MCHUNGAJI ALIMWAMBIA ASIOLEWE NA HUYO JAMAA, MAANA ATAKUFA, NA AKAFA KWELI
Habari yako kaka Spesho mimi ni binti wa miaka 25. Nina changamoto moja naomba nisaidie mawazo yako. Dada yangu yaani binamu yangu aliolewa 2023 akafariki 2024 mwezi wa 9. Sasa kwa situation ilivyokuwa mpaka wao kuoana kuna mchungaji alimuambia asiolewe na huyo jamaa unless awe imara sana kiroho maana atakufa na magonjwa mazito na ni kweli aliugua kisukari na presha.
Sasa shida ni hii, mimi shemeji nilikuwa namfahamu kwa miaka 5 kabla ya wao kuoana lakini sikuwahi kuongea nae wala kutaka kujuana nae kabisa sikuwahi!! Ila msibani tukaongea na tukabadilishana namba. Sasa mimi na yeye tunawasiliana kila siku na akiwa na shida ananiambia na mimi nikiwa na shida namuambia. Ishu imekuja ananiambia anataka kunioa, nimemkatalia sababu hisia hizo sina ila nimegundua anayemshauri anioe ni shangazi yangu (mama wa dada yangu aliyefariki) nimekaa nikawaza nikahisi huenda shangazi anataka na mimi nife sijui?
Kwasababu mchungaji aliwaambiaga shida ipo kwa wazazi wa kiumeni wala mwanaume hana shida na hajui kama kwao ndo kuna shida. Mind you mimi ndo binti wa pekee kwetu. Hivi nimewaza nimehisi shangazi ana niwazia mabaya. Au ni mimi nakosea kuwaza?? Naomba unishauri nataka kumkataa kwa namna itayobaki na heshima kati yetu
Lingine kubwa, ni mimi natamani kuwa na familia, niwe na mume wangu na familia. Ila nimepitia maumivu kwenye mahusiano nimejikuta naogopa sana kuwa kwenye mahusiano na muda mwingi niko single.
Nikijipima naona natamani kuwa mke na mama kwa mume mmoja na niwe na familia ila naogopa sana habari za mahusiano. Nishauri nifanyaje? Natamani hata mwakani majira kama haya niwe na kwangu. Is it desperation? Ama nakosea kuwaza hivi?
Kama niko desperate nisaidie nifanyaje kudeal na hii hali nisije kukosea kuolewa nikajutia milele. Asante kwa kunisikiliza

