JAMANI BOSS USIWEKE
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 11
Tulianzia duka la simu, nikanunuliwa simu moja kariiii awee nilifurahi mno, bibi nae akanunukiwa, nzuli tu kubwa, nikapelekwa hotel moja nzuli tukala, tukapiga picha ilitoka vizuli P katabasamu aisee nilifurahi nikamsifia akaomba tupige nyingine yani hii mwamba ndio akaua kabisa yani, alinitizama uku anatabasamu kama ananitaka ivi yani tafrani tu…
Ilitoka vizuli mno pale pale nikaweka profile, na p nikachukua simu yake nikaweka niliona mwamba kama hataki anajikaza kuonesha kafurahi, muda huo nikaweka adi stutus na line niliyokuwa na tumia ni ya P, ile iliyokuwa kwenye kibatan, alichonipatia, tulienda mpaka nyumba kubwa ya P, muda huo simu yake ilianza kuita na yangu no za nje ya nchi, aliniomba simu akaizima nikashangaa huyu vipi tena, ila sikuwa na mashaka kabisa..
Nikaendelea na safari yetu, tumefika tukapokelewa vizuli bibi akapiga vigeregere sasa nimekuwa uyo ni bibi yake p nikawa nashangaa tu, akasema ile bangiri ya ukoo haikubali mtu yeyote alieliwa na mtu tofauti na damu yao, yani ni labda uwe bikra ama uwe ushaliwa na uyo mmeo wa ukoo huo tu tofauti na hapo haipiti, ndo nikasanuka duh, bibj aliaga akaludi kwake siku io io jioni nililia lakini haikusaidia nishakuwa mke wa mtu, nilimuomba akachukue mhitaji mmoja pale kituo cha kulelea watoto akae nae, tulikubaliana na kufanya maamuzi tutafanya hivyi kwa sababu tayali kuna mtoto pale toka mwanzo nilitaka kumchukua tuishi nae ni wa kiume…
Bibi alipelewa na Amir adi nyumbani, usiku Amir na P nikawa siwaelewi wakawa hawatulii kabisa, mala wako huku mala kule nikajiuliza hawa wanashida gani🤔, nikaamua kulala mpaka napitiwa usingizi P hajaja chumbani, kumekucha tu ivi leo nikawa wakwanza kuamka, nilimuacha p kalala ata sijui kaja saa ngap, nilisaidia na dada wa kazi, japo alikataa ila nilimuondoa hofu asijali…
Tulipiga kazi,nikaandaa chakula cha bibi na maji ya kuoga, nikaenda kumuamsha, nikamuogesha, nikampaka mafuta, nikampa na chakula ale uku namfanyia masaji, ya miguu, bibi alifurahi mno,P ameamka kakuta nishamuandalia nguo za kazini, taulo viatu, kila kitu na chakula, alioga akaanza kunitafuta…
Alinitafuta mno, dada wa kazi ndo akamwambia nimekuja kumuogesha bibi ni muda, huenda nimeshamaliza nilibeba na chakula kabisa, akaja akapiga hodi tukamruhusu, ajakuta tuko bize na story, na masaj, alifurahi adi machozi, alimsalimia bibi yake, alivyomaliza nilimuomba ruhusa kazini nianze kesho, aliniambia wote tuko off wiki hii yote, kuna kitu tu anaenda kufanya mala moja afu ataludi…
Nilimuomba simu akajifanya anahalaka akatoka nikamfata, alinipa ila akasema nisipokee simu tofauti za nje ya nchi,nilikubali nilivyowasha tu simu, ikaita ila nikaludi kwanza kwa bibi kum masaj,simu ikawa simu,sikupokea nilihisi niya kazi, imefika mchana, no tofauti tifauti, nilivyowasha data…
Nikakuta no nyingi tu za nje uko zimetuma sms, sikufungua nikawa na yangu tu, jioni P aliludi akasema alibanana sana, nimsamee kwa kuchelewa ata sikuwa na ubishi mtoto wa watu, usiku wakati tunakula niko chumbani mimi na P na bibi tunakula nae, tukasikia vulugu,kelele P na bibi wakatizamana,kisha bibi akamwambia P nenda muache mke mwenzangu apa ukapokee hao wageni hakikisha unaludi, nilimwambia Bibi ni wageni twende wote afu tutaludi wote, kabla ata hatujamaliza kuongea mtu mbili zikaingia zinahasila🙄….
