BOSS NAONA AIBU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 16
Mimi nilikua mzima na mwenye kuona kila kitu kilichokua kinaendelea, Sam alinikumbatia kwa nguvu sana huku akimshukuru bibi mganga kwa kunisaidia kupona.
Vick alikua anasumbua walimfunga kamba nilizokua nazo mimi, walimfunga kwa nguvu mpaka nikamwonea huruma.
Mara walifika mama Vick, mwenyekiti wa kijiji na wagambo wawili, walisema kwamba wamekuja kumkamata kaka kwa kumpiga mama Vick na kumteka Vick.
Mama Vick alipoona hali ya mtoto wake alianza kulia kwa sauti ha juu huku akimwomba yule bibi mganga aweze kumponyesha mwanae.
Mganga alimwambia anyamaze kama anataka uchizi utolewe kwa mwanae upelekwe kwake au achague mtu yeyote wa kuuvaa huo uchizi kati ya mwenyekiti au wagambo wawili.
Kusikia hivyo mwenyekiti na wagambo wake walisepa chezea uchizi wewe wakiogopa kuchaguliwa na mama Vick.
Bibi mganga akamwondoa Vick uchizi na kumuonya kwamba endapo atajaribu kuchezea maisha yangu au yeyote katika familia yangu ajue ndio mara ya mwisho kuvuta pumzi yake ya uhai.
Vick aliniomba msamaha na kudai kwamba hatorudia tena, mimi bila kinyongo chochote nilimsamehe, wakaondoka na mama ake. Bibi mganga nae aliomba kuondoka zake.
Kwa furaha aliyokua nayo Sam alimpa yule bibi
laki moja, bibi alishukuru sana alibebwa kwenye
pikipiki na kupelekwa nyumbani kwake huko
mpitimbi.
Tulilala na siku inayofuata tuliondoka kwa ndege, mimj na Sam.
Kaka tulimwacha kijijini, tuliporudi dar. Sam alikwenda kuonana na baba ake alimpa mahall ya kwenda kulipa kwetu, alisafiri baba Sam mpaka Songea alilipa hiyo mahali yote na kurudi mjini ambapo maandalizi ya ndoa yalianza haraka sana.
Mimi na Sam tulienda kazini baada ya mwezi mmoja na wiki moja kupita bila kugusa ofisini kwanza tulipokelewa na katafrija kafupi cha kutufurahia tumerudi salama.
Wakati wenzetu wanapita kutupongeza kwa kutupa mkono.
Saraphina alifanya kitendo ambacho sikupendezwa nacho badala ya kumpa mkono Sam alimkumbatia kwa nguvu. Yaani unamkumbatia kwa nguvu zote mume wangu mtarajiwa, niliona ananitania Saraphina, wivu ulinivagaa nilivuta wigi lake kwa nguvu.
Minyoosho aliyosukwa vibaya na chogo lake kama matv ya zamani lilionekana vyema si akajikuta kakasirika anakuja kunivaa na mimi nilikua namsubiri kwa hamu.
Chapter 17
Tulipelekeana za makofi mfululizo, kwenye kitengo cha kupigana mbona natisha mimi, nilimchezeshea vibao vya kukata shombo na ngebe, mimi si mwanamke wa kijijini halafu yeye wa mjini hawezi kupigana eti anataka kuning’ata hapo ndo nilitaka kumnyoosha vizuri, bahati nzuri Sam alinikamata alinipeleka ofisini kwake.
na Nyuma Saraphina alikua analia kwa kwikwi. Sam aliniongelesha kwa ukali, nilimuwahi kumwomba msamaha ili hasira zipungue zilizobaki nikamkumbatia mambo sindo hayo yaani nilale kwenye kufua chake halafu aendelee kuwa na hasira hizo hasira zinakaa wapi wakati mimi ndo kiboko yake, kama mwanamke na unajua kumtuliza mumeo hebu jitikise kidogo na ujiambie mimi ndo kiboko ya babaa hehehe. heiya, nilimpelekea mdomo alinipokea, si najua anachopenda nilijidekeza hapo kwa sauti za mahaba ndo nikammaliza kabisa.
