NILIBADILI DINI, NIKAIMBA KWAYA ILI ANIOE, LAKINI AMENIKATAA
Habari kaka naomba unisaidie na mimi ili watu wanipe ushauri mimi ni binti wa 27 naishi na mtu na nimezaa nae mtoto mmoja ila tatizo langu ni kwamba huyu mwenzangu hataki ndoa, toka tumeanza kuishi hadi sasa huu ni mwaka wa 12. Nilipata mimba nikiwa mdogo sana hadi sasa bado tupo pamoja ila naomba watu wanishauri kwani sijui nifanye nini hadi sasa na sielewi kama huyu mtu ana nia na mimi kwani tunakaa vizuri ila mkiongea swala la ndoa basi ujue mtagombana
Nilipofikia hadi wazazi wangu hawana ushirikiano na mimi kama wamenisusa kwani toka mtoto akiwa na niezi mitatu walikuwa wanamuita ila yeye hakuwahi kukanyaga kwetu yaani sio kuwe na msiba wala tatizo lolote sio muendaji kwetu na mimi na yeye dini tofauti mimi muislamu yeye mkristo ila mimi nilijitolea kwenda kanisani jumuiya naimba kwaya yote hayo wazazi wangu wanajua na hawajawahi kuweka pingamizi ila yeye sijui tatizo nini kwake tumeitwa sana na viongozi wa kanisani tumeshauliwa sana juu ya maisha tunayoishi ila mtu bado moyo wake mgumu mchungaji anakuja hadi nyumbani kutushauri ila bado hana muelekeo
Yaani tukishauliwa anaitikia vizuri ila tukirudi nyumbani anaanza kuongea wewe unataka ndoa unajua ugumu wa ndoa wewe au unapenda kuiga maisha ya watu hayo ndo maisha ninayo ishi nakumbuka mwaka juzi kulitoka ofa za ndoa kanisani tukashauriwa akakubali mimi nikaongea na mama yangu akakubali siku zilienda mwezi ule wa kufunga ndoa ulifika nikamwambia mwezi umefika na wewe hakuna hata baba yangu anayekujua kwanini usiende nyumbani kuongea na baba zangu mimi baba yangu mzazi amefariki hao waliobaki ni wakina ba mkubwa na baba wadogo alichonijibu mimi sina mpango wa kufunga ndoa na wewe wewe kaa ukichoka ondoka
Nikamuuliza umesemaje akasema kaa ukichoka ondoka kwakeli niliumia na wazazi wangu sikuwaambia mimi nilitaka kuondoka sasa akaja shangazi yake akasema ukiondoka ndo umetatua tatizo na ukiondoka ukienda kwenu ukifika huko umeolewa sisi tuje kwenu kufanya nini wewe kaa sisi tutaenda kwenu na wazazi wake wakasema hivyo hivyo ila kila siku wamekuwa watu wa kunipanga na hakuna kinacho endelea ila kila siku mwanaume anasema ananipenda hao wazazi wake toka waseme wataenda kwetu imepita miaka miwili sasa bado wananiambia nivumilie sasa huu mwaka 12 toka nakaa na mtoto wao mwakani tunaanza mwaka wa 13
Naomba mnishauri niendelee kuvumilia au niondoke maana kwasasa hata moyo wangu haujui ufanye nini nimekuwa mtu wa mawazo sana

