Mume Wangu Alinifumania Tukaachana, Sasa Hivi Anatembea Na Mwanangu
Mwezi wa tatu mwaka huu mume wangu alinifumania na kaka hivi ambaye alikuwa ni fundi wa kuchomelea mageti karibu na lilipo duka letu la kuuza spea, dada niwe mkweli kosa lilikuwa Langu mpaka Leo najutia sana, na nilisha omba sana msamaha ikashindikana, nimetuma sana watu kuniombea msamaha lakini Bado haelewi.
Sasa Baada ya Mimi kutoka Kwa mume wangu, mtoto wangu wa kike ambaye nilimzaa kabla ya kuoana na mume wangu yeye alikataa kuondoka akasema anabaki pale pale, nilifanya juu chini Ili niweze kumtoa pale lakini aligoma kabisa, yeye alisema hawezi kutoka pale wakati yeye ndo kamsomesha secondary yote shule ya hela.
Ilibidi nimuache pale Mimi nikaondoka, Sasa nimeanza kusikia tetesi kuwa mume wangu anatembea na binti yangu japo Sina uhakika, ila naambiwa mara nyingi wanatoka usiku kwenye gari wanaenda kwenye starehe, na pia Kuna muda Wana safiri wote, ila Kila nikimpigia simu mwanangu kumuuliza hicho kitu anakataa na kudai siyo kweli.
Dada, Mimi na mume wangu tulizaa watoto wawili, na wote walibaki kwake pamoja na huyo binti yangu ina maana jumla wapo watatu, pale Wanaishi na mdada wa kazi sema Sina mazoea naye ningemuuliza.
Kwa Sasa Nina mawazo sana natamani hiki ninacho kifikiria kisiwe kweli kitanitesa sana kwenye maisha yangu yote, naumia mno dada yangu natamani muda urudi nyuma.

