DADA WA KAZI KANIPINDUA, NIKAFUKUZWA AKAOLEWA YEYE NA MUME WANGU
Mimi ni mwanamke ndoa yangu ina miaka saba sasa. Nimevumilia mengi kwenye maisha ya ndoa, nimehangaika kujenga heshima ya familia yangu. Niliamini tumebarikiwa, maana tuna kila sababu ya kufurahia. Tumebarikiwa watoto wawili.
Lakini naandika haya nikiwa nimevunjika moyo. Tatizo lilianza pale tulipomleta dada wa kazi. Nilimchukua kwa nia njema, atusaidie majukumu ya nyumbani kwa kuwa mimi nilikuwa na majukumu mengi kazini. Nilimchukulia kama mdogo wangu, nikampa uhuru wa kutosha.
Baada ya muda, nilianza kuona mabadiliko kwa mume wangu. Alianza kunidharau, kunijibu kwa ukali, na hata mara nyingine analala sebuleni. Nilidhani ni changamoto za kawaida za ndoa. Siku moja jirani akanivuta pembeni na kuniambia..
“Dada, kuwa makini. Yule dada wa kazi ni mchawi, nimeona kuna vitu anafanya kwenye bustani nyuma ya nyumba yenu.”
Nilikosa amani. Nilianza kumchunguza. Nilikuta vitu vya ajabu chumbani kwake, vitambaa vimefungwa pamoja na nywele, poda, na maji yaliyowekwa kwenye chupa ndogo. Nilipomwambia mume wangu kuhusu haya, hakuniamini. Badala yake, alinigeuzia kibao na kuniambia mimi muongo nina chuki binafsi na huyo dada.
Cha ajabu zaidi, wiki mbili baadae, mume wangu akanifukuza nyumbani. Aliniambia kwa ukali kuwa niondoke na huyo dada wa kazi ndio atabeba majukumu ya nyumbani.
Nilihisi kama dunia imenichoma na kisu moyoni. Dada wa kazi aliyekuwa ananiita dada kwa heshima, sasa amegeuka kuwa mke wa mume wangu?. Nimebaki najiuliza ni uchawi kweli umehusika hapa, au ni tamaa tu za mume wangu? Nimehangaika kwenye maombi, nimepiga magoti, lakini bado moyo wangu umejaa maumivu makali.
Nikimuomba anipe taraka anasema mimi niende tu mahakamani akiitwa atakuja kujibu.. Lakini mimi nampenda sana mume wangu,tumetoka mbali nae mpaka hapo alipofika kuna juhudi zangu nyingi..
Naomba msaada wa mawazo yenu, maana moyo wangu umechoka lakini bado naona kama nina haki ya kusimama kama mke halali.

