NILIYOYAONA KWENYE CHUMBA CHA MUME WANGU TAJIRI
Mkasa Wa Kweli
Mimi ni mama wa watoto wawili. Kisa changu kinaanza miaka michache iliyopita nilipokutana na mwanaume mmoja kipindi cha uchumba wangu. Alikuwa na kila sifa ya mwanaume wa ndoto mwenye mvuto, maneno matamu, na juu ya yote, alikuwa na pesa nyingi . Sikuamini kuwa mtu kama mimi ningeweza kumpata mwanaume kama huyu.
Wakati huo huo, maisha yangu yalikuwa yanabadilika kwa kasi. Kwa bahati mbaya, mama yangu mpendwa alifariki ghafla . Ilikuwa ni siku ya huzuni sana maishani mwangu. Lakini ndani ya huzuni hiyo, mume wangu alisimama na kuniunga mkono kwa kila hali akigharamia msiba, akinituliza, akinionyesha mapenzi yasiyoelezeka. Baba yangu naye alifurahishwa sana na mwanaume huyu “mwenye uwezo” na hivyo bila pingamizi alinipa ruhusa kuolewa naye. Nilihisi kama nimepata mbadala wa upendo wa mama kupitia kwake.
Lakini kumbe…
Baada ya ndoa, mambo yalianza kubadilika. Kulikuwa na usiku nilikuwa naota ndoto za kutisha mama yangu akinililia, akinionya, nikimbie na muondoke kwenye hii ndoa lakini kila nilimwambia baba anakataa na kusema nimeshaolewa hakuna kuomba TARAKA, lakini sikuweza kuelewa maana yake. Tabia ya mume wangu pia ilianza kubadilika. Alikuwa na vyumba ambavyo alivizuia kabisa nisikaribie. Kila alipokuwa akifanya “safari za biashara,” kuna nguvu ya giza ilikuwa ikitanda nyumbani. Niliogopa, lakini nilijipa moyo.
Mpaka siku moja, nilivumbua kitu kilichonisambaratisha kabisa . Niliona chumba kimoja akiwa amelala na mavazi ya ajabu, damu ikiwa imemwagika chini, na picha ya mama yangu ikiwa kwenye meza huku ikiwa imedungwa sindano katikati. Dunia yangu ilivunjika. Nilijua hapo hapo mama yangu hakuondoka kwa kawaida. Alitolewa kafara ili mimi niwe mke wa huyu mwanaume mwenye utajiri wa kishirikina
.
Na baadaye ya tukio hilo mume wangu alirudi huku amekasilika sana baada ya siku mbili mtoto wetu mmoja akafariki na mume wangu alinilaumu mimi kwamba ndio chanzo na msiba wetu kwamba sio msikivu na muerewa nipo matatani naogopa sana.
Nililia, niliumia, nilihisi mwenye hatia. Niliishi kwenye ndoa ya hofu kwa muda, nikijifanya kupotezea kwa muda lakini sina amani hata na uzi mali tulizonazo , nikitafuta namna ya kujiokoa mimi na mtoto wangu. Hadi leo, naendelea kujitahidi kutoka kwenye minyororo ya giza aliyoninasa nayo. Ila simfahamu nianzie wapi mana alishaniambia hakuna kitu nitafanya yeye asijue?
Funzo : Sio kila anayeonekana mzuri ana moyo mzuri. Sio kila utajiri umetoka kwa Mungu. Fahamu unapoingia katika maisha ya mtu, unaingia pia kwenye ulimwengu wake wa siri. Wengine huvaa tabasamu mbele, lakini ndani yao ni mauti safi.
Mama yangu alinipenda hadi mwisho, alijitoa kwa ajili yangu. Na leo, natumia sauti hii kuonya wengine: msiangukie majaliwa ya macho na mali.
Tafuteni amani, si fedha.