ANA WANAWAKE HUKO NJE, LAKINI HANA MTOTO HATA WA KUSINGIZIWA
Habari, Mimi ni mama mwenye mtoto mmoja Nina miaka 32 ninaishi na mwanaume huu mwaka wa 6 hatujabahatika kufunga kupata mtoto ila mimi kanikuta nina mtoto mdogo sana yeye ndo kamlea mpaka sasa mtoto ana miaka nane, napitia changamoto ya kukosa mtoto mwanaume ananidharau kuwa sizai na wakati yeye ana wanawake huko nje lakini Hana mtoto hata wa kisingizia hata ukimwambia twende hospital tukapime hakuna ushirikiano kabisa
Mimi Nina kazi na najipambania sana sio mwanamke ambae nimekaa nyumbani bila kazi namsomesha mwanangu shule ya gharama tu lakini moyo wangu unaugua maana mie ndo naonekana mgonjwa sizai mpaka walishamipeleka kwa waganga kuangalia kama nani ana shida nikaambiwa mimi ndo Nina shida lakini mwanaume Hana shida yoyote na wakaniambia akitoka nje anapata mtoto na mimi nikitoka nje napata mtoto najiuliza hiyo ni sayansi gani ya namna hiyo?
Nabaki na maswali je mimi ni mgonjwa au mwanaume ndo mgonjwa niko njia panda naombeni ushauri maana nimechoka matukio kila siku pia naogopa nisije nikaletewa magonjwa maana mwenzangu anahangaika na wanawake yeye kazi yake ni dereva mimi nimeajiriwa shirika binafsi sijui naanzia wapi kutoka kwenye hili dimbwi maana nilimpenda sana huyu mwanaume. Asante naomba ushauri

