MKE WANGU NUSU MTU, NUSU JINI
EPISODE 17 & 18
ILIPOISHIA.
“Umezima taa Munil?” nilimuuliza kwa mshtuko mkubwa maana ilipo swichi ya taa na kitandani tulipokuwepo sisi ni mbali, ni lazima mtu atoke kabisa kitandani kuifuata swichi.
“Nimezima mimi ndiyo.”
“Umezimaje?”
“Nilikwenda.”
“Siyo kweli, Munil usinifanye mimi ni mtoto mdogo aisee.”
SASA ENDELEA
“Khaaa! Sasa nikudanganyie nini jamani?”
“Umenidanganya Munil kwa sababu hujatoka kitandani na taa iko mbali lakini unadai umeizima kwa kutoka!”
“Ee, siyo kwamba nilitoka mzima, nilisogea pale mwisho wa kitanda ndipo nikapeleka mkono na kuzima swichi.
Kwa maelezo hayo ya Munil nilizidi kumshangaa na kumwogopa kwani hata ukisimama hapo aliposema bado ilikuwa huwezi kunyoosha mkono na kuifikia swichi.
“Munil,” niliita.
“Abee mume wangu”
“Bado umenidanganya. We hapo hata ufanyaje huwezi kwenda pale kwenye ukingo wa kitanda ukanyoosha mkono na kuifikia ile swichi, iko mbali sana.”
Nilimwona Munil akiamka kitandani, akasogea hadi kwenye ukingo wa kitanda. Alinyoosha mkono na kuifikia swichi, akawasha ile taa! Tap!
Kusema ule ukweli nilishangaa sana, pia nilishtuka kwani nilichobaini ni kwamba wakati ananyoosha mkono kuanzia kiunoni kwake kwenda shingoni alirefuka sana na ndiyo maana aliweza kufika kwenye swichi.
“Oke, oke!” nilisema nikijifanya nimemwelewa lakini huku na mimi nikishikilia msimamo wangu kwamba alirefuka sehemu ya kati ya mwili wake.
***
Asubuhi ya siku iliyofuata, mimi niliamka nikiwa nimechoka sana, tena nilichoka kupita kiasi kwa hiyo sikuwa najisikia kutoka nyumbani.
Sikumbuki ni muda gani Munil aliamka lakini nilibaini tu kwamba alikuwa nje akiosha vyombo na kushughulikia mambo mengine.
Nilipoamka ilikuwa yapata saa nne asubuhi, nikaenda kwanza chooni kabla ya mambo yote. Niliweza kuona alama za kwato za wazi kabisa kutokea nje ya mlango wa kuingia kwangu kwenda chooni, bafuni na kutoka nje.
“Hivi inawezekana kweli hizi kwato ninazoziona ni za Munil mke wangu?” nilijiuliza mwenyewe lakini sikupata jibu lolote zaidi ya kuendelea kuhisi tu.
Moyoni nilijielekeza jambo moja kwamba, nikishaoga na kunywa chai niondoke kwenda kwa shemeji kumwambia hali halisi ya mke wangu Munil.
“Lazima niende na lazima nikamwambie anipe ushauri, huyu si mwanamke mzuri,” nilisema moyoni.
Basi, sasa wakati wa kunywa chai nilimwambia Munil nilipenda zaidi mayai kuliko mkate na siagi. Akasema anakwenda dukani kununua mayai.
Alipotoka tu, nikakumbuka tukio la jana yake la yeye kwenda kwenye ukingo wa kitanda na kunyoosha mkono mpaka kuifikia swichi ukutani na kuwasha taa.
Nilijaribu kufanya hilo zoezi, nilikwenda kwenye ukingo wa kitanda hicho nikajiegemeza na kunyoosha mkono ili kuifikia swichi lakini sikuweza hata kufikia robo!
“Mh! Si nilisema mimi!” nilijikuta nikitoa sauti hiyo mi mwenyewe.
Nilirejea kukaa kwenye kiti ili Munil asije akanikuta nafanya lile jaribio.
Alipoingia, Munil alionekana kuwa na wasiwasi na mimi na kile chumba. Aliangalia kitanda akaniangalia mimi kisha akaguna na baadaye kucheka sana.