EP 12
Mmoja alikuwa mtu mzima na mwingine alikuwa binti tu wa kawaida, ila wote wazungu, yule mama alifanana na P ila binti alikuwa tofauti mbali tu, waliingia bila hodi mama P alikuwa anajua kishwahili vizuli tu, ila yule dada hakuwa anajua, walifika na kuuliza mimi nani? P akajibu mimi ni mkewe amenioa ndoa halali kabisa, mama ake akamuwasha kofi, mimi hapo natetemeka bibi akanishika mkono nakuniambia nisiogope hapa ni kwangu, afu akaongea na mkamwana wake kwa kishwahili…
Alimuita mama Phillip, kuwa na mipaka, kijana anahaki yakuoa wake ata kumi akitaka, mimi hapo ata sielewi, na kingine uyu binti unayemkatalia mwanao ameshamshindwa kama utaendelea kulazimisha, utaondoka nae wewe,mama p akacheka kwa dharau akanitizama nakusema, mwenye mamlaka yakuniondoka kwangu sio wewe mzee ni mme wangu tu, na hawezi, ghafra. Nyuma yake akatokea mzee uyu ni chotara mwafrica mzungu…
Akajibu basi mimi ndie nitakufukuza, yule mama alishtuka akaanza kujiliza kwa mme wake, P akanitambulisha kwa Baba ake, nikamsalimia, akafurahi mno kuniona na vitu vya ukoo wao, akasema pale pale, huyu ndie mkamwana wa familia na ukoo, siomi, atabaki kuwa mke mkubwa lakini mamlaka yatakuwa kwa mke mdogo kwa sababu katimiza matakwa ya ukoo, na hata wewe mama P huna mamlaka kwake hukuwahi kupata hata kimoja kati ya hivi, mwenye anaweza kumkosea ama kumpinga mkamwana mdogo ni mama angu tu, ninyi wengine kuanzia dk hii hamna hio nafasi…
Nilichoka ivi kumbe mimi nimeolewa uke wenza jamani, nilijikuta tu nalia, P aliniona nakia kwa sili alinisogelea nilijikaza tu mbele za watu, ila sikuwa nataka ata aniguse, mama P aligoma akasema kuna mchezo tumwcheza alivyoleta mdomo sana mme wake akamwambia akiongea tena talaka inamhusu, na yule binti akaambiwa kama uke wenza hautaki, analuhusiwa kusai kalatasi za talaka kwa sababu tayali P alishasaini ni yeye tu hataki…
Mama p na mke wa P wakawa wameondoka kwa hasila, walipewa vyumba vya kulala ila mama P akamleta yuke mke wa P chumbani kwangu, mimi na P na baba ake, tulibaki chumbani kwa bibi, mzee akanipa utalatibu wa nyumba nzima nikakabidhiwa na funguo za nyumba korea,na ratiba za uko korea kama mkamwana halali…
Kisha P akaambiwa aandae ratiba ya zamu kwa mimi na P, asionyeshe ubaguzi, uyo kaja kuishi uku lasmi, familia yake imenijulisha, alisema hivyo Baba P, mimi apo sina nguvu mikono yote inatetemeka, kifua kimejaa, natamani nipewe nafasi nilie uchungu uniishe…
Mzee aliomba tukapumzike yeye anamaongezi na mama ake,tulitoka P ananiwahi niko mbio mbio, nafika chumbani nilie, nakuta mtu yuko tupu chumbani kwangu, nikataka kutoka P kafika, alikasilika, uzuli nilikuwa sijaleta nguo yoyote uku bado vitu vilikuwa kule, P alinishika mkono akaniambia, ” mke wangu naomba univumilie kidogo nichukue vitu tumpishe tu kwa amani, siwezi kutumia tena hiki chumba milele nikiwa na wewe, ni kama kukuchafua..
Sikujibu kitu alinishika mkono akachukua vitu vyetu vya muhimu, yule binti akaanza kuongea kikorea ata sikuwa naelewa zaidi ya kusikia tu,nikashangaa kawekwa kofi na P, afu P akapiga simu Amir aje amsaidie kuchukua nguo zake, mimi nilitoka kwanza nje make aliniachia mkono ndo akampigakofi, yule binti alianzisha vagi uku kajifunika shuka, mpaka mzee na wengine wakaja…
Sijui nini waliongea, niliona tu p kaacha nguo zote kabeba tu za kwangu, tukaondoka na Amir, mud huo mimi nambembelezwa tu nitulie, ila ata kuongea siwezi….
