DEREVA WA BABA
Sehemu Ya Kwanza
……. Irene ni mdada wa kishua mtoto wa Don yaan Tajiri 🤗, mtoto wa kitajir Irene ni mtoto wa kwanza kwenye familia yenye mtoto mmoja yaan amezaliwa peke yake 😜, Baba yake ni balozi na mama yake ni Doctor 🙌🏾…..
Siku ya leo Irene alikuwa nje ya uwanja wa ndege wa mwalimu julias nchini Tanzania akitokea Mexco ambako ndio alikuwa chuo kwa muda mrefu sanaa🤗 , hata baada ya kumaliza alimwambia mama yake kuwa hatokuja Tanzania Sababu hapaelewi 🙄🙄😒
..
Akaamua kuwafanyia Surprise😲 wazazi wake kwa kuja Tanzania Bila kuwapaa taarifa 😝🤗
“Waoooh pako vile vilee hii nchi yangu sijui ilikosea wapiii🙄🙄🤔??” Irene alikuwa anajisemeza mwenyewe huku anavua miwani yake akatazama juu kwenye anga🙄🙄
“finally I’m back home oooh☺☺” akatoa simu yake ilikuwa kwenye pochi akatoa Raini iliyokuwa humo akaweka laini ingine iliyokuwa inasoma Airtel🤗 ,
baada ya kuweka akawasha simu taratibu akaanza kupitia majina aliyokua humo mpaka akapa jina alilo kuwa anahitaji lilikuwa limeseviwa Bro mesha🤌 , Akaipiga ile namba iliita kwa sec tu ikapokewa kwa bashashaa yaan unaweza sema huyo mesha alikuwa anaisubiri hiyo simu 😅😅
“Oyooooo!! Irene irenee wee mwanamke wewe usinambie upo Tanzania😜😜” mesha alikuwa kachangamka sanaa akafanya Irene aachie kicheko chake cha mideko☺☺
“yaan we mesha wewe embu nifate kwanza yaan hapa nipo Airport sitaki baba wala mama wajue nataka wanione tu nyumbani 😝😝😝”
“Ohoo umeona sasa mambo yako Irene ,Unakuja kimya kimya kuna mshkaji anataka kukufungia eeh😅😅😅
“Aaah kwa Tanzania hii Broo vipii wewe hakuna mwanaume wa kunichanganya🙄 hakuna wanaume hapaa bwana embu niijie😏😏” Irene alikuwa anaongea huku akibinua midomo yaan yeye bwana Tanzania aah aliona kama uchafu au kujichosha tu hakuwahi ku date na mkaka wa hii nchi 😏😏
Hajawahi kuipenda wala kuikubali hata akawaambia wazazi wake yeye ataishi huko huko mexco na sio huku 😒😒 ,
Mesha akamwambua Irene bwana umefel mie sip Dar es salam siku ya tatu leo tupo Arusha na washkaji tumekuja ki have fun🥰🥰
Ooh irene nguvu zilimuisha hamu tena ya Surprise akawa hana 😒😒
Akamwambua mesha basi nachukua Tax mesha akamwambia hapana usichukue Tax wait hapo hapo ninampigia simu Dereva wa mzee aje kukuchukua hapo chap🤔
Irene akasema aah sitaki lazima nyumbani wajua kuwa ninaenda 😔😔 Mesha akasema Noo!! Nina mwambia aje kunichukua mie hata usiwe na shaka🙌🏾 , Hapo Iren akacheka yes mwambie aje , Mesha akaitaka simu 🙌🏾
Mesha na Irine ni watoto wa baba mkubwa na mdogo yaan baba zao mesha na irine ni ndugu wa kuzaliwa tumbo moja na wao wamekuwa karibu sanaa wamecheza wote na wanaelewana sanaaa🥰🥰 , zilipita kama dakika mbili baada ya mesha kukata simu 😒
Simu ya irine iliita tena mpigaji alikuwa Bro mesha🤔 , akaipokea haraka😛😛 mesha akasema sikia sasa we kaa hapo kuna mtu anakuja hapo sasa hivi 🤔🤔,
Iren akasema akifika utanambia akasema poa poa mesha akasema yaan Irene kesho lazima nije maamaa😅😅😅nimekukumbuka we mtu aisee nakujaa😂 Irene akasema uje unitembeze mjini sasa😒 mana wewe unavyopapenda huku aah 🙌🙌🙌
Wakati bado wanaongea mesha akasema amefika hapo embu angalia prado nyeupe amenitumia ujumbe hapa😐😐 , Irene akasema sawa huku anatoa simu sikioni kisha akaikata 😒😒
Akatoka kuelekea Parking hata hakuhangaika sana aliiiona ile gari imepark pembeni kidogo 🤥🤥