“Unacheka nini sasa?” nilimuuliza kwa woga.
“Hamna kitu.”
“Hamna kitu wakati umecheka sana?”
“Jamani, kwani mtu akifurahi hacheki mume wangu?”
“Kwa hiyo wewe umefurahi siyo?”
“Nimefurahi ndiyo. Kama mume ninaye, maisha ndiyo haya, kuna nini tena?”
“Kifo je?” nilimuuliza kwa kumtega.
“Kifo sikijui mimi wala sijawahi kuona mtu amekufa wala kusikia kuna mtu amekufa japokuwa najua kuna kufa kwa watu.”
“Kuna kufa kwa watu? Una maana gani?”
“Nasema nasikia watu huwa wanakufa!”
“Ina maana wewe si mtu?”
“Jamani hilo si tulishawahi kulimaliza.”
Niliachana na mazungumzo na Munil nikawa nawaza tu jinsi nitakavyomshibisha shemeji na matukio ya Munil ambayo yalishaanza kunichosha sasa.
“Mume wangu,” aliita Munil wakati mimi nikiwa kwenye dimbwi la mawazo kuhusu vitendo vyake.
“Niambie.”
“Hivi unadhani kutoniamini mimi ni dawa ya kumwamini mtu mwingine?”
“Una maana gani?”
“Mi najua huniamini hata kidogo lakini sasa ungejaribu kuniamini. Unajua mnasema wenyewe kwamba kuku ukimchunguza sana huwezi kumla, si ndiyo?”
“Ndiyo.”
“Ndivyo kwangu na hata kwako pia, mimi nikitaka kukuchunguza sana siwezi kukufurahia. Pia nikwambie jambo moja mume wangu katika mambo ambayo siyapendi katika ndoa ni matatizo yetu kuwaambia au kuyaombea ushauri kwa watu wengine.”
Aliposema kauli hiyo nilishtuka sana nikamtumbulia macho.
“Una maana gani?” nilimuuliza haraka. Mimi nilichojua ni kwamba alishatambua mpango wangu wa kwenda kumwambia shemeji matukio yake.
“Natoa tu angalizo lakini sina maana yoyote mbaya au nzuri, mimi nipo tu. Ninapokuwa na ushauri kwako nakupa wakati wowote kama mume wangu, sikukatazi lakini kuamua ya kwako kwani wewe ni mume.
“Ukiona kama kwenda kwa shemeji yako na kumwambia mawazo yako kwangu atakusaidia sawa lakini ungejaribu kuwa makini kwanza kabla ya hiyo hatua.
“Pia sidhani kama kuna umuhimu wowote wa wewe kuendelea kuchunguza mambo yangu hadi kufikia hatua ya kujaribu kuwasha taa ya chumbani humu kwa kukaa kwenye ukingo wa kitanda kama nilivyofanya mimi, japokuwa najua lengo lako ni kuona wewe utaweza kama nilivyoweza mimi?”
Nilishtuka sana, kwani hayo yote, Munil aliyasema nikiamini hakuna alichokuwa akikijua kwani sikumwambia kwamba nitakwenda kwa shemeji.
“Munil nadhani hayo tuyaache.”
“Hapana mume wangu tunatakiwa kuyaongea ili tuyamalize.”
“Mimi nimeamua tuyaache.”
“Kama umeamua kwa dhati sawa.”
Nilimuaga Munil kwamba nakwenda kuonana na rafiki yangu mmoja halafu nitakwenda gereji ambako ni kazini kwangu akasema sawa ila nisichelewe kurudi.
Nilipotoka nyumbani niliamini namfuata rafiki yangu mmoja anaitwa Chamanilili lakini kabla sijafika kwa Chamanilili niliamua kupitia kwa demu wangu mmoja anaitwa Mayinu ambaye naweza kusema
tangu niwe na Munil ndiyo nilikata naye mawasiliano. Yaani Munil alichangia mimi kumwacha demu huyo.
Nilipofika kwenye nyumba aliyokuwa akiishi nilikuta pameota majani mengi, nikashtuka kwani hata kwa muda nilioachana naye hakukuwa na sababu ya nyumba kubomolewa kiasi cha kuota majani.