EP 13
Tulifika mimi uso umejaa machozi, alinibeba nikawa nampiga sitaki kubebwa, alivumilia nimpige lakini anibebe tu,alifika mpaka chumbani kanibeba, aliniweka kitandani akaja kwa juu yangu nayeye ili kunizibiti nisimtoloke,alikuwa pia analia, ” Le wangu nilmsikilize tafadhali najua umeumia sikukujulisha mapema, naomba unisamed kwa hili, usinifikilie vibaya, nakupenda mno Le, yule mwanamke, nilimuoa ndoa pia ya serikali, lakini sio kwa matakwa yangu, alinilewesha akasingizia nimemtoa bikra..
Nikalazimishwa kumuoa, sikuwa na namna nilihisi huenda kweli kwa sababu ni kweli nilitembea nae ila nachokumbuka hakuwa mpya kama alivyodai, nilipiga sana, lakini badae ikaonekana na mimba pia kabeba, tylifanya DNA, majibu yakatoka ni kweli ni mwanagu, sikuwa na ujanja nikamuleta kwa bibi, ili akabidhiwe vitu vya muhimu lakini viligoma, ikajulikana kadanganya hakuwa mpya, bibj akagoma kumpa chochote kitu kama baraka, wakawa maadui sana, Baba akasema tayali anadamu yetu atuwezi kumkataa, niendelee tu na maisha, hata yeye mama angu alimuoa akiwa hana vigezo, nisijali imeshatokea…
“Ikabidi tu maisha yaendelee, lakini siku moja akiwa na mimba nilimfumania anamtukana bibi na anataka viti kwa nguvu, walikuwa wanashilikiana na mama, nilichukia sana, akaomba msama yakaisha, ila bibi yangu walizidi kumnyanyasa,siku moja akaingiza mwanaume ndani, chumba ninacholala mimi na yeye, walijua nimesafili nilikuwa nakuja huku lakini ndege ikawa imeniacha..
Na mzee pia alikuwa kasafiei na mama,niliingia milango ilikuwa wazi, hata mlinzi getini hakuwepo, nilivyofika chumbani, nasikia sauti za chumbani kufika namkuta wanapeana na mlinzi kitandani kwangu, walivyoniona walishtuka,mwanaume akawa anataka kukimbia, mwanamke anamvuta ajikinge, mwanaume akampush akadondoka,akadondokea tumbo…
Ikapelekea mimba kuhalibika, ilibidi nimuwahishe hosptal nikwajulisha mzee na mama wakaja, niliwasimulia hali halisi, lakini uyu mwanamke alikana akasema namsingizia kwa kuwa simpendi, niliandika sain talaka, nikaiacha hapo, nilivyoona familia yangu pua hawanisaport nikaamua kuondoka, ila mzee aliniamini, akaomba nisamee, nilishindwa..
Lasmi nikahamia Tanzania, alikuja mpaka huku nilimfukuza zaidi ya mala 9, ndio maana nikajenga hii nyumba akija huwa naondoka mpaka siku akiondoka ndo naludi, huu ni mwaka wa 4 toka nimemuacha, lakini haelewi,kukuoa wewe ni kwa sababu sitambui kama ninamke ni karatasi tu bado ila nitajitahisi asaini na nitafunga ndoa ya milele ya mke mmoja tu, niliogopa kukwambia sikutaka kukupoteza mke wangu naomba unielewe mke wangu nakupenda sana….
