CHUKI YA MAMA
Part 1
Naitwa Clara nina miaka 29 ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kati ya watoto 8, mama yangu alizaa kabla ya kuolewa hivyo alizalia nyumbani kwao na aliyempa mimba hakuweza kumoa maana alikuwa mme wa mtu, baada ya mimi kufikisha miezi minane mama yangu aliolewa na mwanaume mwingine na kuanza maisha mapya mimi aliniacha nyumbani kwao yaani ujombani.
Niliishi na wajomba na mama wadogo ndio walikuwa wakinilea huku bibi akijitahidi kunihudumia maana alikuwa mtumishi wa serikali.
Niliishi mda mrefu sana bila kuona mama hadi nikaamini bibi ndo mama. Baada ya kutimiza miaka kumi ndo mama alikuja kiniona nikiwa darasa la nne ndo kutambulishwa nikamtambua kama mama lakini sikumzoea mapema, nliendelea kuishi na bibi ndipo mama na mme wake wakaanza kunifatilia wanichukue lakini ujombani walinikatalia.
Baada ya kuhitimu Darasa la saba nilifaulu vizuri sana lakini bibi ndo alipambana kunipeleka shule maana mama alisema asihusishwe kwa lolote maana nmekataliwa.
Nilifanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza hadi nikamalza kidato cha nne bila mchango wowote kutoka kwa wazazi. Huko mama akawa ameshazaa watoto 7, matokeo yalitoka nikawa nimepata 4 ya 26, ila bahati mbaya bibi akawa amestaaf kazi, hivyo nlikosa msaada wa kuendelea na masomo japo nlikuwa nimetuma maombi vyuo tofauti na vyote nlikuwa nachaguliwa.
Mama yangu tayari alikuwa amewekeza nguvu zaidi kwenye familia aliyoipata huko, upande wangu nilianza kujishughulisha na ushonaji na kwa mda mfupi nlikuwa fundi maarufu sana maana nlishona kwa bidii na machungu makubwa,baada ya kuwa fundi miaka 2 nilipata wazo la kujisomesha nikaApply chuo cha afya nikachaguliwa, nikaanza kusoma huku nikishona.
Inaendelea