HIVI NI SAHIHI MAMA KUINGIZA MWANAUME NDANI, MBELE YA WATOTO WANAOJIELEWA?
Kaka shikamoo, mimi ni binti wa miaka 19 nina wazazi wangu wote wawili ila walishatengana, nimelelewa na bibi yangu tangu mdogo hadi namaliza kidato cha nne mwaka 2024, upande wa mama tupo watoto watatu na kila mtu ana baba yake.
Kilichonileta hapa ni kuomba ushauri, kipindi nasoma secondary likizo nyingi nilikuwa naenda kumsalimia mama ila kitu cha kushangaza alikuwa analeta mwanaume ndani, nimeenda kumsalimia kama mara 3 hivi yani kila nikienda nakuta ana mahusiano na mwanaume mwingine jumla ya wanaume nilioshudia akiwaleta ndani ni wa tatu achana na baba wa wale wadogo zangu
Shida inakuja hivi yaani kila nikikumbuka anayoyafanya najikuta nimekasirika ghafla na Kulia kila akininiuliza sababu za kukasirika nasema hakuna shida yoyote yeye anachoamini ni kwamba mimi namdharau mara nina kiburi mimi simdharau namheshimu kama mama yangu ila kila nikikumbuka anavowaleta ndani naweza nikakasirika hadi nashindwa kula siku nzima kuna muda nasema bora niache kwendaa kumsalimia ila ndo hivo siwezi kuacha ni mama yangu na nampenda sana,
Hivi ni sahihi mama kuingiza mwanaume ndani mbele ya watoto Wanaojielewa ?

