Ni Mfumo Uko Hivyo, Au Mimi Ndio Sielewi?
Jamani wadau naombeni mnisaidie majibu yenu hapa kuhusu nitakachokieleza hapa huenda mimi ni sina elimu na haya mambo ya mtandao au sielewi!
Maana ukipata jambo ulilete kwa wadau harafu watakusaidia majibu wenye uelewa wao,! Katika maisha yangu nimeumizwa sana na kitu mapenzi kuna muda nilikuwa sitamani hata kuyasikia katika masikioni mwangu kutokana na nilivyoteseka na hili janga!
Mimi nina watoto wangu wawili alhamdullillah mwenyezi Mungu amenijaalia nashukuru, sasa habari iko hivi kuna mchumba nilimpata akasema anataka kunioa wala hana mpango wa kunichezea kabisa maana alipo toka huko hata yeye ameumizwa vibaya mno kwa hiyo aliponiona mimi akaona kama nitamfaaa jinsi nilivyo na tabia yangu, yeye yupo dar ila mimi nimesafiri pia naishi dar, kwa hiyo tumewasiliana kama miezi 6 hivi tupo tunawasiliana na tunaongea vizuri!
Kuna siku akaniambia kuwa baba yake amemuagiza kwenda chalinze kusimamia mafundi kujenga ila akaniambia sehemu hiyo mtandao shida sana ni ndani kidogo kwa hiyo mtandao unasumbua ila nikija huku barabarani tutakuwa tunawasiliana ni kasema sawa,! Mimi sehemu niliyopo siwezi kumpigia simu kwa kawaida lazima ni mpigie whatsap au imo ndo tunaongea,!,
Sasa siku hizo zote namuona yupo online yaani kila muda nikimpigia anasema niko barabarani huku tupo na baba tumekuja kununua vifaaa, nikamuagiza mtu ajaribu kumpigia kawaida mida ya usiku simu inaita maana yeye ni dereva bajaji nilituma yule mtu muulize yuko wapi akamjibu nipo tegeta maana yeye ndo anapokaaga na bajaji anaendesha huko huko alipomuuliza hivyo akakata simu nasi yule mtu akaniambia nimempigia kapokea kasema yupo tegeta ni kasema sawa, nikajua kuwa amenidanganya!
Pia nikamuuliza unarudi lini huko chalinze akasema bado kazi haijaisha! Nikasema sawa ila nikaamuambia kuwa wewe unanidanganya haupo chalinze nimeshajua, basi akaniambia ni kweli kama umetuma mtu anipigie mimi huwa siongei ukweli kwani sisi huwa tunatekwa kwa hiyo naongea ili ajue niko wapi, pia namba ngeni siijui siwezi sema ukweli kuwa niko wapi, basi tukawa tumegombana, ila kesho yake asubuhi akaniambia nimesharudi hapo kumbuka jana yake kuniambia kusema sijui atarudi lini maana kazi bado, basi. Nikajua ni uongo tu huu nadanganywa nikawa nimepotezea!
Majuzi Kati kutwa nzima hapatikaniki katika simu kesho yake akaja kuniambia simu imezima na fundi kasema haiwaki tena maana iliingia maji nikasema mbona umenitafuta naona hapa alichonijibu akasema eti kachukua laini kaweka kwenye simu ya rafiki yake ndo akanitafuta mimi nikasema ungeweka laini kwenye simu ya rafiki yako ingekuja namba ya rafiki yako isingekuja yako!!
Sasa mimi nauliza kuichukua laini yako kuweka kwenye simu ya mtu kila kitu kinasoma chako?! Yaani Facebook, whatsaap, imo kweli jamani mfumo uko hivyo au mimi ndo sielewi??!! Mnisaidie majibu hapo mimi nikamkazania kuwa hicho kitu si cha kweli unanidanganya kabisa haiko hivyo basi akawa ametuma sms kuwa anaona simuamini kama vipi nimuache na maisha yake ya uongo na mimi niendelee na maisha yangu tuu?

