NILIKUWA DADA WA KAZI, SASA NI INJINIA
Nina imani uko salama kaka Spesho
Kuna story niliwahi kukupatia kuhusu kaka mmoja alikuwa anaitwa hamisi.. hamisi wa kibada kama unakumbuka vizuri
Sasa nimekuja leo kutoa ushuhuda namna MUNGU alivonifuta machozi kutoka kuwa dada wa kazi niliyedharauliwa na Hamisi wa kibada hadi kuwa Mke halali mwenye biashara inayoeleweka
Ushuhuda upo kama ifuatavyo:
Baada ya kuumizwa na yule Hamisi wa kibada niliamua kuachana na mapenzi kabisa yaani nikaanza kusali kwa nguvu zote yaani nikawa ninamuomba ruhusa bosi wangu kila jumamosi nikawa ninaenda kanisani,bosi wangu akaniruhusu maana mimi ni msabato yaani nimezaliwa kwenye usabato Baba yangu na Mama ni wasabato sasa baada ya kuanza kwenda kanisani kuna mahubiri yalitokea yanaitwa DAR NET EVENT 2025 NURU YA MATUMAINI wasabato wanayafahamu hayo mahubiri,
Sasa nilibatizwa kwenye yale mahubiri maana nilikuwaga sijabatizwa ingawa nilikuwa msabato tangu kuzaliwa, lakini baada ya kubatizwa tu maisha yangu yalibadilika sana yaani nilianza kusali sana kuliko kawaida nikawa nafunga na kumuomba MUNGU anisaidie nijitambue, nipambane,nisikate tamaa.
Sasa siku zikaenda nikawa naenda kanisani hivo hivo kila jumamosi boss wangu ananipa ruhusa naenda kusali, nikapata mchumba bhana ni mwanaume tu mtu mzima ananizidi umri aliniona hiyo siku tulikuwa tunafungua kambi la kibada akaniomba namba tukawa tunawasiliana siku zikaenda akanambia tuonane tuongee vizuri tukapanga siku tukaonana sehemu tu ya wazi nikaenda tukaonana tukapiga stori akanambia anataka kunioa sasa mimi nikawa siamini kama yupo serious maana engineer kabisa kuja kunioa mimi house girl?, halafu muda mfupi tu hata hatujafahamiana tabia vizuri anataka kunioa?
Ikanibidi nipige magoti nimwombe MUNGU nikamwambia MUNGU “kama huyu ni mwanaume sahihi kwangu naomba nipe ishara” baada ya kuomba nikawa ninasikilizia sasa nione kama kweli yupo serious, baada ya hapo tukapanga tena kuonana tukaonana tena tukaongea nikamuona kweli yupo serious sasa akaanza process za kunitolea posa zikakamilika akanitolea mahari tukafunga ndoa na baada ya kunioa amenifungulia biashara yaani hata siamini jamani kama nimepata hii bahati namshukuru sana MUNGU yaani nimependeza sana kama vile siyo mimi,biashara yangu inaendelea vizuri na ninampenda sana Mume wangu ndoa yetu ina amani yaani tupo lelelele kabisa sitakuja kumsaliti Mume wangu maana amenipenda wala hakujali status yangu.
Sasa ushauri wangu kwa wadada ni kwamba unapopitia changamoto inayokuumiza mshirikishe MUNGU omba kwa kumaanisha na unapoomba hakikisha unaacha mambo ya kipumbavu yaani omba kwa kumaanisha kabisa na utaona mambo yatabadilika katika maisha yako..
Mimi nimeona kabisa ukimwomba MUNGU kwa uaminifu anakujibu na anakuinua kama alivo niinua mimi kutoka kuwa housegirl hadi kuwa mke halali tena mwenye biashara inayoeleweka.. aisee MUNGU anajibu maombi jamani tunapokosea tujirekebishe turejee tuombe msamaha kwa MUNGU na tutabarikiwa na kusamehewa.

