MCHUNGAJI AMENISHAURI NIZAE NA MUME WA MTU KWAMBA NAZEEKA
Naomba ushauri naomba ufiche jila langu kaka mimi nilikutana na baba mmoja mtu mzima akanitongoza akasema nataka niwe mke wake wa pili kwa vile mke wake wa kwanza amekua mtu mzima hawezi kuzaa tena mimi nikakubari basi kwa vile nilijua ni mtu mzima atakua amemaliza ujana maana ana miaka 59 sasa hivi mimi ni 29 basi akanipangishia nyumba tukanza kuishi pamoja nikamwambia basi twende nyumbani wakakufahamu akasema subiri ukijifungua tu nitaenda
Basi kuna siku nikawa nimekaa nae simu ikaita nikasikia sauti ya mwanamke na mtoto analia nikamuliza huyu ni nani akasema ni shemeji yangu anaomba msaada basi tukaendelea kukaa badae nilikua naenda nyumbani kujitazamia sasa nafika stendi namuona huyu mwanaume ameongozana na mwanamke wanaenda sokoni nikamuliza huyu badae nikamuliza huyu ni ni nani akanza kuona aibu akasema nimezaa nae tu nikamuliza wewe si ulikataa akasema niliona utachukia nikwambia sawa akasema lakini hata mke wangu wa nyumbani anajua kwamba nimezaa
Basi mungu akanisaidia nikajifungua mtoto wa kike basi kilicho nileta kwenu ni kwamba mimi nilikua nasali tu ile ili mradi lakini badae nikamua kuokoka kabisa nikamshirikisha mchungaji maisha ninayoishi na mwanaume wa mtu mchungaji wangu akasema huyu ndo mwanaume ambae mungu amekupa unafikiri utapata wapi mwanaume mwingine?
Nilikaa miezi saba bila kukutana nae kimwili nikaenda kwa mchungaji kwamba aniombee nipate mume sahihi akasema wewe unataka kumuacha huyu mwanaume ili uwe malaya uwe unadanga nikasema mimi naona kabisa natenda dhambi akasema hapana na hivi leo ninavokwambia mpigie simu umwambie aje leo alale kwako basi kweli nikafanya hivo akaja nikashiriki nae basi nikawa naenda sokoni nikakuta mahubiri yale maubiri utafikiri waliniona mimi nikAjikuta mwenyewe roho inanuma nikasema leo lazima huyu mchungaji mbona nimuelezee maisha yangu
Akaniambia kweli kwamba unakosea pakubwa inatakiwa utubu ubatizwe na maji mengi na huyo mwanaume uachane nae tukuombee upate wa kwako basi ikapita kama. wiki na hapo nimeamua haswa kwamba Mungu naomba unisaidie katika safari yangu ya wokovu ule mkutano ukaisha nikakaa kama wiki mbili nikajikuta nina ujauzito tena wa huyu mwanume nikamshirikisha mchungaji wangu akasema hapo tena mwanangu swala la kufunga ndo sahau mwanaume gani atakae kuoa ukiwa na watoto wawili?
Nikampigia yule mchungaji wa kwenye mkutako akasema huyo mchungaji wako anakukatisha tamaa wewe kama umeamua huyo mwaume achana nae msikilize Mungu atafanya njia pasipo na njia basi mimi nikamsikiliza huyo mchungaji wa mkutanoni najikuta nina amani nae akiniombea na kunishauri nilimwambia mwanaume kwamba mimi.nimeokoka kwahiyo mimi kushiriki tendo hapana na hapo nyumbani kwako nimeondoka akakasirika sana
Jamani yaani niko njia panda najikuta hii mimba naichukia kutoa nogopa yaani nipo njia panda jamani naombeni mnishauri msinitukane..

