CHUKI YA MAMA
Part 2
Nilisoma chuo miaka miwili nikarudi mtaani kusaka ajira, kipindi nasubiri ajira nilifungua office ya ushonaji huku nikimsaidia bibi, baada ya mwaka nilijitegemea nikapanga karbu na bibi maana ilifika mda wajomba wakaoa pale nyumbani familia ikawa kubwa na makazi yakawa hayatoshi.
Hivyo nikaomba nipange nikaruhusiwa nikapanga, nilikuwa na mchumba ila alikuwa masomoni bado. Mwaka 2018 mchumba wangu akahitimu mafunzo ya udaktari akarudi nyumbani aliponikuta nimepanga alinishauri tuishi pamoja ili akipata kibarua aende nyumbani kujitambulisha, niliishirikisha familia wakaniambia tu niwe makini siku hizi watu wanabadilikaga.
Tulianza lasmi kuishi pamoja na mchumba wangu, miaka miwili hakuwahi kupata kazi ila kwa kuwa nlikuwa na office nlifanya kila kitu, baada ya mama yangu kujua nina mtu alianza kunifatilia na mume wake ili wapate mahari lakini nliwaambia mume wangu hajapata kazi akipata atakuja.
Heey! Mama alinibadilikia na kuanza kunitukana kila siku kwamba naishi na mwanaume bure, ila nlikaa kimya. Mwaka ulipita nikapokea taarifa kutoka kwa wadogo zangu kwamba Mama aligombana na mume wake akaondoka nyumbani hawajui alipo, kiukweli nliumia sana maana nlikuwa najua maumivu ya kuishi bila wazazi sikutaka mtu mwingine alipitie hili.
Nilianza kushirikiana na baba wa wadogo zangu kumrudisha mama nyumbani, nilifuatilia hadi nikajua kuna mwanaume amempangishia sehemu nikamtafta huyo mwanaume bahati nzuri nilikuwa namjua nikaongea naye nikamuomba amrudishe Mama nyumbani alikubali na kuniahidi ataongea naye.
Baada ya mama kujua nimejua siri yake alinichukia zaidi na hata nyumbani kwao walinichukia maana alikuwa akiwasaidia shida zao ila mimi sikujali niliwaambia huyo ni mama yangu ikitokea akaharibikiwa mimi ndio ntaubeba mzigo.
Mama alirudi nyumbani ila akiwa na chuki kubwa sana kwangu
Inaendelea.