KWANINI KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NA WANAWAKE AU WANAUME WENGI SANA SIO SIFA YA KUJIVUNIA
1. Utawarithisha watoto na ndugu zako umasikini.
Wazazi na walezi wenye akili wanatumia pesa zao kuwekeza kwenye ardhi,nyumba na biashara ambazo zitawafanya waishi vizuri uzeeni lakini pia warithishe watoto wao. Lakini wewe, kutumia pesa zako gesti na kwenye viwanja mbalimbali vya starehe na wanaume au wanawake wa kila aina vitakufanya kufilisika kiuchumi na kukosa urithi mzuri kwa watoto wako.
2. Utawarithisha watoto wako na ndugu zako kutokujiamini.
Kutembea na wanawake au wanaume wengi sana ni moja ya dalili ya mtu asiyejimini na asiye na msimamo. Hivyo basi, ulivyo na tabia yako mbaya, kuna uwezekano mkubwa wa watoto wako kurithi tabia hizo kwasababu wanajifunza kwa kuona matendo ya wazazi na walezi wao kwa asilimia kubwa sana katika utoto na ujana wao. Vivyo, kuna ndugu pia wanaweza kuiga maovu yako kama ambavyo inawezekana wewe ulirithi kutoka kwa wazazi au ndugu zenu!
3. Utawarithisha watoto wako magonjwa ya ngono!
Wapo watoto wenye virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine ya ngono ambayo walipata magonjwa hayo kupitia wazazi wao kwa kuzaliwa. Hivyo basi, angalia usiwe mmoja wa wazazi wa aina hiyo!
4. Utawarithisha watoto wako na ndugu zako SIFA mbaya!
Watoto wako watanyoshewa vidole kwa kuitwa kuwa ni watoto wa nje ya ndoa. Watoto wako na ndugu zako watanyoshewa vidole iwapo utafumaniwa na mke au mume wa mtu. Watoto wako wanaweza kuwindwa kulipizwa kisasi kwa wewe kukataa ujauzito wa mtoto wa mtu mwingine au kumpatia ujauzito mwanafunzi. Rafiki, mchuma janga hula na wa kwao. KUWA MAKINI SANA KWA KUACHANA NA TABIA HIZO USIWAPATIE NDUGU ZAKO MATATIZO.
5. Utawarithisha watoto wako na ndugu zako vita ya kugombania MALI pamoja na uadui wa kudumu.
Watoto wako wa huko mtaani uliowatelekeza pamoja na wanawake wa huko mtaani wanasubili ufe waanzishe vurugu ya kudai mali zako. Kuwa makini rafiki usimuachie mke wako na watoto wako matatizo, kama inawezekana kabla ya kifo chako gawa mali zako vizuri na weka mambo sawa upumzike kwa amani.