Akatembea haraka haraka mpaka akafika hapo kwenye gari akagonga kioo kwa vidole vyake mana vioo vilikuwa vimefungwa full🙌🏾,
kioo kikashushwa mmh kwanza iren akaguna baada ya kukutana na uso mwinginee hajawahi hata kuuona Dereva wa baba yake anamjua vizuri ni mtu mzima japo kaondoka miaka imekuwa mingi hajarudi😬😬 …
Kwenye gari alikuwa kijana tu japo amekaa kwenye siti haikumnyima urefu wake na mapana kwenye kifua kuonekana vizuri🙄, alikuwa amevaa kofia zile wanaita vijana Cap 🧢 nyeusi furana nyeusi ilikuwa imemshika mikono yake na kusababisha misuri itune haswa Jifua lake mapana 60 likafanya Fulana izidi kupendeza 👌👌
Baada tu ya kufungua kioo akamtazama irene na kufunga mida huo huo hakusubiri neno 🤥, irene akagonga tenaa ,Kioo kikashushwa ,Dereva mpya akamtazama irene kuanzia juu mpaka chinii kwa dharau akamwambia we malaya vipii embu katafute bwana huko mbele oyaa sivutiwi na wewe kuwa hapa embu potea😏🙄
Irene akasema whaaaat 😳😳😳we kaka kichaa?? Kikafungwa tenaa ,Irene alikuwa tayar anatetemeka kwa hasira et mi malayaa haha😁😁 alikuwa anacheka cheko la uchungu akachuku simu yake mikono inatetemeka😢😢🤨
anajisemea tu kwa kurudia maneno ya huyo Dereva mpya et mi malaya havutiwi na mimi hahah Seriously🤨🤨???
Simu ikapokelewa akaongea kwa jazba Sikia bro unauhakika ni hii gariii?? Akamtajia plate number🤔🤔 ,Mesha akasema Yes ndio enyewe gari ya mzee hiyo Irene akamwambia ongea na huyo mjinga ananiita mie malayaa🥺🥺🥺??
SEHEMU YA PILI
Mesha akasema ooh mungu wangu jamani jamani sikumwambia kama anakuja kumchukua mwanamke alijua mie yaan nimesahau kabisa ngoja nimpigie🙄🙄
Irene akasonya msonyo wa nguvuuu yaan alikuwa na hasira hakujali swala la kuambiwa et yeye havitii aah lilikuwa linamuuma mnooo 🤨🤨🙆
Hazikupita hata sec mbili mlango ukafunguliwa wa gari 😒😒
Dereva akasema Sorry madam sikujua kama ni wewe sikupewa taarifa zako😬🤥, uso ulikuwa umemshuka hatari
Irene hata hakumjibu akaingia ndani ya gari kimyaa kabisa🤨🤨 …
Wakafika mpaka nyumbani mama yake na irene ndio alikua nyumbani muda huo na hakuwa na Taarifa za kuja kwa bint yao😒😒 alipo muona manusura avunje mguu kwa kumkimbilia ile furaha ya kuonana na mama yake akajikuta anasahau kabisa zile mambo alizosemwa na Dereva wake😅😅😅…
Nyumba ilichamgamka gafla kila mtu alikuwa na raha🥰🥰🥰 baba yake akamwambia irene mie umekuta nina safar ya kwenda Airport hapa naelekea Kenya kuna mkutano nitarudi kesho kutwa tutakuwa wotee😊😊, iren vile alikuwa amemkumbuka baba yake na hata lisa halijafika tangu amefika baba ake anaondoka akamwambia twende wote nikusindize mpaka Airport mie nitarudi 🤗🤗
Wakaingia ndani ya gari , baba yake akamwambia Irene huyu ni Dereva wetu mpya kwako😃 ila kwetu sio mpya ni mtoto wa mzee Boza Anaitwa Yaksun 😃😃,, Iren akasema ooh okay 🙄
Alikubali huku akivuta kumbu kumbu za zee Boza ndio alikuwa Dereva wa baba yake miaka mingi tangu anakuwa anajielewa mara zote huyo ndio alikuwa dereva wao huyu ndio kwanza kamuona leo hapa😒😒
Baba yake akamwambua Yaksun huyu bint yangu anaitwa Irene na fikiri ulishamsikia sana ndo huyu bwana 😅😅,Yuksun akasema nashukuru kukufaham,😒😒 huku akimtazama kwa kuiba iba alikuwa anaona aibu kwa jinsi alivyopishana na mtoto wa boss wake bado hilo swala na yeye lilikuwa kichwani 😆😆 ….
