaka 25 Nampenda Mungu Sana,Huyu mkaka nilikutana Nae mwaka 2022 alinipenda Sana Lakini Mimi kwa wakati huo sikuwa nawaza habari za Mahusiano Wala Nini…. Nikampotezea kabisaa tukawa marafiki Watumishi wa Mungu anampenda Mungu Sana na Mimi pia vivyo hivyo.
Katika kipindi chote hicho Sikuwahi kujua umri wake Elimu yake wala kazi yake ni mtu anaficha Sana vitu vyake Basi sikuona shida kabisaa… Aliendelea kunifuatilia Sana akitaka anioe me sikuwa tayari Kuna wakati tuliacha kuwasiliana kabisa kwa muda mrefu Mara nyingine ananitafuta mwenyewe tunawasiliana Tena…. To short the story
Mwaka huu tulikutana Tena Alikuja kanisani kwetu alikuwa anahudumu semina ya Pasaka akaomba kuonana na Mimi nikakubali akanambia tu Leo nakuuliza Mara ya Mwisho utakubali nikuoe au hauko tayari …. Kweli Mimi nilikuwa nampenda Sana Sana ingawa sikuwa tayari kuingia kwenye mahusiano ikabidi nimkubalie hiyo siku. Ndiyo siku nikajua umri wake Elimu yake n.k ananizidi mwaka mmoja tu…
Kaka tangu hiyo siku nimkubalie hatujawahi kukaa kwa Amani ikitokea tumekaa kwa Amani Basi ni siku mbili au tatu za wiki baada ya hapo tutavurugana hata zaidi ya wiki…. Hivi Sasa tuna wiki ya tatu hatuwasiliani kabisa tulitofautiana tu kwenye mazungumzo… Yeye hataki kuulizwa kitu chochote
Ikitokea nimemuuliza au amenambia kitu nimekataa anasema nimedharau kwa Sababu namzidi Elimu na Uchumi… Lakini kweli Mimi sijawahi tumia Elimu yangu au Uchumi wangu kuonyesha dharau yoyote kwake…. Ila yeye anasemaga kwa Sababu unanizidi Elimu kila kitu nikikwambia hunisikilizi hunitii
Tulipotofautiana zilipita siku tatu nikamwomba kuongea nae,Alikataa kabisa kabisa na akanambia niwe huru na Mambo yangu Ikiwezekana hata Niolewe tu
Niliumia Sana nikajua ni hasira tu… Baada ya siku mbili nikamtafuta Tena kwa kumtumia message akanambia niwe huru na Mambo yangu
Kaka najua sio Mara zote hili linakuwa hivi Kwa watu wengi…. lakini nimefika mahali nimeanza kuamini umri na Elimu Kuna wakati ni vitu vya kuzingatia Sana mtu anapofanya machaguzi ya kuoa au kuolewa. Awali nilikuwa siamini kabisa hivi vitu Ila nawaza tu huyu mkaka chochote kilichotokea lazima tu atasema kwa Sababu unanizidi Elimu Ndio maana hunisikilizi hunitii daah
Basi niishie hapa

