Full Story

Kumbe Utajiri Wa Kaka, Ndiyo Unatumaliza

JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

SIJAAMINI KAMA UTAJIRI NA MAFANIKIO YA KAKA NDIYO YANATUMALIZA

Hadithi Ya Kweli

Mwaka 2011 kaka yetu alimfuata mdogo wetu ambaye ndiye alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yetu ๐Ÿ‘ถ.
Kipindi hicho, mdogo wetu alikuwa ameolewa mkoa mwingine, tofauti na mkoa anaoishi kaka ๐ŸŒ.

Kaka alisafiri moja kwa moja hadi kwa mdogo wetu. Cha kushangaza ๐Ÿ˜ณ, alivyo fika tu, aliomba alale naye.
Mdogo wetu alikataa kabisa โœ‹ na akaanza kuogopa hata kukaa ndani kama mume wake hayupo ๐Ÿ˜ข.
Kaka aliendelea kumshawishi sana lakini mdogo wetu alikataa kwa msimamo. Hatimaye, kaka akaondoka ๐Ÿšถโ€โ™‚๏ธ.

Baada ya kuondoka, mdogo wetu akampigia dada yetu mkubwa ๐Ÿ“ž na kumueleza yote yaliyotokea.
Dada mkubwa akatupa taarifa sisi wengine, tukashauriana na kuamua ibakie kuwa siri ya familia ๐Ÿค.

Miezi mitatu baadaye, mdogo wetu alianza kuugua ugonjwa wa ajabu sana ๐Ÿค’.
Aliteseka mno, tukampeleka hospitalini ๐Ÿฅ, tukampeleka kwenye maombi ๐Ÿ™ lakini hakukuwa na nafuu.
Baada ya mwaka mmoja wa mateso makali, mdogo wetu akafariki ๐Ÿ’” na kuwaacha watoto wawili mmoja akiwa na miaka 6 ๐Ÿ‘ฆ na mwingine miaka 3 ๐Ÿ‘ง.

Baada ya miezi 7, mama yetu naye akashikwa na ugonjwa ule ule ๐Ÿ˜”.
Tulijaribu kila njia, lakini baada ya mwaka naye alifariki ๐Ÿ•Š๏ธ.

Baada ya miezi 5, baba yetu pia akashikwa na ugonjwa ule ule ๐Ÿ˜ข.
Hapo familia nzima tukaanza kurumbana โšก, kila mtu akimnyooshea kidole mwenzie โ˜๏ธ kwamba ndiye anayehusika.
Tulikuwa tunaita waganga ๐Ÿ”ฎ ili watueleze, lakini kila mganga akimtaja mwingine. Hali ikawa vurugu na ugomvi wa kila siku ๐Ÿฅบ.
Mwaka mmoja baadaye, baba pia akafariki ๐Ÿ˜ญ.

Ilipita mwaka mmoja bila tatizo, lakini ilipofika mwaka mmoja na miezi 3, dada yetu wa tano kuzaliwa naye akashikwa na hali ile ile ๐Ÿ’”.
Aliteseka mwaka mzima na hatimaye akafariki, akiwaacha watoto wanne ๐Ÿ‘จโ€๐Ÿ‘ฉโ€๐Ÿ‘งโ€๐Ÿ‘ฆ huku mtoto wa mwisho akiwa na miezi 8 tu ๐Ÿผ.

Cha kushangaza zaidi ๐Ÿ˜จ katika vifo vyote hivyo, miili ya marehemu ilikuwa inabadilika, nyuso zao zikifanana na za sokwe ๐Ÿฆ.

Sasa, imepita miaka 10 bila kifo chochote katika familia yetu.
Mwezi wa 7 mwaka huu nilichukua uamuzi wa kutembelea ndugu zangu ๐Ÿค kwa kuwa vifo vya wazazi na dada zetu vilitufanya tutengane kwa muda mrefu.

Nilianza kwa kaka yetu mkubwa ๐Ÿ‘‘. Nilichokuta kiliniacha na maswali mengi ๐Ÿคฏ:

Ana miliki kanisa kubwa โ›ช

Amejenga majumba ๐Ÿ 

Anamiliki magari ๐Ÿš˜

Na amejenga shule, inayotarajiwa kuanza mwakani ๐Ÿซ

Awali, nilikuwa nimesikia kuwa amekuwa mchungaji, na sikutilia maanani ๐Ÿ•Š๏ธ. Lakini sasa nilivyoona hali halisi, nikabaki na maswali mengi sana hasa nikikumbuka yaliyopita ๐Ÿ˜Ÿ.

Inawezekana kweli kwamba huu ni utajiri wa Mungu ๐Ÿ™Œ, lakini moyoni naomba Mungu anisamehe ๐Ÿ˜” naona utajiri huu unahusiana kabisa na vifo vya wazazi na dada zangu ๐Ÿ’”.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba kila ninapomweleza ndugu mwingine kuhusu mashaka yangu haya, wanakuwa wakali sana ๐Ÿ˜  na hawataki kabisa nizungumzie jambo hili ๐Ÿšซ.

Naomba mawazo yenu kuhusu ili swala?

error: Content is protected !!