Baba iren akaendeleza story na bint yake wakati gari inaondoka tayari akamwambia mzee Boza anaumwa sana hali yake sio nzuri nikaona kuliko kutafuta Dereva huko mtaani bora nimchukue mwanae mana familia yao naijua vizuri na tumekuwa kama ndugu sasa🙌🏾, irene akasikitika sana baada ya kujua yule mzee ni mgonjwa☹☹ …
Baada ya kumuacha baba yake pale Airport irene alimuomba Yaksun ampeleke kwenda kumuona mzee Boza🤔 , Yaksun yeye alikuwa kimya muda wote anafata tu amri anayopewa 😒
Wakafika mpaka nyumbani kwao yaksun , mzee Boza alipo muona tu Irene alimjua japo ni muda mrefu sana hajamuona 😟😟,
Irene alimsalimia mzee boza akatoka kwenda kuongea na mke wa mzee boza yaan mama yale Yaksun🙌🏾 ,alikaa huko lisaa zima ,Yaksun yeye alikuwa bize na habar zake tu
Baada ya kumaliza ndo akamwambia tuondoke ,njian kila mtu alikuwa anataka kumsemesha mwenzie lakini pa kuanzia palikuwa hakuna😆 Yaksun alitamani kumwambia mtoto wa Boss samahani kwa ule muda alivyomkosea adabu 😅😅😅
Lakini Irene kuambiwa et havutii aah hili lilikuwa tusi linalomtesa😪😪 alitamani kumwambia we kaka embu badili kauli yako🙌🏾 akifikilia sana anaishia kusonya tu mana wanaume wa Tanzania wote anawaona kama wajinga😒 sasa kwanini anaumiza kichwa akapotezea huku akisonya tena kwa sauti kweli kweliii😏😏
Yaksun akajishtukia kwa upole akamwambia aah madam samahani kwa kile kilichotokea pale naomba tu uniwie radhi😔😔😔 Yaksun aliongea kwa upole kweli kweliii na ndivyo anaonekana muda wote anauso wa upole sanaa mkaka wa watu hana hata shida 😟😟
Irene akapata kichwa waah 🤗🤗 kwa nyodo akasema Never mind🤨,Afu akageuka pembeni huku anacheka kwa kuibia ibia yaan akaona kamkomeshaa 😅😅…..
Usiku irene alikuwa anachart na mesha kwa sms, mesha akamwmabia Kesho nakuja kwahiyo kiwanja wapii tukafurahii🥰🥰. , mesha ni mtu wa kujirusha kwa sana ku have fun😜, muda wote yeye anawaza bata alishamaliza chuo akitaka kazi hata muda huu anapata lakini anamalizia kwanza ujana wake ndio aanze majukumu kwao pesa ipo sana tu🤗🤗
Irene akamwambua nakusikiliz wewe bwan😊 , huku anacheka kwa emoj akamwambia basi fresh mie sintakuja hapo Nyumbani😇 nitakwambia uje sehem afu nina bonge wa Surprise yako🤗🙌🏾
🤗🤗 irene akamwmabia olee wakooo Mesha 😄😄 …
Asubuhi irene alimfata Yaksun baada ya mesha kumwambia watakutan waPi na muda gani 🤔🤔,
Akatoka kavaa ki pensi kifupii na bode yake imekaa haswa irene ni mrembo mnoo mnoo akamuita Yaksun kwa dharau oyaa we kaka 😒,Yaksun alikuwa ndio anafika kutoka kuosha gari 😟😟, akashuka akawa kasimama mbele ya mlango anamsikiliza Irene 🤔🤔
Irene kwa dharau akamwambia sikia wee sa mbili kuna sehem naenda okay so fanya mizunguko yako yotee by sa mbilii uwe hapa sawaa🤔!!