Nilijaribu kuangalia nyumba za jirani zote zilikuwa zimefungwa na wenyewe hawapo.
“Mh! Nini kimetokea? Halafu hata kama nyumba ilibomolewa mbona za majirani hakuna hata moja yenye watu au walihamishwa?” nilifikiria mwenyewe kichwani.
Nilitoka kuendelea na safari zangu, mbele nikakutana na Mayinu, uso wake ulipooza licha ya kuniona jambo ambalo sikulitegemea.
“Mayinu mbona umesinyaa hivyo?” nilimuuliza.
“Mbona kawaida tu.”
“Aaah! Si kawaida yako yaani hujaniona siku nyingi halafu leo kuniona unakuwa kama tulionana asubuhi tu!”
“Mimi nipo kawaida,” alisisitiza Mayinu akiwa amenifikia maana baada ya mimi kumuona nilisimama.
“Nyumba ilivunjwa?” nilimuuliza.
“Ipi?”
“Uliyokuwa unaishi?”
“Jamani, ivunje na nani sasa?”
“Mayinu mimi nimetokea pale.”
“Mimi nilitoka nusu saa iliyopita na ndiyo narudi. Sasa ivunjwe na nani na kwa ajili gani? Tena wakati natoka nyumba ya jirani kwa mama Ally walikuwa wanapika chakula kwa ajili ya genge lake.”
“Mimi sijaona nyumba, nimeona majani na jirani sijaona mtu yeyote zaidi ya nyumba kufungwa.”
“Pameota majani?! Au umekosea nyumba wewe?”
“Unadhani naweza kukosea nyumba yako?”
“Ndiyo nashangaa.”
Palepale nilianza kuhisi kuwa huenda Munil ana mkono katika tukio lile kwani niliwahi kuhisi siku za nyuma nilipokwenda kwa dada wa demu wangu mmoja yalitokea mauzauza.
“Kwa hiyo?” aliniuliza Mayinu lakini bado hakuwa na uso wenye nuru. Alionekana kama anaumwa.
“Basi ngoja turudi,” nilimjibu nikigeuka naye.
Tulitembea huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua kama kweli nilipotea nikaenda sehemu nyingine au kuna kitu cha zaidi ya ninavyojua mimi.
Kila hatua tano mbele iliashiria kuwa nilikuwa nimekwenda kwenye nyumba sahihi kabisa na wala sikupotea kama ilivyodaiwa na Mayinu.
“Ulipita hapa?” aliniuliza Mayinu.
“Ndiyo.”
“Hapa je?”
“Kote huku jamani, mimi nitapasahau nyumbani kwako kweli?”
Ghafla tulitokea kwenye nyumba yake, ikiwa ipo vilevile ninavyoijua, nikashangaa. Hata nyumba za majirani zilikuwepo na huyo mama Ally aliyesema alikuwa anapika chakula nje kwa ajili ya genge lake nilimuona akashtuka kuniona, akasema:
“Hee! Mwana mpotevu huyo.”
Nilimsalimia, akasema nimepotea hadi nimekuwa mweupe tofauti na zamani, akanikaribisha.
Mayinu aliniingiza ndani kwake, nikakaribia, akafunga mlango huku akisema:
“Umekuja kunipa penzi au kunisanifu nikoje kwa sasa?” Mayinu aliniuliza kama kwa ukali kidogo.
Ilikuwa kumuweka sawa nikaamua kumwambia nimekuja kukupa penzi.
“Kama umekuja kunipa penzi sawa, twende chumbani my dear, nimekumisije?”
Tuliongozana hadi chumbani, Mayinu akasimama, akanikumbatia na kuanza kunipa ulimi kwa muda wa dakika kadhaa mpaka nikawa nimepata moto.
Alinivua nguo, alipomaliza na mimi nikamvua nguo yeye kisha wote tukapanda kitandani.
Tuliendelea kuchezeana hapa na pale ili kuzidi kuchajishana. Mwishowe tukafikia kipindi cha kuanza
kwa mchezo. Mchezo ulikuwa mzuri, Mayinu alinikumbusha mbali sana huku na yeye akidai alinimisi kama mimi pia nilivyommisi.
