MUME WANGU AMENIAMBUKIZA UKIMWI MAKUSUDI
Mimi ni mama wa watoto wanne mtoto wangu wa kwanza nilizaa nilipomaliza form 4, baadae maisha yalikuwa sio magumu sana lakini niliona nimekosea na kuiaibisha familia yangu ndipo niliona Bora niolewe. Nilikuja kuolewa na mwanaume mwingine ambaye siye baba wa mtoto Wangu wa kwanza Kwa sababu nilikuja kugundua mwanaume niliyezaa naye ni mume wa mtu kwa hivyo sikuona vema kuendelea kuharibu ndoa hiyo. Sikutaka kuwa sehemu ya machozi ya huyo mama na nilijua one day anaweza kuwa mama wa mtoto wangu na ndivyo ilivyo hadi sasa maana baba wa mtoto baadae alimchukua mtoto na anamsomesha huko alipo.
Hivyo baada ya kuolewa nilibeba ujauzito wa mtoto wangu wa 2 Kwa huyu mume wangu ilikuwa sogea tuishi yeye ni mwalimu, niliamua kukaa Kwa kutuliaa Kwa sababu niliamini sio busara kuendelea na tabia za ujana kwa hivyo nilikaa Kwa adabu nisiharibu Tena nimekuwa mwaminifu Kwa huyu mume wangu
Nina muita hivyo Kwa sababu baada ya kujifungua mtoto wa 2 tulifunga ndoa ya serikali
Nifupishe kidogo….
Mume wangu huyu ana tabia ya wanawake sana na anavuta sigara zote anakunywa pombe na ni mkibosho nimezaa nae watoto watatu alishatembea na marafiki zangu woote kifupi moyo wangu umekufa Ganzi sina hisia nae Kwa maana hanihudimi Kuna wakati hata chakula ndani unakuwa ni shida watoto nina pambana nao mimi nilikuwa nashtaki Kwa wakwe but nikaja kuona haisaidii maana kibao kinanigeukia mimi kwahivyo nikanyamaza
Tukahama tukahamia mkoa mwingine tulivyofika huku nikamshauri tufungue duka la Mangi ili nisikae nyumbani tulifanikiwa kufungua lakini duka limeisha maana akitoka kazini atakaa huko anafunga saa 6 Usiku akitoka atapitia grocery atakunywa ahonge katembea na Wateja hadi sasa Wateja hamna mauzo yameshuka sana
Amenifanyia mengi hadi naona simpendi Tena yaani sijui namuona kama nini tuu
Hata ndugu zangu wakija kwangu ananuna hataki nikiongea kwanini unanuna wageni ni Baraka na mbona ndugu zake wanakuja nnia wahudumia vizuri wakitoka kurudi ma kwao wanasifia tuu kwamba fulani kapata mke
Kuna kipindi nilipoona duka limeisha nikamwambia nichukue mkopo niweke dukani alikubali na akasema atalipa kupitia mshahara wake baada TU ya kuweka mzigo dukani alikataa kulipa akasema nitalipa mwenyewe
Hali imekuwa mbaya maana aliacha kununua chakula nyumbani tukawa tunakula dukani nimeshindwa marejesho na duka limeisha hata hajali nimechoka sana nikiwaza kuanza upya naona ni ngumu nishauri nifanye nini maana naona nimefikaa mwisho simpendi na sina hisia nae kabisa nikiwaza hawa watoto siwezi kuwaacha kwakweli Kwa tabia zake maana hata binti wa kazi wananikimbia kisa anawataka
Kuna kauli alishawahi nitamkia kwamba hata akiniacha Nani atanitaka nishazaa watoto wa 4 Tena alinitukana mbele ya dada zake. Pia alishawahi niambia hata akifa nijue sitoambulia kitu kwake nitafute vyangu
Alishaniambukza ukimwi, nilishakata tamaa na hii ndoa ukiongea na wachungaji wanakwambia vumilia nyumbani unaambiwa vumilia
Sio kwamba sijui kutafuta pesa najua na ninaweza yeye mwenyewe ana apliciate hilo hata 70% ya Vyombo vya ndani nimenunua mimi Kwa hela yangu maana mimi ni fundi nashona nguo za kike na kiume
Naomba nipostie nipate ushauri Kwa follower’s wako nitapitia comment

