ANANIAMBIA WAHI KAFUNGUE DUKA, KUMBE LENGO LAKE ALALE NA MDOGO WANGU
Nina umri wa miaka 32 na ni mama wa watoto wa 4, mimi na mme wangu umri tuko sawa, kati ya hawa watoto wawili ni watoto wa baba mwingine yaani mtoto wangu wa kwanza na wa pili. Pia nimebahatika kuzaa na mme wangu watoto wawili pia.
Kaka huyu mwanaume sio mtu mbaya sana kwa familia yake yaani ni mtu anajali na hajawahi kuwabagua watoto kabisa kwani anawalea vizuri tu, tangu tukutane walikuwa wadogo kawalea kama watoto wake tulikuwa kwenye upangaji hadi tukafanikiwa kujenga na kupata mafanikio kidogo. Huyu baba so kwamba hali ya ugomvi ndani haikuwepo ilikuwepo sana ila ndo hivyo ndoa ni uvumilivu kama kunipiga kanipiga sana tu ila bado nipo napambana nae kibishi bishi. Kumbe kadri ya siku zinavyoenda kila binadamu uzaifu wake ndo unaonekana,.
Mme wangu ni mpole sana nilimuamni vibaya pale wanawake wenzangu walipolia na kunisimulia maisha ya ndoa zao mimi nilijigonga kifua na kusema kumbe mimi nimeolewa,,,la hasha kumbe bwana hakuwa hajapata vijisent na sikuwa namjua zaidi nimekuja kumjua kuwa ni professional pale alijisahau akaja na simu yake ndogo aiseee mmmh.haikuishia hapo yaani nimetoka kulala nae mimi usiku asubuhi ananiambia wahi dukani kafungue kumbe lengo alale na mdogo wangu. Na hiyo siku nilimfuma live live sikuwa na cha kumwambia bali nilimsamehe tu.
Ikajirudia tena kwenye simu yake nikakuta video za ngono alizosex na wanawake zake tena tofauti tofauti napo sikusema nilinyamaza kumbe inaniathili kwa ndani sasa hivi nimekuwa mtu wa kustuka stuka tu yaani mapigo ya moyo yako mbio mbio yaani nikimuona roho iko juuu juuu tu upendo haupo yaani nimechoka kuna time natamani niachike ila ndo hivyo tukikaa sawa nasahau.
Sasa kinachonishangaza mwanaume mwenzenu hajawahi yatambua makosa yake na sidhani kama anajua kama nimeathilika sasa hivi yeye ndo amekuwa wa kunitafutia ugomvi yaani anatafuta sababu tu ili tu niongeee anipige anapenda sana kupiga aliwahi nipiga nimetoka kujifungua alooo sitasahau aliponivunja mguuu ko sasa hivi amekuwa mtu wa kunichimba sijui anataka nini , ukikaa na wanawake wenzio kesi , dukani akija mteja wa kiume na awe mgeni kesi na hata hawa tu anaowajua akijirudia rudia kuja kwangu ni kesi, chooni uende na simu make akipiga usipokee kesi ,akichukua simu akakuta namba ngeni hata wewe mwenyewe huijui kesi ,akipiga simu akute inatumika kesi yaani siku hizi haeleweki kazi hafanyi kwa weledi kama mwanzo amekuwa mvivu tu yaani muda wote akuchungechunge tu hata ukiwa umekaaa umetulia anauliza unamuwaza nani
Mimi naomba nisaidiwe majibu na wanaume niishi nae vipi huyu mwanaume mwenzenu? Nimejaribu hata kuishi kwa kuigiza imeshindikana . Ni stori ndefu hata siwezi maliza andika yote, yote kwa yote nyie wakaka mimi kupigwa sasa hivi nimechoka maana rafiki yenu hajui hata kupiga huwa natamani apate hata msela mmoja amletee dharau amtwange kisawasawa nb sasa hivi akija kunipiga nataka nimfunge maana nimeshamwambia kama anaona simfai aniambie niondoke ila anakwambia kuna siku nataka nije nikukanyage sasa nami ikitokea akanikanyaga asiniue lazima alale sero, nisaidieni niishi nae vipi,,