Yeye ndiye aliyetangulia kumaliza hamu yake akaendelea kuniburudisha mimi ambapo pia nikawa nakaribia kumaliza hamu yangu. Nilipomaliza nilimwegemea kifuani kidogo nilipoinua uso baadaye ili nimbusu nikashangaa kumuona ni Munil.
“Ha! Munil,” nilisema kwa mshtuko mkubwa.
“Unajua wewe mwanaume hutosheki? Nakushangaa sana,” alisema Munil akinisukumia huko nikadondokea upande wa pili kwenye godoro.
“Munil mke wangu,” nilimwita kwa sauti yenye mtetemeko wa ajabu.
“Kwenda huko, hivi unajua kama mimi Munil nina uwezo wa kukutoa roho ndani ya dakika moja tu ukawa umesahaulika hapa duniani kwenu? Au unataka niseme nini kwako ili unielewe we mwanaume usiyekuwa na haya wala soni?
EPISODE 19 & 20
“Basi mke wangu, kwanza nimegundua kwamba hakuna cha siri nitakachokifanya halafu wewe usikijue.”
“Kwa hiyo kama ungefanya mimi nikashindwa kukijua ungekuwa unanisaliti kila kukicha siyo?”
“Hapana mke wangu.”
“Sasa nini? Nilishakuonesha ishara kama mara moja kwamba uachane na wanawake wengine nikajua umejua lakini sasa nahisi kuwa kumbe hukujua au ulijua bali ulipuuza.
“Uliwahi kufika motoni?”
“Sijawahi.”
“Kuna aliyewahi kufika akakusimulia kulivyo?”
“Hakuna.”
“Basi naomba uwe unatulia sana mume wangu. Najua wewe unasakamwa na shetani tu lakini usinifanyie hivyo mume wangu, kama ni utajiri tunao mkubwa sana mpaka unashindwa jinsi ya kuutumia maana tangu baba yangu amekupa zile pesa sijakusikia ukisema unataka kufanya biashara yoyote.
“Kwanza mimi naona hata mpango wa kupangisha nyumba ungekufa tukanunua kiwanja tujenge jumba la kifahari mbona fedha inatosha.”
“Ni kweli mke wangu.”
“Haya, twende nyumbani sasa.”
Tulivaa nguo na Munil, tukaondoka. Wakati tunatoka niliamini kwamba, nje nitamuona yule mwanamke aliyekuwa akipika chakula cha gengeni aliyenichangamkia lakini hakuwepo na mazingira ya nyumba yalikuwa yale ya mwanzo ya kuwepo kwa nyasi nyingi na nyumba kubomolewa.
Nilishindwa kumuuliza chochote Munil, nikaamua kumfuata kwa nyuma kama mbwa anayetembea na bosi wake kwenda mahali.
Nilitegemea maajabu kutoka kwa Munil njiani sikuyaona hadi tunaingia ndani. Nilipokaa tu akasema:
“Mume wangu najua kama una mipango mingi sana, nakuruhusu uende lakini akilini mwako ondoa suala la kunisaliti, sipendi hata wewe huwezi kupenda.”
“Ni kweli mke wangu, siwezi kupenda na nimefurahi sana kunisamehe kwako. Ila nakwenda kwa yuleyule rafiki yangu.”
“Nenda salama mume wangu, nakupenda sana,” alisema Munil akasimama na kunikumbatia kwa nguvu zake zote.
Niliondoka, nilitembea kwa kuinamisha kichwa chini kwani kitendo alichonifanyia Munil ni cha ajabu sana sijawahi kukisikia kwa watu wengine.
Kufika Kibaha mjini nilipata wazo la badala ya kwenda kwa rafiki yangu huyo niliamua kwenda kwa rafiki yangu mwingine anaitwa Isaya.
Isaya ni rafiki kaka kwani amekuwa akinisaidia mawazo na amenizidi umri. Kwa hiyo niliamini niende kwake kwa ajili ya kumwomba ushauri kwamba ni biashara gani nifanye na kiasi kile cha pesa nilichopewa ukweni kwangu.
Nilimkuta Isaya amekaa sebuleni na mke wake. Watoto walikuwa nje na ndiyo walionipokea.