Yaksun akamjibu haina shida madam , neno madam likamkera irene na vile kama alikuwa bado ana hasira na Yaksun 🤨 ,heey naitwa irene Not madam okay??😏
Yaksun akajisemea moyoni makubwa 🤔, Usoni akatabasam tu akasema saw Irene😒 ,Tabasam la Yaksun unaeweza sema ni mtu mweye dharau kiburi na majivuno lakini anapendeza sana 🥰🥰
Irene akaenda mpaka chumbani kwake mbele ya kioo chake akawa anajitazama huku anaongea mwenyewe☹ , yaani mimi simvutii😒😒?? Hahah yaan mimi hakuna mwanaume ambae ananitazama tu asimeze mate et sivutiiwi na wewe mfyuu😏😏 ” akasonya huku anajitupia kitandani akavuta simu yake akawasha data 🤥🤥🙌🏾….
SEHEMU YA TATU
Wakati anawasha data Irene akakumbuka neno malaya 🙄, Akaweka kwanza simu pembeni akasogea karibu na kioo chake akajitazama 🤨,et naonekana kama malaya?? Mfyuu 😏😏
Akasonya akarudi kitandani akajitumia mgongo chini akitazama juu akavuta simu yake kabla hajafanya chochote tena akaitwa kwa ajili ya kufungua kinywa ikabidi aitelekeze simu yake atoke kwenda kula sebleni 😌….
Wakati wa chakula irene akamuaga mama yake kuwa usiku anatoka na kaka yake mesha😊 ,zaidi ya kuwa makini hakuna neno lingine alitoa mama yake sana alimuasa tu awe makini huko 🤗🤗🤗,
Sa moja kamili irene alikuwa mbele ya kioo chake kawaka hatari👌mtoto shape ,rangi mashaallah mguu wa bia 🥰 Sura nayo amejaaliwa , alikuwa kava kinguo kinaachia karibu mwili wote nje na hayo ndio mavazi yake haswa 👌👌 ukiangalia kwa kutulia unaweza ona hata ki tako kwa mbalii kinabembea mashaallah 🥰🥰🥰😅
huyo ndo irene mtoto wa kishua kweli maisha yake kama wa mbele🙌🏾 , alikuwa kashasahau kama miadi ya Yaksun ilikuwa ni sa mbili usiku na sio sa moja 😬
“Yes !! Unaweza sema mtoto wa kimbeleee waooh 😅afu kuna lijitu et linasema hata hunivutii mfyu😏😏 ” irene aliongea kwa kugezea sauti ya Yaksun huku anaweka kidole puani 😏😏🤨
Baada ya kujiona yupo kamili kila idara akachukua pesa akatia ndani ya Pochi , simu yake ilikuwa inaita sanaa 🙌🏾😬,mesha alikuwa akimpigia hakupokea kwanza alitaka kupokea akisha toka🤥
“Oooh mungu wanguu mamaaa kwanini huyu dereva ametoka ,hayupo yeyee wala gari aah😏” irene baada ya kutoka nje akakuta Yaksun hayupo na gari alio kuwa anategemea kutoka nayo pia haipo,Akaingia ndani analalamika huku anaigonga miguu yake chini kwa hasira 😪😪🤨
” Alitoka akasema hachelewi kurudi kuna mahala ameenda binafsi😒 “
“Anakiburii! Naomba namba yake😏😏”
Irene akachukua namba ya Yaksun kwenye simu ya mama yake akaipiga iliita kidogo ikapokelewa 🙌🏾
“Kwahiyo hao wanawake zako wanaovutia ndio wanakuvutia sanaaaa mpaka unasahau kazi siooo🤨🤨??” Irene aliuliza moja kwa moja kwa shari bila hata kujitambulisha , Yaksun aliijua sauti vyema sana 🙄
“Kwani naongea na nanii” Akauliza bila hata papara sauti ilikuwa imepoa sana kama mtu ambae yupo sehemu iliyo tulia 🤥
Irene akacheka kwa dhihaka afu akasonya , kusonya ni kama siraha yake au ni kama bint alielelewa kiswahili sanaa😒😒🙌🏾 ,
Yaksun akauliza tena naongea na nani kama hautajisikia kujitambulisha naomba ukate simu yako dada🤔., Yaksun alikata simu baada tu ya kumaliza kuongea hakusubiri tena mpigaji ndie akate simu
“Haaa!!! Kanikatia simu haa😟😟!!! Heheh et anakazi nyingii kwahiyo mie kazi yangu ya ziada mungu wanguu🙆!!!” Irene alitoka kwa hasira mpaka alipo mama yake
