Mume Wangu Hana Nguvu Za Kiume, Ila Huyu Mpenzi Wangu, Ambaye Ni Mume Wa Mtu, Anazo Nguvu
Asante, Mimi changamoto yangu Nipo kwemye ndoa Nina miaka 7 kwenye ndoa nimepata watoto watatu ila Wawili wametangulia mbele za haki
Changamoto ilianza Baada ya kumzaa mtoto wa 3. Mume akanibadilikia akawa na mahusiano Nje ya ndoa nilipogundua akawa mkali sana changamoto kubwa ikaanza Mara tuu Baada ya mwanangu wa pili kuumwa na kufariki akasema Mimi na mamangu ni wachawi, tumemuua mwanae
Sasa tunataka kumuua na yeye, akasema nisipate shida nikitaka kumuua nimuwekee tu sumu kwenye chakula yeye akila atakufa, pia akaniambia Nipo kwaajili ya mtoto nisingekua na mtoto anganirudisha nyumbani kwetu, nikaamua kuishi kwaajiri ya mwanangu lakini nikajiapiza nikikutana na mwanaume ambae yupo serious nitaingia nae kwenye mshusiano
Basi Baada ya miezi mitano nikapata mwanaume nae NI mume wa mtu ila ananijari sana ,Sasa tupo kwenye mahusiano changamoto iliyonifanya niingie mahusiano mapya mume wangu hana nguvu ZA kiume ila huyu mpenzi wangu ambaye ni mume wa mtu Ana nguvu
Bado nampenda SanA mume wangu ila amegundua kwamba Nina mahusiano mengine Nje ya ndoa na yule MME wa mtu Ana mke na watoto naomba ushauri kama nikiendelea na mume wangu sitapata utamu maana hana nguvu,na nikibaki kwa mume wa mtu nahisi naiba penzi la mwanamke mwenzangu, nachanganyikiwa kabisa…
Nisaidieni jamani