“Eee bwana vipi, mbona umepotea namna hii rafiki yangu?” Isaya alisema akinishangaa. Akaendelea:
“Kwanza nakuona kama umenawiri sana, umepata pesa nini?”
Mimi nilicheka tu, nikakaa kwenye kochi huku mkewe akinikaribisha kwa furaha naye akidai hajaniona siku nyingi sana.
“Mimi nipo sana ila sema tu mambo yalikuwa mengi. Lakini katika yote naomba samahani kwenu kwamba nilioa bila kuwaambia.”
Walishtuka, wakatazamana. Isaya akauliza:
“Umemuoa nani?”
“Kuna dada mmoja anaitwa Munil.”
“Munil?” aliuliza haraka mke wake.
“Ndiyo shemeji, unamfahamu nini?”
“Hapana, ila kuna habari zimesambaa hapa Kibaha kwamba kuna kijana amefunga ndoa na jini. Sasa watu wanasema huyo msichana ni jini kwa sababu hajulikani alikotokea na ana mwonekano tofauti kabisa na wasichana wetu wengine hapa Kibaha.
“Nasikia anaonekana mara mojamoja sana akitembea mitaani. Na huwa anapendelea kuvaa magauni mpaka chini kabisa kwa vile hana miguu ya binadamu ana kwato kama za ng’ombe.”
Wakati mke wa Isaya anasimulia hayo, mimi mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kwa kasi nikijua
msichana anayesema hapo lazima atakuwa Munil. Kwa sababu gani? Hata mimi niliwahi kujiuliza kwamba tangu nimeishi Kibaha sijawahi kumwona Munil. Pia, sijawahi kumwona akiwa amevaa nguo nyingine mbali na magauni.
“Da! Shemeji si huyo,” nilisema kwa sauti iliyotoka kwa uvivu sana.
“Kwani huyo uliyemuoa wewe ni mtoto wa nani hapa Kibaha au ametokea mkoa?” aliuliza Isaya.
Itaendelea wiki ijayo.
“Hapana, kwao ni mkoa huuhuu wa Pwani ila wazazi wake wanaishi Bagamoyo.”
Niliposema hivyo wakatazamana tena, lakini Isaya kama akayumbisha mazungumzo kwa kusema:
“Mimi bwana kwa muda tulioachana niliamua kukata shauri na kuokoka. Kwa hiyo mimi na nyumba yangu tumeokoka na tunamtumikia Bwana!”
“Ooh! Ni vyema sana Isaya. Sasa mimi bwana nimekuja nina shida. Shida yangu nimepata vijisenti kidogo sasa ishu iko kwenye biashara. Je, nifanye biashara gani?”
“Mh! Labda kwanza ungesema umepata kiasi gani ndipo nikushauri.”
“Kama shilingi bilioni mbili hivi.”
“Hapana, kwao ni mkoa huuhuu wa Pwani ila wazazi wake wanaishi Bagamoyo.”
Niliposema hivyo wakatazamana tena, lakini Isaya kama akayumbisha mazungumzo kwa kusema:
“Mimi bwana kwa muda tulioachana niliamua kukata shauri na kuokoka. Kwa hiyo mimi na nyumba yangu tumeokoka na tunamtumikia Bwana kwa sasa!”
“Ooh! Ni vyema sana Isaya. Sasa mimi bwana nimekuja nina shida. Shida yangu nimepata vijisenti kidogo sasa ishu iko kwenye biashara. Je, nifanye biashara gani?” “Mh! Labda kwanza ungesema umepata kiasi gani ndipo nikushauri.”
“Kama shilingi bilioni mbili hivi.”
Isaya na mkewe walishtuka sana. Wakatazamana kwa macho ya wasiwasi. Ilionekana kama hawakuamini maneno yangu.
“Shilingi ngapi?” aliuliza Isaya huku akikaa sawasawa.
“Kama bilioni mbili hivi.”
“Haiwezekani!”
“Ndiyo nakwambia sasa.”
“Wewe, pesa yote hiyo umeitoa wapi? Umeiba?”
“Hapana, nimepewa na baba mkwe wangu.”
“Baba wa mkeo huyo uliyemuoa?”
“Ndiyo.”
“Mh! Shemeji hongera sana. Kumbe umeoa kwenye ukoo wenye uwezo mkubwa sana.”
