Mchumba Wangu Mlokole, Kila Ninachokifanya Anakijua, Hata Akiwa Mbali
Na Mimi naona niombe ushauri,
nipo kwenye mahusiano na mdada mmoja ambaye ni mkristo na ni mtu wa dini sana Yani wale walokole hasa Japo Mimi sio mkristo.
Cha ajabu ni kuwa huyu dada anaweza kunambia vitu Ninavyofanya licha ya kuwa tunaishi mitaa tofauti.Sasa naombeni ushauri je mtu anawezaje kujua Mambo anayofanya mtu mwingine licha ya kuwa wako sehemu tofauti?
Yani anaweza kukuambia kuwa umekula chakula Gani na akapatia kabisa muda huo huo na wakati Yuko mbali kabisa huko.
Na hiyo haitoshi ukiwa kazini anaweza akakuambia ulisalimiana na watu wangapi na ulipitia wapi wakati wa kutoka kazini au wakati wa kwenda, na ukiangalia kweli ni hivyo, Sasa nashindwa kumuelewa huyu mdada mpaka ananiogopesha.