Tukatoka zetu ofisini hao kwenye gari kisha tukaenda eneo flani hivi ni maalumu kwa watu wanaopenda kuendesha farasi, nilikua siwezi kuendesha ila Sam alikua mtaalamu bhana, aliniweka mbele na yeye nyuma aliniendesha weeh, nilijisemea hivi ni mimi Thedy au naota maana mambo ambayo nilikua nafanyiwa yalikua yamepita ukomo wa kufikiria kwangu kama ipo siku na mimi nitatendewa yaani nilijuaga hayo mambo ni kwaajili ya wakorea au wachina tu.
Tulipotoka eneo hilo la farasi, tulipanda boti na
kwenda kisiwani Mbudya, huko tulichezeea maji, tulipiga picha nyingi sana. Jioni tukajirudisha wenyewe nyumbani tukiwa na furaha kama yote, kidudu mtu wa kuitwa Saraphina tulimsahau kabisa.
Tukiwa katika maongezi ya hapa na pale, Sam alipokea simu ya mtu mzito sana Mzee Kavishe, huyu ndie alikua mmiliki wa hiyo kampuni ambayo alikua anaiongoza Sam.
Makazi yake huwa nje ya nchi huko Canada, aliamini kampuni itakwenda vizuri chini ya uongozi wa Sam ndio maana ilikua inapita miaka hata miwili hajarudi nchini kwani alijua kampuni ipo mikono salama ya Sam.
Sam alipokea simu na kusalimia, mzee alipokea salamu hiyo na kujikooza kidogo. “Vipi hali ya kampuni Sam?” Mzee Kavishe aliuliza.
“Inafanya vizuri sana, tumekua tukipokea watalii wa ndani na nje ya nchi, faida ya kampuni Imeongezeka kwa asilimia ishirini na tano ukiringanisha na mwaka uliopita na ndio kwanza tupo mwezi wa kumi bado miezi miwili kwa nature ya biashara yetu mwezi wa kumi na mbili kipindi cha mapumziko tutapata watalii wengi ambao watapelekea faida yetu ikoe maradufu”
“Hongera sana kijana wangu umekua bora na Imara mara zote kwa ustawi wa kampuni yetu, sasa kuna jambo lingine wafanyakazi wamekua wakilalamika kwamba uongozi wako umepoteza ushawishi ndani yao, siwezi kuzunguka sana na kukuficha jambo hili, si unajua kwamba nilikupa nafasi kubwa sana kwenye kampuni nafasi ambayo nilimnyima mwanangu wa kumzaa?”
“Ndio mzee nakumbuka na naelewa vizuri” “Bhasi leo mtoto wangu amekua akinisumbua sana kanitumia video ya wafanyakazi wawili wakike wakipigana ofisini kwa madai ya kukugombania wewe, hivyo anaomba nimpatie nafasi ambayo uko nayo wewe, na wewe nikushushe ili aweze kurudisha nidhamu eneo la kazi unalionaje hilo?” Mzee kavishe alieleza alichokua anakimaanisha kisha alitega mtego III Sam ajichinje mwenyewe. Nilimtazama Sam usoni alionesha kufadhaishwa sana na swali hilo, nilijilaumu sana kwa kumsababishia hali hiyo kwa wivu wangu wa kijinga nilijilaumu kwa kuanzisha ugomvi ofisini.
Chapter 18
“Mzee maamuzi kamili yapo mikononi mwako, wewe ndie mwenyekiti wa kampuni, muda wowote unaweza mchagua mtendaji anaestahili kuibeba kampuni yetu, kwa upande wangu niko tayari kwa nafasi yoyote ile hata ukinipa ufagiaji wa ofisi, mimi nitaipokea bila kinyongo na kuhusu wafanyakazi kupigana nikweli wamepigana ila tuliwadhibiti na swala lao nitalifanyia kazi ili kuwarudisha kwenye hali yao ya utendaji wa kazi nazani nimetolea ufafanuzi vizuri kazi kwako mzee wangu” Sam alirudisha mpira kwa mzee kavishe afanye yeye maamuzi.
