Kwa Hapa Nilipofikia, Njia Pekee Ninayoona, Ni Kumroga Tu
Habari kaka pole na majukumu…. samahani naomba unipositie Kwa followers wako Angalau wanishauri maana maumivu ni makali sana ….Mimi ni Binti wa miaka 24 nimemaliza chuo mwaka huu…. nilikuwa na mpenzi Wangu ambae nimeanza nae mahusiano mwaka 2020 nikiwa naenda kuanza form five japo ilikuwa ni ngumu kidogo kumuaminisha kama sitobadilika Kwa ajili yake maana yeye kaishia la saba na watu wengi ikiwemo ndugu zake walikuwa wanamwambia hatutoweza kuoana kwa sababu Mimi nimesoma na yeye hajasoma kwahiyo IPO siku nitamuacha nifate wasomi wenzangu…..
Nilitumia nguvu nyingi sana kumuaminisha maana nilikuwa inmependa kweli mwisho wa siku akaniamini tukaanza mahusiano yenye amani bila kukosana Kwa sababu muda mwingi Mimi nilikuwa shule…. kiukweli alikuwa ananihudumia kadri ya uwezo wake japo hakuwa na uwezo mkubwa lakini alijitahidi hata nilipokuwa shule nikipiga simu nahitaji Hela atafanya namna anitumie
Baada ya Mimi kuchaguliwa kwenda chuo niliamua kuwahusisha wazazi wangu kuwa nimepata mwenza na nilifanya hivi Ili yeye aendelee kuniamini zaidi maana alianza kuonekana kuwa na wasiwasi…kweli wazazi wangu walinikubalia na wakanisihi nisije kumuacha kijana wa watu kama kweli nina malengo nae….kiufupi baada ya kwenda chuo tulikuwa tunakosana sana akipiga simu nikashindwa kupokea Kwa wakati anakasirika hata kama nikiwa darasani anataka nipokee Ili ahakikishe, muda mwingine nilifanya hivyo nilipokea simu na kuiacha on Ili asikie sauti ya mwalimu lengo ni kulinda mahusiano yangu
Lakini kumbe muda wote huo Mimi najilinda Kwa ajili yake yeye tayari ana mahusiano na watu wengine huku mtaani Yaani ni zaidi ya mtu mmoja
Nilivyogundua vile niliumia sana sana Yaani Mimi muda wote najitahidi kuwa mwema kwake lakini kumbe mwenzangu ana mahusiano pembeni
Kiukweli nililia sana na hata nilipokuwa nikijaribu kuongea nae anasema hakuna mwanaume mwanimifu hata nikimuacha yeye nikaenda Kwa mwingine Bado wote ni walewale, nilisamehe tukaendelea na maisha
Muda mwingi kwenye mahusiano yetu tangu nigundue sio mwaminifu kwangu tulikuwa tunakosana sana na ndipo ataamka na hoja ya kuwa ninataka nioe nimechoka kukaa mwenyewe
Ilifikia hatua Mimi nikachoka na Hilo neno nikawa namjibu wewe oa maana Kuna kipindi nilipita kwake baada ya kumaliza chuo nikaja kugundua Kuna mama mtu mzma anamzidi kama miaka sita amemzalisha nililia sana tena sana, nilisamehe pia nikijipa moyo atabadirika
Sasa baada ya Mimi kumaliza chuo aliniomba aje nyumbani atoe kishika uchumba Kisha tukaishi wote, Mimi Hilo kwangu halikuwa na shida ila shida ilikuja pale nilipojaribu kuongea na wazazi wangu walidai atoe na mahari ndo anichukue
Lakini nilivyokuwa nikiangalia hali yake ya uchumi ni kweli asingeweza kutoa hivyo vitu Kwa wakati mmoja na kunichukua nilikuwa naumia ila Sina namna, aliniomba nitoke nyumbani Kisha taarifa watapa Kwa baadae lakini niliogopa ndipo nilipoamua kumuambia Mimi naomba nitafute kazi kwanza angalau tuwe tunapata chochote
kiufupi tujipange kwanza na kweli alinikubalia maana Kuna kazi nilikuwa nimepata hivyo nikaona hii ndo chance ya kutengeneza maisha yetu
Kumbe mwenzangu ndo alikuwa ameshafika mwisho wa uvumilivu ndipo alipoamua kwenda kuchumbia na kuoa Tena kanisani mpaka Sasa ana kama week mbili akasahau tulipotoka na hata ndugu zake walivyojaribu kumuuliza amekuwa akisema Nina majibu mabaya nimejibu oa na kiukweli tulipokuwa tunakosana tulikuwa tunajibishana vibaya muda mwingine tunaamua kukaliana kimya hata week nzima Ili kuepusha kujibizana
Kiukweli naumia sana mpaka nataman nishike dawa nisambalatishe ndoa Yao maana nikifikiria tulipotoka ndo nazidi kulia zaidi nakumbuka niliwahi kupokea boom nikiwa mwaka wa pili nikatoa 360k Ili aanzishe biashara yoyote sikuishia hapo nikamkopea mkopo kausha damu za kina mama ( brac) Kuna muda anashindwa kurejesha inabidi Mimi na mama yangu turejeshe maana jina lilokuwa linasoma ni langu la mdhamini la mama bado akakodi shamba nikatoa Hela ya kupalilia Mimi.
Lakini Leo hii kaenda kuoa mtu mwingine nakuniacha na ujauzito kisa nilimjibu OA Tena tukiwa kwenye ugomvi jamani naombeni ushauri wenu nifanye Nini maana Mimi natamani nimshikie dawa