“Mamaaa hivi huyu kijana mmeleajee mbona anadharau sana 🤨🤨”
“Irene wangu ni yule yule kipenzi hasira hata hazijakuisha haya njoo hapa kipenzi uniambie amekufanyaje njoo😊😊”
mama ake akamkumbatia anajua udhaifu wa mwanae tangu mdogo ni mtu mweye hasira za haraka mwepesi ku panic sana 🤌
Irene akamuelezea mama yake kuwa alishamwambia Yaksun kuwa jioni kuma sehemu ampeleke lakini mpaka sasa ndo hivyo hayupo halafu anampigia simu anamkatia bila hata kusema neno🤨🤨…
Mama irene akachukua simu yake akampigia Yaksun🙌🏾, Yaksun yeye alikuwa nyumbani kwa wazazi wake😒😒 ,alipoona tu simu ya mama irene akajua kumekucha akatazama saa yake iliyokuwa mkononi hakuwa na presha baada ya kuona ndio kwanza sa moja na dakika 12 , mwendo wa kutoka kwao mpaka nyumbani kwa boss wake ni mchache anafika 😒🙌🏾
Akaipokea ile simu kwa heshima ,baada ya salamu mama iren akamuuliza upo wapi akajibu nipo nyumbani mama akamwambia njoo irene kuna sehem anataka umpeleje , Yaksun akajibu sawa mama nakuja 😔🙌🏾…
Iren akaona kama wanamuendekeza yaaan kwa jinsi mama yake alivyoongea nae kwa upendo hakulidhika kabisaa moyo wake ulikuwa una duki duku🥺🥺 akatamani kumwambia kuhusu kumuita malaya🙌🏾 ,akasahau kama aliombwa msamaha roho ya chuki inamsimama wimaaa 🤨
Akajisema yaan nitakukomesha wewe Yaksun walai subiri sasa🤨🤨🙌🏾, akainuka pale kwa mama yake akatoka nje kabisa ya geti kumsubiri Yaksun 🤨
Akaliona gari linakuja taratibu 😡😡😡 hasira zikampanda hakusubiri hata gari imsogelee yeye akaifata hukoo 🤨🤨 “yaan kunichelewesha kote kulee unakuja kama vile umebeba maharusi we mbona kiburi sanaaa😏??” Irene aliongea kwa kufoka
Yaksun akamtazamaa 🤔 akamwambia Madam sorry 🙏 “
,”hee madam madam madam how many time when I tell you I don’t want you to call me madam,, ooh mungu wangu sijui hata kama English unajua ,SI.TA.KIII U.NII.TE.hivyooo🤌😒 aah” akafungua mlango wa gari Akaingia kwa hasira Yaksun akasema “Sorry” irene hakujibu kitu alibaki kimyaa ila ndo kavuta mdomo kama samaki chuchunge🤣🤣
Yaksun alikuwa anamuangalia Irene kupitia kioo cha mbele vile amevuta midomo😅😅 yeye anacheka tu moyoni ashamjua huyu bint anakosoro zake huyu😅😅🙌🏾 ,
sema ndo mtoto wa boss hakuna njia ingine🤣. Irene kwa bahati mbaya alitazama kioo cha mbele kwa dereva akagongana macho na Yaksun🤭🤭 ,macho ya Yaksun yalikuwa yametulia yanamtazama meupee mashaallah kaka anamacho mazuri 🥰🥰🥰 kwa mwanamke mwenye hisia zako lazima uanze kuvutiwa na macho ya huyu kaka kabla hujaona jifua lake lilivyojitengeneza vizuri kwenye Tishirt zake🥰🥰😋
Irene akashindwa hata kushusha macho wala kukwepesha😊 , Yaksun taratibu akapeleka macho yake mbele kuendelea na kazi yake 🙌🏾,
Hakuwa amepanga irene alijikuta tu baada ya kukutanisha macho na Yaksun moyo wale ulidunda lakini alijua tu Yaksun tayar kamtamani au kavutiwa na yeye kwa jinsi alivyoubwa vizuri🤭😋 ,uzuri wake Irene ndio malingo yake yalipo
“Sa kwanini ananitazama hivyo ,mfyuu si alisema mie sivutii huyo😒 aende huko kwanza sio hadhi yangu😏 “
SEHEMU YA NNE
Mawazo ya Irene yakaenda kuwa Yaksun tayar amemtamani ndo mana anamtazama hayo macho ya umakini na kumkagua🤣🤣 , Yaksun hakuwa huko kabisa alikuwa anamsikitikia ni mschana mwenye papara sana japo kamjua kwa haya masaa kadhaa tangu akutane nae🙌🏾 ….