“Utabaki hapo sio kwasababu ya upendeleo ni kwaajili ya uwezo ulionao, makosa yaliyopo kwa wafanyakazi ni rahisi kuyarekebisha ila kubadili mtendaji na kusababisha hasara kubwa kwa kampuni itatuchukua miaka mingi kuifidia, siwezi kuingia kichwa kichwa kwenye huo mtego, chapa kazi kijana wangu” Mzee Kavishe aliuamini uwezo wa Sam kuliko mtoto aliomzaa.
“Ahsante mzee wangu kwa imani yako kwa mara nyingine nami nitakulipa utendaji usio na wasiwasi hata kidogo. Pia nikukaribishe kwenye harusi yangu mwezi ujao
“Oooh kumbe unaoa jambo zuri sana, nitarudi bongo kuhudhuria harusi yako kijana wangu”
“Nitafurahi sana kukuona mzee wangu” waliagana hapo na sasa nililiona tabasamu usoni kwa mume wangu mtarajiwa, nami nilifurahi nilimkumbatia na kumwomba tena msamaha kwa kile kilichotokea ofisini, alinituliza na kunambia nisijari kwani hata yeye angeona nikikumbatiwa na mwanaume mwingine kwa namna ile angeshindw kujizuia angepandwa na wivu na hasira, tulicheka kwa furaha, alinibeba na kwenda bafuni pamoja huko tuliogeshana tulipotoka huko tulipeana mambo matamu kitandani.
Mchezo ulinoga sana tulijikuta tunafanya wee, ila sisi ni warafi jamani ilipofika saa nane usiku ndipo tulilala, tulipoamka tulifanya mazoezi ya pamoja tulipata chai ndipo tukaendelea na mambo mengine, siku hiyo ilikua jumamos hivyo hakukua na kwenda kazini ilipofika mchana tuliingia kwenye gari na kwenda kwa mchungaji kanisani.
Tulimweleza juu ya matamanio yetu ya kufunga ndoa takatifu, mchungaji alitupongeza kwa hatua hiyo muhimu na kubwa sana, alituombea na kutuambia kwamba tutaanza mafundisho ya maisha ya ndoa, tulikubali na jumapili iliyofuatia ndoa yetu ilianza kutangazwa kanisani, Sam alikua na marafiki wengi sana hivyo walimchangia pesa ndefu tulipanga harusi yetu iwe ya kifahari kwa maana yawepo magari mengi sana ili kusimamisha mjini, hatimae siku ilifika.
Tulikua mbele ya madhabahu ya Mungu, nyuma yetu walikua wanadamu wengi waliopendeza, walikua na furaha ajabu, ila kwa upande wangu nilijiona nna furaha kuliko wote ila niliposikia sauti ya Saraphina akiipaza na kusikika na kila mtu ndipo nilijua kwamba mwanamke huyo alikua mbaya kuliko wanawake wote duniani, nilitamani nikamkamate nimfinye finye mpaka awe karatasi, nilibaki kumtazama kwa hasira alivyokua akitamba ndani ya ukumbi wa kanisa.
Chapter 19 & 20
“Mchungaji kwenye amri ya tisa inasema kwamba usimshuhudie jirani yako uongo, ukiitazama vizuri hiyo amri imevunjwa na bwana harusi, alinidanganya kwamba atanioa na leo amekuja kumwoa mwanamke mwingine, moyo wangu unaugulia maumivu sana, sioni raha ya kuendelea kuishi ni kheri nikafe huko ili nikamshitaki huyu jamaa kwa baba yangu. Jamani ninyi wote hapa hakuna ambae moyo wake haujawahi pitishwa kwenye upande wa upendo hebu fikiria yule mtu uliempenda kwa moyo wote, ukawakataa watu wengi kwaajili yake, ukaacha ratiba zako nyingi ili uweze kuishi nae siku zote ila anakubadilika na kuoa mwanamke mwingine.
Wazazi wa binti sijui mnajisikiaje kuona binti yenu anaolewa na mwanaume mlaghai kama Samson kama aliweza kunihadaa mimi niwaahidi muda wowote mkubali kumpokea binti yenu akiwa anatiririsha machozi ya kusalitiwa na kuachwa, hii ndoa inayotaka kufungwa leo ni batili kama nenp linasema kwamba lifungwalo duniani na mbinguni limefungwa, mimi natamka hivi hii ndoa haitokua na upendo, amani wala furaha hata mara moja, haitopata mtoto hata iende wapi, Sam wewe ni muongo, wewe ni muongoo” Saraphina alilinyamazisha kanisa kwa dakika alizokua anaongea.
