UTAFAHAMU TABIA HALISI ZA MWANAUME KUPITIA MAMBO YAFUATAYO!
Kupitia safari,utajua ni tabia gani mwanaume husika anazo kupitia ulaji wake(vitu anavyopendelea kula),kujiheshimu kwake kwa watu asiowajua, kuzungumza na watu asiowajua na namna ambavyo anastahimili mazingira mapya ya ugenini! Kuna wanaume hawawezi kuishi vizuri ugenini, watakuaibisha tu!
2. Uhusishe masuala ya Pesa.
Mwanaume utajua tabia yake halisi kama ni mchoyo au bahili, kama ana roho nzuri au mbaya, kama anajua kutunza pesa au kutumia vibaya pale tu ambapo utahusisha masuala ya pesa.
3. Utakapomuona akiwa mwenye Hasira.
Akiwa mwenye hasira,utajua kama anaweza kujiongoza mwenyewe na sio kuongozwa na hisia zake! Wanaume ambao wanaua,wanajeruhi wake, marafiki au ndugu zao ni wale ambao wanaongozwa na HISIA.
4. Utakapomuona akiwa amelewa.
POMBE inamfanya ashindwe kuficha Siri zake, atakwambia yote akiwa amelewa!
5. Uishi pamoja naye kwenye nyumba moja.
Ukiishi na mwanaume kwenye nyumba yake utajua tabia zake zote!
6. Utakapomwambia “HAPANA”.
Ukimwambia mwanaume hapana kwenye kitu anachokihitaji. Hapo ndipo utakapojua tabia zake halisia ambazo anakuficha!
7. Hawezi kulala na wewe(Mwanamke) wakati wowote ambao anataka yeye.
Kama ni mwanamke, ukimnyima mwanaume tendo la Ndoa, hapo ndipo atakuonyesha tabia zake halisia ambazo amekuficha!
8. Umshuhudie baada ya kupata “HASARA”.
Mwanaume akiwa amepata hasara( amefiwa na mtu anayempenda au kumtegemea kweye maisha yake, Biashara yake imefilisika yaani amepata hasara) utajua tabia zake halisia lazima zijidhihirishe wazi wazi!
9. Umshuhudie akiwa hana pesa au Amefilisika.
Tabia ambazo anazionyesha mwanaume akiwa hana pesa au mwenye pesa nyingi,mara nyingi hizo ndizo tabia zake halisia! Sio za kuigiza.
10. Umshuhudie namna ambavyo anaishi na Familia yake, marafiki zake au watu asiowafahamu(strangers)!
Je, unafikiri mambo hayo kumi hapo juu,yanatosha kuwafahamu WANAUME? NITAJIBU NA KUSOMA KOMENTI ZOTE.