Baada ya kushuka alipo hitaji kufikishwa🤨 , Ametembea kidogo kuingia ndani ya Club ambayo ndio ilikuwa akutane na Mesha 😌😌,
Yaksun akamuita kwa nyuma huku anakuja kwa mwendo wa haraka haraka☹
Irene akatabasam akajisemea mshenzi huyuu kwahiyo uvumilivu umemshinda 😁😁😁 ngoja nimchambee si alisema mie sivutii hahah aloo😏😏
Yaksun akawa tayar kamfikia akasema aah ma….hapana si…..” kabla hajaongea alichokifata irene akamwambia embu we kaka sikia nikuambie usijisumbue sawa😏, yaani mimi na wewe ni vitu viwili tofaut kabisaaa yaan kabisaa hatuendani so Goo!!”
🙄🙄Yaksun akabaki ametoa macho anamshangaa Irene huyoo akaishia ndani 🙌🏾, aliguna tu akageuza kurudi huku akiitazama simu iliyokuwa mkononi kwake🙄🙄 ,
Ilikuwa simu ya Irene aliisahau kwenye gari na zile haraka haraka zake na ndio Yaksun alimfata haraka kumpa baada ya kuiona ☹☹
Akaingia ndani ya gari kwanza akaanza kucheka yaan anakumbuka maneno ya Irene akajikuta kicheko kinaongezema 🤣🤣🤣”et alikuwa mexco 😅😅Au alikuwa Buza huyu Demu mswahili kama ninii aah🙌🏾” Yaksun akaupiga usukani huku anaitazama simu ya irene pembeni ya siti alikuwa ameiweka🤔🤔 ,akawa anajiuliza aende au asubiri mpaka irene atakapo gundua kuwa hana simu yake aaah alijikuta anapiga tena ngumi kwenye usukani wake 🤥
Kibarua kimekuwa kigumu tangu amekuja irene🤔🤔alifanya tu maamuzi ya kuweka kichwa juu ya usukani wake asubiri hapo😬😬🥺 …
Irene kafika hadi ndani hamuona mesha watu wengi, akaamua kuchukua simu yake ili ampigie mesha ,Anafungua pochi haipo Simu 😒😒”Ooooooooh munguuu” akajikuta analalamika kwa sauti ya juu huku anashika paji lake la usooo “aaaah jamaniiiii aaah” mwili ukamuisha nguvuu aibuu ikamvaaa
Pembeni kulikuw na kochi akajitupia hapo hana hamu hata 😒😒
Sec hiyo hiyo akamuona mesha anaelekea upande wa kaunta kwa mbali😬, akainuka haraka haraka akamfata mesha “Hee!!😳 mbona umekuja kimyaa”
“Sikia Broo embu naomba unisaidie jamani nisaidie☹🙌🏾”
Mesha ikabidi atoe utani wake baada ya kumuona Irene kama hana mood fresh 🤔🤔
Akamwambia eenhee haya nambie kuna ninii
Irene akamwambia kaka naomba umpigie simu Yule Dereva wa baba nimeacha simu yangu ndani ya gari mule 🙌🏾” mesha akasema sawa njoo huku nyuma sasa tutoke kwenye kelele 😌
Mesha alimtoa nje ambapo sauti za muziki hazifiki kwa sana akachukua simu yake akampigia Yaksun😒 , Haikuchukua hata muda mrefu ikapokelewa ,Mesha akamwambia Sister ameacha hapo simu yake Kakaa sijui tunafanyaje😒😒??”
Yaksun akasema mie bado nipo hapa hapa mwambie aijie huku parking nimeiona ndio sababu sijaondoka bado🤔🤔 ….
