JOIN US WHATSAPP
CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM
CLICK HERE
Jirani Yangu ana Tabia ya Kuniachia Mtoto wake, Yeye anaenda Kudanga
Naomba nipostie kwa fans wako wanisaidie kimawazo. Kuna mpangaji mwenzangu anatabia ya kuniachia mtoto wake nilale nae, yani yeye anaenda kudanga usiku ananiachia Mimi mtoto, nalala nae mpaka asubui akija ananilaghai na vi elfu 20 20 vyake.
Kiukweli Mimi hii tabia sipendi kabisa. Mana isije siku likamkuta mtoto tatizo nikaingia matatizoni. Naombeni njia nzuri ya kumkatalia anisipe mtoto wake nilale nae mana nimesha mzoesha hii tabia, ningejua siku Ile Ile ya kwanza ningekataa.
lakini ndo ivyo baada ya kuona vihela tena nikaingia kwenye mfumo.