Aliongea huku akivujisha machozi ya unafki huyu msichana alidhamiria kabisa kuharibu harusi yangu ambayo iliandaliwa kwa pesa nyingi yaani alitaka kuipa doa bila sababu za msingi, nilitaka kuingilia jambo hilo wakati nawaza Sam aliingilia na kuongea.
“Sikia Saraphina hata dunia ipinduke tukabaki
wawili tu duniani, sitoweza kuishi na mwanamke
mwongo na mwovu kama wewe, leo hii kanisa
litajua kwa namna gani wewe ni zaidi ya uongo
wenyewe.
Kanisa lilitulia na kumwacha Sam afanye kile ambacho alitaka kukifanya alisogea mpaka pale kwa kijana wa studio aliunganisha simu yake na kompyuta, Projector ilikua inaonesha maneno ya biblia alibadili na kuonesha video.
Kwenye video alionekana Hussein na Saraphina walivyokua wanapanga mpango wa Saraphina kuingia kwenye ndoa na Sam ili kumuibia, kumfilisi wakipata pesq wakaishi pamoja kwa pesa walizoiba, pia Saraphina alioneshwa akiongea kwa mdomo wake hampendi Sam na hajawahi tokea kumpenda kabisa. Kufika hapo nilijikuta napiga makofi watu wa kanisani nao waliungana na mimi kwenye kupiga makofi.
“Mwongo huyo, sio mimi jamani msimwamini huyo, mwongo huyooo, ameniedit jamani hiyo ni Ai Saraphina aliongea lakini hakuna aliemsikiliza awamu hii wazee wakanisa wawili walimchukua na kumtoa kanisani ili shughulia yetu iendelee kama kawaida.
“Mafuta yamejitenga na maji sasa, tunamshukuru Mungu kwani hakuchelewa kutuonesha ukweli ni upi na uongo ni upi, njia ya mwongo ni fupi sana duniani” Mchungaji aliongea maneno ambayo yalijawa na mafumbo ila yalionesha ni kitu gani alikimaanisha. Niliulizwa kama nitakua tayari kuolewa na kuambatana na bwana Samson mpaka kifo kitakavyotutenganisha, niliitikia ndio nitafanya hayo kwa msaada wa Mungu nae Samson aliulizwa akajibu sawasawa na mimi, tulivishana pete.
Watu walishangilia mmoja baada ya mwingine, tulienda mahali pazuri kupiga picha baada ya ibada kisha tulienda ukumbuni huko ndo mazawadi yalikua kama yote sherehe ilikuwa kubwa sana, watu walikula na kunywa.
Mzee kavishe alisimama na kusema kwamba anampa samson asilimia hamsini umiliki wa kampuni kutokana na utendaji wake uliotukuka kwani aliitoa kampuni chini kabisa mpaka kufikia hapo.
Kila mmoja alishangilia sana, tuliingia kwenye maisha ya ndoa huku tukiendelea kufanya kazi. Saraphina alipatwa na kichaa nazani kitendo cha kudanganya kanisani hakikumwacha salama.
Hussein nae alifukuzwa kazi kwani alikua mhasibu wa kampuni ambapo alihusika na upotevu wa millioni mia mbili za kampuni, aliishia kufungwa miaka ishirini na tisa gerezani na alitakiwa kuzilipa fedha hizo siku atakayomaliza kifungo chake kama atashindwa ataanza kutumikia kifungo upya, haikuonekana njia ya yeye kutoka gerezani tena, mwisho wa ubaya ni aibu.
Mimi na Sam wangu tulipata watoto saba si unajua tena tunaipenda michezo kwahiyo hatukuona shida kuongeza dunia kama tulivyoagizwa na Mungu wetu, kufikia hapa sina la ziada zaidi ya kukukaribisha kusoma kazi zangu zote zijazo kwani ni kazi nzuri sana. Mungu akubariki kwa kusoma mpaka hapa Mwisho.