Alinifumania Akanisamehe, Sasa Amekuja Kutuingilia Mimi Pamoja na Shoga Zangu
Mimi nimekaa na huyu kaka kwenye mahusiano Kwa miaka miwili, tulikuwa na mpango mwakani tufunge ndoa, alikuwa amesha nitambulisha kwao na marafiki zake wote mpaka kazini kwake.
Sasa mwezi wa tano Shetani alinipitia nikawa nimempata mbaba hivi alikuwa ananisumbua sana Kwa muda mrefu, Sasa kutokana na yeye kuwa ananipa vitu vingi sana ikabidi tu nimkubalie, yule baba yeye ni mtu mzima na ana familia yake.
Huyo baba nimekaa naye kwenye mahusiano miezi miwili ndo mchumba wangu akajua, siku Moja Niko hotelini na yule mbaba mchumba wangu alinifumania akiwa na marafiki zake, hakufanya kitu chochote wakaondoka.
Ilipita kama wiki hatuna mawasiliano ikabidi Mimi nianze nikawa nampigia simu hapokei, natumia sms za kuomba msamaha lakini Bado hajibu, mwisho nikaanza kuwa nawatuma marafiki zangu kuniombea msamaha, Sasa mwezi huu 9 alinijibu akaniambia amenisamehe, akaniambia niwaambie marafiki zangu wajiandae atutoe out Ili kufurahia.
Tarehe 12 tulitoka ila mida ya saa tano usiku akatuambia tuna onaje tuchukue vitu tukafurahie kwake, tukaona sawa akachukua nyama kilo 4 na vinywaji vingi tuka ondoka, tulivyo fika kwake tulifurahia sana, sijui hapo katikati kilitokea Nini, tulikuja Kuamka asubuhi wote tupo uchi sebuleni tume ingiliwa mpaka kinyume na maumbile Mimi na marafiki zangu wawili, halafu inaonekana tuliingiliwa na mtu zaidi ya mmoja.
Baada ya hapo alituomba tuondoke kwake tulipiga sana kelele tukiwa pale nje kwake na watu wakawa wamekuja, tuliwaeleza ila wote wakawa upande wa mchumba wake, Kuna mama mmoja alionekana ni kiongozi wa mtaa akatuambia tuondoke kabla hajaita polisi , Ilibidi tuondoke tu na Toka siku hiyo akaniblock kabisa na hatuna mawasiliano.
Kinacho niuma dada yangu ni huu unyama alio tufanyia.

