Najaribu Kuamini kwamba, Mwanaume Haridhiki na Mwanamke Mmoja
Habari kaka samahani me niko na tatizo kwenye mahusiano nahitaji unishauri.
Mimi ni binti age 24, 2019 kuna kaka nilianza nae mahusiano Alikuwa ananipenda Sana lakini kwa upande wangu nilikuwa simpendi.
Tuliendelea na hayo mahusiano hivyo hivyo mpaka 2021 mie nikabeba mimba ya mwanaume mwingine na yeye alipata taarifa kutoka kwa rafiki zangu.
Lakini kipindi hiki hatukuwa karibu kila mtu ana mambo yake lakini huyu kaka hajawahi kuniambia tuachane wala hataki kusikia ilo neno kutoka kwangu.
2022 nilijifungua moshi nikarudi dar na akajua kama nimerudi akaja kumuona mtoto na alimpenda Sana mwanangu na nilikuwa nikiwa nashida ya mtoto kuhusu chochote ananisaidia.
Tuliendelea hivyo pasina na mahusiano yasio eleweka mpaka 2024 tukaanza kuwa serious na mahusiano, kumbuka huko kote tupo kama hatupo japo mie nikimwambia tuachane yeye hataki kabisa anasema mie ndo mwanamke anaenipenda.
Lakini tulivyoanza kuwa serious kuna siku niliota ananichet zaidi ya mara 3 nikasema hii sio kawaida kwahiyo nikachukua simu yake wakati kaenda kuoga nikachunguza na kweli nikakuta sms za mwanamke.
Huyo mwanamke anamwambia huyu mwanaume amtolee barua, kaka sijawahi kumuona akiwa na rafiki wa kike wala kumsikia akiongea na mwanamke yeyote zaidi ya ndugu zake nakumbuka nililia Sana yaani hata alivyorudi kuoga nilishindwa kuongea nae nikaondoka kwake usiku huo huo.
Alinitafuta Sana, aliniomba msamahaa sana lakini sikumsamehe kama week hivi nikamsamehe sasa 2025/9 nilianza kuishi nae na yeye amenipita miaka 8 na sasa hivi ni mjamzito wa miezi 2.
Lakini kinachonichanganya mara nyingi nakuta sms za wanawake japo ni kwa siri sana yaani kwenye recycle bin ndo nazikuta au messenger
Nikimuuliza hana cha kujitetea zaidi ya kuomba msamaha, mie kwa upande wangu nachanganyikiwa nashindwa kumuelewa je anataka nizae ili baadae anitese na hii mimba ama laah japo anaonyesha kujali Sanaa nipo njia panda nashindwa kuelewa nikae upande gani naomba nishauri please.
Najaribu kuukubali msemo wa mwanaume haridhiki na mwanamke mmoja lakini bado nashindwa kuamini, Ama nitoe hii mimba nawaza sana inaniumiza kwakweli now nipo kimya siongei nae anajifanya anajali na mie sitaki kuongea nae maana naona kama ananijok tu.

