Daah.. Kumbe Kila Tukifanya Mapenzi, Mume Wangu Ananirekodi Video
Shikamoo kaka samahani nipo hapa kuomba ushauri maana aapa sijui nakufa au naelekea dunia ya ngapi ni hivi nina mwanaume nimezaa nae mtoto sasa ana miezi nane yeye binafsi ana miaka 44 mimi nina miaka 25 sasa ni hivi jana usiku alirudi kazini nikampokea vizuri pole na kazi namuuliza mbona nakupigia simu hupatikani akanipa simu ananiambia angalia kama simu imezima
Hapo sasa nikapokea, napokea tu kutoa paswedi nilicho kiona mpaka kwenye utumbo mpana ulitetemeka kajisahau sijui kufuta nimekuta kamtumia mwanaume mwenzake video za uchi kumbe akifanya mapenzi anarekodi kimya kimya bila anaefanya nae kujua nimekuta kamtumia mwanaume mwenzake video za wanawake tofauti tofauti zaidi ya wanawake kumi
Sasa kinacho niuma mpaka mimi ninaeshi nae na nimezaa nae kanirekodi bila hata mimi kujua jana ndiyo nimeona ya ayubu nilihisi kufa kufa nguvu zote ziliniisha sasa nikasema nijitumie akashtuka simu yangu lete kanyakua haa!! namuuliza nini hicho uku natetemeka mpaka mkono yupo kimya halafu alimtumia na ujumbe nishachoka kufanya na wanawake anamuandikia huyo mwanaume
Mie huyo mwanangu mgongoni na begi anakubali sasa niondoke kapambana nilimpa makofi nilimng;ata hasikii anazidi kunizuia kuomba msamaha mpaka majirani wooote wameamka sasa nikakubali kulala nimelala sebuleni saa kumi naamka kujiandaa na safari naamka simu ya mama yake inaita napokea naambwia na fulani unaondoka nikamjibu nishakata na tiketi tayari kapambana usiondoke usiondoke hata hiyo tiketi iende bure nitakupa hiyo hela yako
Sio dakika baba mkwe kapiga kaongea usiondoke namjibu tu baba hapana ngoja niondoke kaongea unanidharau kwanini uondoke naomba njoo nyumbani nimekataa mwisho akaanza kuongea maneno makali kama laana fulani hivi kuwa simsikilizi kwanini nisiende halafu kwetu nikaondokee kule mwisho maneno ya mzee yalinitisha mbona nikakubali sasa hapa nimekata tiketi la basi la saa mbili usiku naelekea huko kwa wakwe plees ushauri wenu pleas mpaka sas asijala chochote nalia tu

