Nimeachwa na Wanaume Saba, kwa Sababu Sijui Kulia Kitandani
Habari yako dada yangu, Mimi ni binti umri wangu ni miaka 21 Kila nikiingia kwenye mahusiano naishia kuachwa japo Mimi ni mrembo sana.
Nimesha ingia kwenye mahusiano na wanaume sana na wote wananiacha bila sababu za msingi, Yani nikisha lala nao mara ya kwanza, mara ya pili basi wananipotezea, nilikuwa siwaulizi nini sababu mana Mimi sipendi kumuanza mwanaume kwenye mawasiliano au kwenye kuchat.
Mwanaume wa tano ilibidi nimwulize kwanini ananipotezea bila sababu, akasema hajanipotezea ila Yuko bize tu, niliendelea kumsumbua mwisho akaniambia eti Mimi sijui mapenzi uzuri wangu unanipa kiburi, nikamuuliza kwanini, akadai sijui kulia Wala mahaba, Toka hapo hakuwahi kunitafuta tena.
Sasa mwezi huu wa Saba niliingia kwenye mahusiano nikasema ngoja nibadilike, naye nikalala naye mara ya kwanza na mara ya pili akanipotezea, Kila nikipiga simu hapokei na sms hajibu, ikabidi niende mpaka ofisini kwake, bahati nzuri nilimkuta ilibidi nimbane aniambie kwanini ananipotezea, akawa hanipi majibu ikabidi nianze kulia akaanza kunibembeleza ninyamaze mwisho ndo akaniambia kuwa eti Mimi bado mdogo sijui mapenzi, nilimuuliza anamaanisha Nini? Akasema yeye hapendi mwanamke bubu kitandani ndiyo maana akaona tu tuachane.
Dada Toka siku hiyo mpaka Leo Mimi sielewi na naogopa tena kuingia kwenye mahusiano nitaendelea kutumika sana bila malengo yoyote,
Dada naomba unipostie,Yani Ili ulie inatakiwa iwe Nini? Au unaamua unalia tu?

