AKIFIKA TU HUNIFANYIA UKAGUZI, KWA KUNIINGIZIA VIDOLE SEHEMU ZA SIRI
Hello habari, Naomba unipostie kwa fans wako nipate ushauri wa hiki ninachokipitia……
Mimi ni msichana age yangu 27 naishi Dodoma. Miaka mitano iliyopita nikiwa naishi na kufanya kazi ya kuuza duka la dada yangu nilijikuta naingia kwenye mahusiano na baba mmoja mtu mzima age yake 58 ambaye alianza kunishawishi kwa ofa mbalimbali akija dukani na mwisho nilijikuta nimeimgia kwenye mahusiano. Alidai kuwa amenichunguza mimi ni binti mwenye tabia nzuri anataka kubadilisha maisha yangu.
Alinipangishia apartment na kunishauri nihame kwa dada yangu na aliniahidi kunifungulia biashara. Kweli alinipa mtaji wa kufungua salun ya kike na kabla ya kufungua alinilipia ada nikasomea kozi Ususi na Urembo.
Baada ya miaka kadhaa maisha yalianza kubadilika ambapo mwanzo alikuwa akiishi Arusha na familia yake na tulikuwa tukionana akija Dodoma kwenye vikao vya serikali. Cha kushangaza akahamia kikazi Dodoma na tukaanza kuishi wote. Kuna siku nilimsikia akiongea na mwanasheria wake juu ya kumpa talaka mke wake hapo ndipo akili yangu iliposhtuka ikabidi nimuulize kwa nini anataka kufanya hivyo hakunijibu kitu alinipotezea tu ila nilimshauri afanye hivyo nashukuru hadi sasa anaendelea na mke wake japo kuwa migogoeo ipo na pia haya mahusiano mke wake anayafahamu.
Amekuwa na wivu ulipindukia hataki nifanye kazi, haniruhusu kwenda sehemu ambayo yeye hayupo na hata salun huwa ananipeleka na kunirudisha yaani hata kupanda usafiri wa umma (pikipiki, bajaji au daladala) hataki ikabidi aninunulie gari kwa kuhofia kuwa nitatongozwa.
Mwanzo nilijifariji kuwa huenda wivu ule unatokana na performance yake hafifu kitandani (Jongoo anawika kwa shida sana hata akijitahidi kuwika anaishia kukoroma tu) nilivumilia kwa kuwa napata mahitaji yangu ila kwa sasa nauona mwisho wangu.
Kuna siku tuligombana sana akaamua kubeba vitu vyake na kuondoka zake kwa kutumia ile gari ambayo alininunulia kwa jina langu. Nilipomwambia asiondoke na gari langu alicheka sana kwa dharau
kumbe alishaibadilisha umiliki bila hata mimi kujua na inamsoma yeye. Aliondoka ila baada ya wiki kama mbili alirudi na kuniomba msamaha ila ile gari hakurudi nayo na mimi nikaamua kuipotezea tukaendelea kuishi.
Mara nyingi huwa anasafiri kwenda kwenye vikao vya serikali mikoani na hata nje ya nchi hapo ndo huwa tunagombana sana maana huwa anataka tusafiri wote nikimwambia kuhusu usimamizi wa biashara yangu anasema kwani inaniingizia bei gani yupo radhi anilipe hata two million nisafiri naye ila sio kuniacha na nikikomaa kutokwenda atapiga sana video call usiku na mchana.
Kinachoniumiza zaidi mara nyingi akitoka kazini iwe nimeshida saluni ama nyumbani akifika tu hunifanyia ukaguzi kwa kuniingizia vidole sehemu zangu za siri eti anapima kuona kama nimechepuka inaniumiza sana
Mwaka jana 2024 alininunulia kiwanja hapa Dodoma ambacho kiliandikwa kwa jina langu na mwaka huu mwezi uliopita alianza kunijengea nyumba. Kwa sababu aliniambia itakuwa nyumba yangu niliona sio vyema nisiweke jasho langu ambapo nilichukua akiba yangu yote 19,000,000/= niliyokuwa nimejiwekeza benki ili aiongezee kwenye ujenzi japo kuwa yeye katumia gharama kubwa zaidi lakini nilipata mshituko baada ya kuona hakujali hata kidogo huo mchango wangu. Ujenzi upo asilimia 90 sasa na kuna dalili za kunigeuka kama aliyonigeuka kwenye issue ya ile gari. Nifanyeje ili asije kunigeuka na kupoteza kila kitu ukizingatia akiba yangu yote nimempatia na hadi sasa nina miaka mitano niko naye.
Cha mwisho ni familia yangu, Kuna siku aliichukua kwenye simu yangu namba ya mama yangu mzazi na kuwasiliana naye bila mimi kujua, baadae nikajua na nilimweleza mama ulivyokuwa na umri wake lakini hakuonekana kunisikiliza zaidi ya kusema nafaa kuolewa naye kuwa hana uzee wowote kumbe alikuwa akimtumia pesa na ninavyoongea sasa tayari ndugu zangu wameshapokea posa.
Nisaidieni maana ndugu zangu wameingiwa na upofu wa fedha hata nikisema chochote naonekana mimi ndo mkorofi. Nikiangalia hatima ya maisha yangu sioni maana nawaza nikisema niishi naye ina maana sitazaa maisha yangu yote na nitaishia kumhudumia kama house girl? Sikufikiria kama tungefikia hatua hii, Nilipokosea naomba mniwie radhi ila kwa sasa nisaidieni ushauri nifanye nini?????
Ahsante sana