Mesha akaikata simu akamwambia haya ifate yupo parking hapo nje😌 “
Irene akasema, mimi ndo nifate 🙄🙄🙄kaka nifatieeee!!😔😔😔
Irene ilibidi ambembeleze Mesha kuifata simu kila akiwaza yale matambo alomtambia Yaksun 😅😅😅😅🤣 uso unamjaa hayaa anaona Aibuu moyoni anajisemea kumbe alikuwa ananiletea simu yangu aaaah😩😩😩😩 Mesha akamwambia Washkaji kule nitawaweka sana afu sio vizuri fata mie utanikuta ndani we njoo juu sie tupo
Duu😔😔😔😔Irene akasema sawa ,Kumwambia kaka yake anaona aibu , akajivuta taratibu ule mwendo wake wa ki twinga hakuwa na mood nao tena alikuwa anatembea utadhan wajapani🤣🤣mikono mbele hatua za hapa na hapa akaiona gari iyo ipo parking akasimama kuitazama kwa zaidi ya dakika nne😆😆,
Simu ya Yaksun ikaingia msg taratibu akainua kichwa chake kutazama simu bahat mbaya macho yake yakatazama upande wa kushoto wa gari 🤣🤣🤣akajikuta anacheka baada ya kumuona Irene amesimama kwa mbali kidogo yaan usimamaji wake tu.unaonesha hajiamini kabisa 🙌🏾🙌🏾
Akachukua simu ya irene hata kusoma ujumbe wake alighairi , akafungua mlango kumfata ,Irene alikuwa mdogooo kama pilitoni 😅😅 Afanye yeye ujinga aibu aone Yaksun🤔😆😆😆 ,mana alikuwa anamfata huku anakumbuka zile zarau zake🙌🏾
Alifika akamnyooshea tu simu afu akageuka kuondoka zake hakuna aliemsemesha mwezie🤔🤔 , Iren alichapua haraka haraka kurudi kule aliko elekezwa na Mesha kumkuta ☹☹
Anafika kwanza alipigwa na mshangao ile surprise aliambiwa na mesha hakika ilikuwa zaidi ya Surprise 😲 walikuw ndani ya chumba private walikuwa watu watatu tu na Irene akawa wa nne wanawake wawili na wanaume wawili
Kilichomuacha mdomo wazi irene kumuona mbele yake mkaka wa ki mexco mbele yake wakati yeye alimuacha huko mexco 🙌🏾
SEHEMU YA TANO
“Lawrence???😲😲😲😲 Irene alimuita huku anamfata kwa kasi manusura hata aanguke kila mtu alikuwa anacheka
“Sio vizuri Lawrence aaah sijapendaaaa😔😔😔😔” hapo irene alikuwa anatoa lawama kwa lugha ya kingeleza huku miguu yake anaigonga chini ,sauti kaiachia ya kudeka kabisa
“Nilitaka kukufanyia surprise irene”
“Ooo’😇😇😇 Lawrence ni mtoto wa mfanya biashara mkubwa sana Mexco familia yao ni maarufu na yenye pesa sanaa , Na ndio mpenzi wa Iren kwa miaka yote ambayo yupo mexco katika vitu ambavyo vilimfanya asirudi nyumbani moja ni hii mpenzi wake Lawrence ndio alimpa uzito kuondoka mexco 🙌🏾
Katika mipango yao ilikuwa baada ya kumaliza Masomo Lawrence aje nyumbani kwao na Irene kujulikana Rasm ,🥰 lakini Lawrence akawa na kona nyingiiiii 🤌, hata kuondoka Mexco kwa Irene aliondoka kwa hasira baada ya kuona mambo yake na mpenzi wake yanakwenda kombo☹ 🙌🏾
Kitendo cha kumkuta hapa hakuweza kuamini anampenda mno huyu kaka yaan wanapendana haswaa🫠🫠🫠 👌
Lawrence akamwambia niliongea na kaka ako anipokee baada ya wewe kuondoka kwa hasira nashukuru alinikubalia😘😘
Wanajibusu kila sehem ya mwili 🤗😊🥰
“Ooh jamani basi inatosha hayaa tuenjoy” mesha ndo aliwakatisha mana kunako endea alimuona kabisa dada ake alishabadilisha macho🤣🤣
Wakati mesha anawakatisha mambo yao🙌🏾. Mlango ukafunguliwa tena wakaingia wakaka watatu na mdada mwingine mesha akasema oyaaa wanangu karibuni embu Dj achia vitu sasaaa 🙌🏾🙌🏾” muda huo huo akaingia mdada muhudumu pisi ya kwenda wale wakaka walio ingia marafiki zake na mesha wote wakaanza kukonyezana 😉😉😊
Mesha akawaoma “ongea nae tu msela kila kitu helaaa” mmmh ikabidi wote wacheke mana mesha ni kama aliwasuta ile kuongea kwa sauti 😅😅😆
Mdada alikuwa mzuri mnoo unaweza sema labda ameenda Uturuki kurekebisha baadhi ya sehem zake za mwili, japo irene alikuwa mzuri mnoo🥰🥰🥰 lakini hapa alitulia kidogoo mdada kashona ukiw mwanaume haswaaa huwezi kumuangalia mara moja tu afu et uendele na kazi zako aah🙌🏾 wee🤗🤗 hata kama ukiwa sio Rizk yaan jogoo wako mtungi hapandi lazima ulaani kwanini haupandi mtungiii lazimaa 🤣🤣🤣🤣
Nyie kuna watu mungu kawaumba afu unasema huyu mdada mbona mzurii jamani 😋😋anaweza kupata mwanaume yeyote anaemtaka yeyoteee👌 akamuoa tena kwa kumnyenyekea lakini yeye yupo huku anazungusha pombe kali na kuchezesha makalio kwenye ma club 🥺🥺
Haya bwana kila mtu na maisha yake aliyozoea au tusema mungu ndio anapanga kila mtu amuweke kwenye nafasi gani??🤔🤔 mie sijui bwana kama kila mtu anachangua njia yake ama vipii🤣🤣🤣 ila huyu dada muhudumu ni mzuri mnoo huyo mesha mwenyewe alijuta kuja na dem wake hapo 😅😅😅😆…
Walikuwa kwenye chumba ambacho ni club ndoto huko wanaita private🙌🏾 hakun watu baki mnakodi sehem yenu tu kuna kunywa huko kucheza mziki pool table😉😉, mkihitaji wanawake wa kuwaburudisha wanakuja kucheza kamali yaan kila kutu mnakipata mkiwa nyie bila usumbufu wa walevi wengine .🙌🏾😆….
