HUWA ANASUBIRIA NISINZIE, NDIO AANZE KUNIINGILIA
Kaka habari mimi ni mama wa watoto wawili naishi na mme wangu tangu tufunge ndoa Sasa tuna miaka 4..
Lakini kilichonileta kwako ni kwamba.. Mume wangu ni mtu ambae hajali kabisa kuhusu mimi hanaga muda na mimi hata nikimuomba tupate nafasi ya kuzungumza na nimshirikishe ninavyojisikia kuhusu upweke anakubali tu lakini hatimizi
hata kunitunza hanitunzi hata watoto kuwanunulia mawazi ni mpaka mimi kwa kuwa na mimi Nina kibarua ndio hicho kinakua kinanisaidia na hata swala la chakula anahudumia lakini sio kwa kiasi kinachotakiwa na kwa asilimia kubwa mimi ndio nakua na mzigo mkubwa zaidi nikipata kihela huko kwenye kibarua changu inabidi niwanunulie watoto chakula na vi mavazi yaani mpaka mimi najisahau kujinunulia hata nguo ili tu watoto wangu wasikose kula na kuvaa
Pesa ya matumizi huwa haniachii ni mpaka nimwambie na nikimwambia ananiachia 1000 ikizidi sana 2000 nikimwambia haitoshi anakuwa mkali anasema Hana pesa nimekua nikiumia sana na Kila kitu mpaka amwambie mama yake hata tukikosana
Hata kwa swala la tendo la ndoa nimekua ni mtu ambae sifurahii kabisa maana Huwa hakuna maandalizi yeyote na Huwa anasubiria nikisinzia ndio anaanza kuniingilia nakua napata maumivu makali na akishamaliza aniniacha tu hivyo hajali kabisa kama na mimi natakiwa kufurahia
Nimekuwa nikiishi tu hivyo Kuna muda nawaza hii hali itaisha lini na hapo nyuma nimeshawahi kufuma sms za mwanamke mwingine akimwelekeza Lodge aliyochukua kwa ajili ya kufanyia mambo Yao nilipomwambia akawa mkali anasema mimi ndio chanzo Cha kumfanya akachepuke na kwa wakati huo mimi nilikua bado mzazi Nina wiki 3
Je kwa mtu wa tabia kama hii nawezaje kuishi nae ili na mimi nisiwe namfikiria ? maana yeye hanaga muda na mimi kabisa niombee ushari kwa folowers wako kaka samahani kwa gazeti..

