Anataka Kumuacha Mume Wake, Nimuoe Mke Wa Pili, Ili Nimzalishe Watoto
Nilipokuwa nahitaji kuoa kuna mchunba nilionyeshwa na baba yangu, alikuwa mzuri haswa, ila mzee aliambia kama umempenda nataka umtongoze mwenyewe mkikubaliana basi uniambie tupeleke posa. Nikafanya hivyo, kama kawaida akaanza kuringa almost mwaka mmoja, ila sikukata tamaa sababu nilimkubali sana.
Lakini akaja akakubali sikumwambia mzee nikaendelea kukaa nikasema huyu mpaka niichape kwanza. Basi wakati naendelea nae mtaani kulikua na binti fulani mkali sana, sasa alikuwa ni rafiki wa watoto wa kaka yangu mkubwa ambao ni mabinti wakubwa wanasoma chuo.
Sasa mimi nlikuwa namchukulia kama mwanangu coz nae ananiita baba mdogo kama wale mabinti wa brother.
Wakasoma wakamaliza wakati huo nishamaliza chuo napiga kazi sekta binafsi, mambo yalipoanza kukaa poa nikapanga room nikahama pale home. Siku moja nikapokea simu ya yule binti anaeniita baba mdogo, akaniambia wanao wamenambia umehama kwani umehamia wapi, nikamuelekeza akasema weekend nitakuja kukusalimia…
Mmmh nikasema huyu mtoto anautaka kumbe, nikamwambia karibu, basi bwana nikajipanga geto lilikuwa kali kiasi, mara paaah saa nane mchana jumapili huyo hapo.
Nikamkaribisha ndani akaingia chumba master. Akaanza aaah bamdogo nasikia joto nikamwambia ingia chooni ukaoge mimi nakupisha halafu nawasha feni utakaa poa tu, akasema sawa akaingia bafuni akaoga heeeeeh katoka na taulo tu… Aaaaah kilichoendelea mshakielewa…
Basi bwana saa moja moja nikamsindikiza home kwao.
Narudi niko njiani yule mchumba niliekuwa namfukuzia nilieambiwa na mzee anapiga simu, ananambia nataka kuja kwako nipaone, nikamwambia karibu, mara paaaah narudi kazini siku ya Jumatano huyo…… Kajibebisha hapo tukapiga stori mara kijasho akasema akaoge nikamwambia sawa tukaoge wote akasema hakuna shida… Kilichoendela ni stori ya kuanza maisha.
Basi nikamwambia mzee ili sasa apeleke posa tuandae harusi, coz mama alikuwa ananambia anataka mjukuuu sasa. Sasa kumbe yule binti anaeniita bamdogo rafiki wa watoto wa brother alitumwa na mama lakini mama hakunambia, basi mzee hakuchukua muda akaenda ukweni kule, akayajenga na mzee mwenzie wakayaweka sawa.
Shughuli ikaanza kwa huyu binti anaeniita bamdogo, daaaah mtoto ananipenda ni balaa, kila siku mazawadi, basi one day nikamwambia kama utani tu, utajiskiaje nikioa mwanamke mwengine, alinambia nitakuroga hiyo ndoa ife au najiua… Maana nakupenda sana.. Daaaah hapo nikasema sasa nimeanza kuyakoroga maana process za ndoa zilikuwa zinaendelea.
Basi ikaenda mpaka nikaoa kweli, aisee yule binti anaeniita baba mdogo alilia nusu ajiue, ikabidi nimplizi sana nikamtafutia dada mmoja mwanasaikolojia akaongea nae sana, akakaa sawa ila nikakata mawasiliano kwa usalama wa ndoa.
Basi kuna jamaa alikuwa anatafuta mke nikamuunganisha bila kujulikana wakakutana nae akaolewa… ndoa yangu ikawa salama.
Sasa changamoto yule binti hapati mimba. Wakati huo mimi na mke wangu tuna watoto, binti katafuta namba yangu kanicheki, anaomba tuonane, nikasema hakuna shida. Kumbe amejipanga eti nimpe mimba maana anahisi mume anashida…
Nikamwambia kwa sasa siwezi beba hiyo dhambi, akasema kunioa ulikataa hata hili dogo pia…Nkamwambia wacha nimfikirie kwanza. Sasa ili nisimvunje moyo nikamuahidi nitafanya lakini sikuwa tayari.
Juzi kati mke wangu kaenda kujifungua maana baadae niliajiriwa serikalini mkoa mwingine na mama alifariki sasa nikamuomba mama mkwe akae nae kipindi hiki kigumu, maisha ya kukaa peke angu yule binti akatumia hiyo nafasi ya upweke wangu sasa. Kila mara simu mara meseji, kumbe hayupo kwa mume wake amekimbia maandamano ya Disemba 9.
Akanambia nataka kuja ulipo, nitakupa pesa unayotaka, halafu nitakupa duka la nguo moja, na kama hutaki kunipa mimba mimi navunja hii ndoa unioe mke wa pili, kwa maana miaka yote hii sina hata mtoto na kila nikipima naambiwa sina tatizo sasa maisha gani haya mwenzangu nikamwambia tukapime hataki….
Sasa nimekuja kwako kuomba ushauri, huyu binti ndoa yake ina miaka minne sasa, hana mtoto lakini biashara zake zimeimarika vizuri na huwa ananishikisha baadhi ya vitu, je nimruhusu avunje hiyo ndoa kweli halafu nimvute mke wa pili…?
Hofu yangu ni je…? Nikishakubali huyo mume wake nae atakubali kirahisi maana ni kweli mimi ndo nilinuunganisha lakini huyo jamaa hanijui maana nilikuwa kama third party tu. Nisije kufa kizembe nikaacha watoto wangu.
Ushauri wenu wapendwa, nimpe huo ujauzito anaoutaka kitu ambacho sikubaliani nacho… Au avunje hiyo ndoa akae eda alafu nioe mke mdogo niwe na miji miwili maisha yaendelee….? Kumbuka hata mimi nishajipata so wala sina shida na hivyo vi ahadi vyake, ila sasa kiukweli namkubali sana lakini bado moyo wangu haujui lipi ni lipi nahitaji mawazo mbadala….
Kiufupi bado nampenda lakini sitaki niwe sababu ya kuharibu ndoa naomba ushauri kwa wadau.