EP 14
Sikujibu kitu zaidi ya kulia tu, alizidi kunikumbatia uku ananiomba msamaa, P naomba niludi kwanza nyumbani, p alikataa kabisa akasema nimpe muda kila kitu kitakuwa sawa, sisi tutaishi hapa hapa, kesho nitamleta bibi, kule sio salama, wale wanawake wawili wana roho mbaya mno…
Na dada wa kazi nitakutafutia naomba unielewe, sikujibu chochote nililala tu bila mwafaka, asubuhi niliamka nakuta P kakaa ananilinda, nilivyoamka ananiuliza naend wapi, ata sikujibu, nilianza tu kufanya usafi, nikapika na yeye akawa ananisaidia, kidogo bibi akaletwa na Amir, chumba chake tayali P alikiandaa usiku…
Nilimuandaa bibi vizuli, alikuwa na msaidizi wake, niliandaa chakula nikajikaza nikaenda kumlisha, Bibi aligundua nina huzuni leo, alianza kunipa ushauli, nakuniomba niwe imala, nilijikuta nalia bibi akaomba nilie kando yake nitoe machungu yangu, nililia P alivyoniona nibavyolia aliumia mno, akaniuliza “Le mke wangu nuambie basi nifanyaje ili usilie, unielewe uwe na amani niambie basi mke wangu…
Sikujibu chochote, bibi aliomba tukae wote aongee na sisi alitujenga na kutuambia hakuna ndoa nyepesi bila msamaa, bila mshikamano, tukitaka kushinda kwanza kila mmoja amwamini mwenzake hata ikitokea nini asimshuku mwenzake hasa mbele ya adui, hili jambo liwe chachu ya kutuimalisha kuwa bola zaidi, tusikate tamaa na kulia lia, tunatakiwa kujua kipi tufanye, huu muda tunaolua umetosha sasa, tunatakiwa kupambana, lakini pia tunapaswa kutafuta pesa yote yanatutizama, tukiyapa maumivu nafasi kubwa tutashindwa kupambana na tutapoteza vingi…
Vita ya ndoa anaepaswa kuilinda kwa juhudi kubwa ni mwanaume, ili mwanamke awe imara kwenye ndoa na bora, anatakiwa kuwa na mwanaume anaemuamini, kumpenda na kumpa kipaumbele,ukimpa mkeonkipaumbele, atapata nguvu ya kukulinda na kuvumilia, na kutafuta njia za kuepukana na vioja vya maadui, lakini mme ukiwa kimya humpisaport mke wako hueleweki uko upande gani unamuua mkeo nguvu yakuwa na wewe, ata kuvumilia au kutatua tatizo, aliki ya mwanamke ni hatali sana ikiwa na utulivu, ukimpenda wewe mme wake ukampa utulivu mke wako awezi kukuangusha…
Atasimama imara na kuja na njia ambazo hutoamini salama na zakushinda, alitupa wosia mwingi mno, kidogo nikashusha hofu yangu japo bado nilikuwa na hasila na P kwa nini asingeniambia tu mapema, tulimaliza kuongea na bibi, tukatoka nikamuomba P niende nyumbani baada ya chakula cha mchana, P akakataa akahisi bado ninahasila nitakatalia kwetu, alivyogoma sikuwa na jinsi, nikaingia chumbani angalau tu nilale make kichwa kilikuwa kinaniuma vibaya mno…
Nimeingia chumbani na P nae kama mkia, akasogea mpaka nilipo, akawa anaongea mimi atasikuwa namsikiliza, nilikuwa nimechoka na kichwa inauma nikapitiwa usingizi, P amekuja kushtuka anaona niko kimya sana, ni machozi tu yanamdondokea, akacheki nimesinzia lakini machozi yako mpaka usingizini,aliumia mpaka ata kazini akawa anashindwa kwenda, zilipita wiki iliyofata akapigiwa simu kuna mwekezaji mpya, akamtuma bamdogo wake amsaidie kupitisha kama iko sawa…
Walikubaliana na huyo mwekezaji akaomba nafaso ya binti yake ajifunze kazi wakaandikishana adi mkataba wa kazi wa miaka mitatu,wa uyo binti, kama sectary, P alikubali, kwa sababu Amir, anampango nae mwingine mwezi ujao, kina kampuni nyingine, ya magari amefungua anahitaji kuia kipaumbele, inafanya vizuli sana kuliko ata hii kampuni mama…
EP 15
Alikubali kila kitu,baada ya wiki 2 tuliingia wote kazini mimi na yeye toka tufunge ndoa ni mwezi sasa hatujafika ofcn, ajabu kufika sectary alieajiliwa ni mke wa P, na ameshajitangaza na picha ya ndoa yao kabandika ukutani kwa kila mfanyakazi, ni kusemwa tu nasemwa, yani niliishiwa pozi, P hakuingia ofcn alikuja ofcn kwangu, kakuta ninaandika barua ya kuacha kazi, alinikumbatia tu…
Akaitisha mkutano wa wafanyakazi wote,kumbe yule mke wa p alivyojua tu leo tumefika alihisi tu ataaibishwa, akampigia mama mkwe wake aje kuokoa jahazi, tukiwa kwenye mkutano wa dharula, P aliwatangazia wote marufuku kuweka picha yoyote ofcn kwake, kama sio yeye, basi mtu mwenye mamlaka ni mimi,huyo mwingine yeye hamtambui ni ex wife,mbele ya mkewe, mwanamke akainuka akaanza kutengeneza ramasha, apo kashjifinza kishwahili japo hajakushika sana ila tayali kashaanza kukijua na anakiongea..