“Dada samahani unaitwa nanii😉😉??” mkaka mmoja alijitoa muhanga kumuuliza huyo dadaa aliekuwa anawahudumia vinywaji 😬
“Mynda” huyo dada akajibu huku anacheka cheka ndo kabisaa wanaume nyoka wakatema mate kwenye suruali zao🤣🤣🤣🤣ila wanaume aliewaroga 🙌🙌🙌🙌
“My GAaad! Vipi naweza pata kampani yako😋😋”
“Aaah mzee Robi nini sasa mie si ndio nimemtaka lakini we vipii🥺🥺??” Ilitokea taharuki gafla baada ya yule alieuliza jina na ndie alieonesha nia ya kumtaka huyo dada tangu mwanzo alipo muona tu😒 , ajabu mwenzie alie ingia nae na ndio alimwambia anamtaka huyo mdada yeye ndio akadakia kumuomba kampani 😅😅
“Embu acha zako Morgan bwana we si uweke dau ” Robby🤔😋 akamjibu mwenzie kwa dhaarau na vile pombe zilikuwa tayar zimepanda
Morgani akamkwida shingo , mesha akainuka haraka kwenda kuwaamulia 🙌🏾, muda wote huo Lawrence na irene hawakuwa hata na habar na ule ungomvi wao walikuwa kwenye sofa kubwa kwenye kona kabisa ya Eneo ndo walikaa wawili tu walikuwa wamemisiana🤗 japo ni siku mbili tu wameachana walikuwa bize kushikana shikana kila mahala pa miili yao 🥰😋
Ugomvi ndio uliwatoa kwenye hiyo mood , Lawrence akamwambia Irene tuwahame tukatafute eneo letu tutakalo kuwa wawil tu🥰🥰 , irene nae akaona bora hivyo mana kitendo cha Lawrence kuja Tanzania na hajawahi kukanyaga aliamini kabisa anapendwa sanaaa🤌 ..
Wakati wanataka kutoka Mesha akawaona akawawahi haraka ili wasitoka akaongea na Irene hapo wamekuja kufurahi sasa kwanini wasaambaane hiyo ni dharula tu kila kitu kitakuwa sawa 😒😒, ikabidi warudi kukaa baada ya mesha kuwasihi sana , Mynda kama alivyojitambulisha yeye baad ya watu kutunishiana kifua akatoka zake chap 😅😅watajua wenyewe 🙌🏾
Amani ikarudi tena mule ndani 😒, kila mtu akapata vibe tena wakaliamsha😅😅 , Robby akainuka anatoka nje morgan akamuuliz eeh kwahiyo unaenda kuongea na Mynda 🤨🤨?? Robby akacheka akasema aah wapi mie nishamtema wa nini sasa 🙄🙄
Robby alienda kweli mpaka kwa mynda ili kuongea nae kama vipi wautumie ule usiku wote😆 ,wakaelewana kabisa akamwambia akianza kutoka atamuita sehem,Robby akarudi zake mwepes furaha yotee 😅😅😅 , Morgan roho hata haikumpa akatoka na yeye mpaka kwa mynda kuongea nae 🙌🏾
Inaendelea…………………..