SIJAAMINI KAMA UTAJIRI NA MAFANIKIO YA KAKA NDIYO YANATUMALIZA
Hadithi Ya Kweli
Mwaka 2011 kaka yetu alimfuata mdogo wetu ambaye ndiye alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yetu .
Kipindi hicho, mdogo wetu alikuwa ameolewa mkoa mwingine, tofauti na mkoa anaoishi kaka .
Kaka alisafiri moja kwa moja hadi kwa mdogo wetu. Cha kushangaza , alivyo fika tu, aliomba alale naye.
Mdogo wetu alikataa kabisa na akaanza kuogopa hata kukaa ndani kama mume wake hayupo
.
Kaka aliendelea kumshawishi sana lakini mdogo wetu alikataa kwa msimamo. Hatimaye, kaka akaondoka .
Baada ya kuondoka, mdogo wetu akampigia dada yetu mkubwa na kumueleza yote yaliyotokea.
Dada mkubwa akatupa taarifa sisi wengine, tukashauriana na kuamua ibakie kuwa siri ya familia .
Miezi mitatu baadaye, mdogo wetu alianza kuugua ugonjwa wa ajabu sana .
Aliteseka mno, tukampeleka hospitalini , tukampeleka kwenye maombi
lakini hakukuwa na nafuu.
Baada ya mwaka mmoja wa mateso makali, mdogo wetu akafariki na kuwaacha watoto wawili mmoja akiwa na miaka 6
na mwingine miaka 3
.
Baada ya miezi 7, mama yetu naye akashikwa na ugonjwa ule ule .
Tulijaribu kila njia, lakini baada ya mwaka naye alifariki .
Baada ya miezi 5, baba yetu pia akashikwa na ugonjwa ule ule .
Hapo familia nzima tukaanza kurumbana , kila mtu akimnyooshea kidole mwenzie
kwamba ndiye anayehusika.
Tulikuwa tunaita waganga ili watueleze, lakini kila mganga akimtaja mwingine. Hali ikawa vurugu na ugomvi wa kila siku
.
Mwaka mmoja baadaye, baba pia akafariki .
Ilipita mwaka mmoja bila tatizo, lakini ilipofika mwaka mmoja na miezi 3, dada yetu wa tano kuzaliwa naye akashikwa na hali ile ile .
Aliteseka mwaka mzima na hatimaye akafariki, akiwaacha watoto wanne huku mtoto wa mwisho akiwa na miezi 8 tu
.
Cha kushangaza zaidi katika vifo vyote hivyo, miili ya marehemu ilikuwa inabadilika, nyuso zao zikifanana na za sokwe
.
Sasa, imepita miaka 10 bila kifo chochote katika familia yetu.
Mwezi wa 7 mwaka huu nilichukua uamuzi wa kutembelea ndugu zangu kwa kuwa vifo vya wazazi na dada zetu vilitufanya tutengane kwa muda mrefu.
Nilianza kwa kaka yetu mkubwa . Nilichokuta kiliniacha na maswali mengi
:
Ana miliki kanisa kubwa
Amejenga majumba
Anamiliki magari
Na amejenga shule, inayotarajiwa kuanza mwakani
Awali, nilikuwa nimesikia kuwa amekuwa mchungaji, na sikutilia maanani . Lakini sasa nilivyoona hali halisi, nikabaki na maswali mengi sana hasa nikikumbuka yaliyopita
.
Inawezekana kweli kwamba huu ni utajiri wa Mungu , lakini moyoni naomba Mungu anisamehe
naona utajiri huu unahusiana kabisa na vifo vya wazazi na dada zangu
.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba kila ninapomweleza ndugu mwingine kuhusu mashaka yangu haya, wanakuwa wakali sana na hawataki kabisa nizungumzie jambo hili
.
Naomba mawazo yenu kuhusu ili swala?
2 Comments
Nzuri sana
Ndugu yangu mtangulize mungu