Bado hatujatulia mama mtu kaja, kawaka vibaya mno, P alichofanya aliita walinzi wamtoe mama ake na mke wake afu akatoa tamko, anamke mmoja sasa mtu ajimix, akanitoa nje tukapanda gari kurudi nyumbani, nilikuwa kimya nikamuomba tu anipeleke kule kituo cha kulelea watoto, alinitizama na kuniomba msamaa, akasema hatuwezi kwenda mikoni mitupu tupite tuhemee, vitu yeye bale ni mfadhili pia siku ile ananikuta pale alienda kusaini mkataba wa ufadhili…
Tulihemea vitu vya kutosha tukaenda bavyo, watoto walivyoniona walifurahi, walinifanya nikasahau kabisa kama niko kwenye matatizo makubwa, P alifulahi mno kuona nilivyona furaha akajua kabisa kumbe nikiwa siko sawa, awe ananileta apa, na kabla hatujaondoka bibi akaja na yule mtoto aliemchukua apa nilifurahi kiwaona jamani, bibi alinijaza pia ushujaa tukampa pesa na joel mtoto aliem adapt tukaomba aje afike nyumbani ajua dada ake naishi wapi…
Tuliondoka nikiwa bado natamani kubaki ila sina ujanja, lakini leo nilikuwa na amani japo sio sana ila angalau,P aliniuliza najisikua kufanya nini, nilimwambia tu anifungulie biashara mimi kazini tena siendi, alikubali akasema alishafanyia kazi hilo, ametafuta flane tupite nizione, kwanza zimepatikana nne, tulipita kuna hio location moja aisee ilikuwa pazuli mno, ila kumbe ni jilani na kampuni mpya ya P mi ata sikujua na niliipenda…
Alikubali na kusema, “Le wewe ni ubavu wangu halali hapa ulipochagua ni jilani na kampuni ya mmeo, muda huo tayali nilishasaini nakulipiwa kodi ya miaka miwili, nikashangaa akanipeleka mpaka pale, akanitambulisha kwa wafanyakazi, akaomba mtu yeyote akija ata kama anapicha ya ndoa yake na yeye, asipewe nafasi ya kuingia aliwapa angalizo na ata kama ni mzazi wangu, wote walielewa Amir alikuja pia, akasema gari ya shem imeshafika naomba nikaichukue bandarini, nilimtizama P nayeye akanitizama, akamluhusu Amir akaomba tubaki wote mpaka Amir aje ndo tuondoke lakini pia anahamua hapa lasmi kufanya kazi kule ataenda Bamdogo wake…
Hii ilinifulahisha sana, nikamkumbatia kabisa, akajua wivu ulikuwa unanitafuna kimya kimya,nilikaa nae tukaagiza chakula ila mimi kikanishinda, nikawa sikielewi, ikabidi niagiziwe kingine nachenyewe kikanishinda, ” Le mke wangu au unaumwa? Ata sijui lakini nina njaa sana, adi nikaanza kulia kisa njaa,P akachanganyikiwa akapika dada anauza keki za vipande, nikamuita uku nalia nikachukua moja ikanivutia nikaomba kumi, P alinitizama akakausha ila kwa ulaji wangu alijua kabisa kumi siwezi huwa nakula mbili au moja…
Alilipia nikaanza kula nilizipiga zote nikaagiza na soda sprite,nikaipiga yote, sikubakiza chochote,apo nikawa na furaha tu,P alinishangaa mpaka nikajua ananishangaa nikaanza kulia, akajua sasa hii mbona mpya sio kawaida yangu kulia lia ovyo..
Inaendelea….đź’Ą

