NAHISI WASIOOLEWA WANAFAIDI ZAIDI KWA KUWA MICHEPUKO
Habari kaka …mimi ni mama wa watoto wawili ila baba tofauti …mtoto wa kwanza familia ilimkataa huyo Mwanaume …mtoto wa pili nimezaa na mwanaume ambaye alikwenda kwetu na kutoa mahari …tumepishana miaka 9 …mimi nina 30 mtoto wetu ana miezi sita
Sasa mwanaume alibadilika Sana na hata tarehe aliyopanga kurudi kumaliza mahari na kusema tarehe ya ndoa ilifika na hakwenda wala kutoa tamko lolote.
Juzi kati nikampigia simu usiku maana alikuwa anaweza hata kukaa siku tatu au nne hajatutafuti… Nilivyo mpigia akaanza kuongea akijua mimi ni mchepuko wake …nilimuuliza sana maswali na yote alikuwa akijibu …wakati huo namrcod … niliumia mno ..
Ila inaonekana alikuwa kama kalewa na yupo kwenye usingizi mzito
Asubuhi nikamtumia ile voice ndo kushtuka kama alikuwa anaongea na mimi
Aliomba msamaha Sana ndani ya wiki moja nikawa sipokei wala kumjibu txt zake …
Nikaona acha nimsamehe ila nikataka kujua ana malengo gani na mimi maana hadi huyo msichana mwingine kamwambia atamuoa na swala la muda tu …akasema anarudi kwetu mwezi ujao kukamilisha na alidai sisi ndo familia yake …
Kaka nilitamani kuzaa na huyu mwanaume hata watoto watatu ila huyu mmoja tu kaninyoosha sina hamu na wala sijui tena kama nitajaribu …anapenda starehe Sana …
Kuna muda natamani hata nimwambie aache kumaliza hiyo mahari ili na mimi niendelee na maisha mengine maana nawaza nikiingia kwenye ndoa ndo nitakoma kabisa ….
Nilikuwa natamani Sana ndoa ila kwasasa sina hamu kwa matendo yake …halafu ninacho waza zaidi tayari nina watoto wawili baba zao tofauti …hivi kweli niwe na baba watatu …naumia Sana jamani
Kuna muda nahisi wasio olewa wanafaidi zaidi ambao wana michepuko wa waume za watu maana siku hizi wanaume wameonekana kuwajali zaidi michepuko kuliko wake zao …naumia Sana
Nishauri kaka niolewe au nimuache tu aendelee n maisha yake