“Ni kweli, mbona nimepewa na gari la kisasa, jipya, lipo nyumbani.”
“Kweli? Mbona huendeshi sasa?” aliuliza Isaya.
“Siendeshi kwa sababu zangu lakini kuna siku nitaanza kuingia nalo mitaani, si unanijua.”
Isaya aliniangalia kwa muda kisha akasema kwa kiasi hicho cha pesa hana biashara ya kunishauri kichwani. Alisema ni vizuri kama nitawaona wataalam wa uchumi wakanishauri nifanye biashara gani!
Tuliendelea na mazungumzo lakini nilipotaka kuaga, Isaya akasema tusali kwanza ili Mungu anibariki!
“Sawa,” nilijibu huku Isaya akisimama na mimi pia nikasimama sambamba na mkewe.
Alipoanza kusema Bwana tunakushukuru palepale nilijikuta chini. Nikaanza kutokwa na povu
kinywani huku nikirusharusha miguu huku najiona.Wale wenyeji walisogelea na kuanza kuniombea kwa kelele lakini baada ya hapo kilichoendelea sikukijua.
Nilipokuja kuzinduka, nilijikuta nipo kitandani, tena hospitalini.
Niliangaza pembeni yangu nikamwona Munil amesimama lakini uso wake ukiwa umekasirika sana. Hakukuwa na mtu mwingine zaidi yake.
“Pole,” aliniambia kwa mkato.
“Asante. Nini kilitokea?”
“Unaniuliza mimi! Mimi ndiyo nikuulize wewe nini kilikutokea.”
“Nani kanileta hapa?”
“Mimi sijui.”
“We ulijuaje kuwa nipo hapa?”
“Nilijua ninavyojua mimi mwenyewe.”
Kwa mbali nilianza kupata picha kwamba nilikuwa kwa Isaya, wakati nataka kuondoka akasema tusali, nikakubali na kusimama ndipo nikaanguka.
“Isaya yuko wapi?”
“Isaya ni nani?”
“Nilikuwa kwake.”
“Mimi sijamwona.”
“Simu yangu iko wapi?”
Munil alinipa simu yangu, nikaangalia namba ya Isaya, nikaipata na kumpigia.
“Haloo.”
“Halo Isaya, vipi bwana?”
“Sasa wewe mbona ulikimbia wakati wa maombi?” aliniuliza Isaya.
“Nilikimbia?”
“Ulikimbia. Mimi nadhani kuna kitu cha kujiangalia sana ndugu yangu, unakimbiaje maombi ya Bwana Yesu?”
Kabla sijamjibu, Munil alinipokonya simu, akaiweka loud speaker, akaanza kuongea yeye.
“Haloo.”
“Haloo, nani shemeji?”
“Mimi naitwa Munil na ndiye niliyemkimbiza mume wangu hapo nyumbani kwako. Wala usiwe na wasiwasi kuhusu yeye, ila nakuonya kuhusu mpango wako wa kutaka kufuatilia maisha yangu.
“Mimi najua mambo mengi tu kuhusu wewe. Mfano, wewe si umeokoka unasema? Lakini mbona una mwanamke kule stendi?”
Nilisikia simu ya Isaya ikikatwa ikalia tii tii tii! Munil alinirudishia simu huku akisema:
“Kwa hili mimi sina tatizo na wewe mume wangu kwani najua ulikwenda kwa Isaya kwa nia njema tu ila wao wanataka kunijua mimi ni nani ndiyo maana niliamua kukukimbiza pale walipoanza kuomba kwa sababu mimi sipatani na maombi”
“Na wala hapa si hospitali kama unavyojua, hapa tupo nyumbani, angalia.”
Kufumba na kufumbua, kweli nikaona nimelala kitandani kwangu, chumbani.
“Ha! Munil, haya mambo yakoje?”
“Haya mambo ni madogo sana mume wangu. Mimi ni binadamu mwenye uwezo mkubwa katika maisha. Hebu nyoosha mkono wako juu,” aliniambia Munil. Nikanyoosha mkono juu.
“Nyoosha tu.”Nilinyoosha tu, nikashangaa mkono wangu unarefuka hadi kushika paa la nyumba.”
Nini kiliendelea?